TIARAEI ndiyo wapi? Au ina maana ya Ti Ar Ei? hihiiii Mie nilishachekwa kuwa sisi Watanzania tunaitamka vibaya R. Tunasema ARA badala ya AR... Sijui upi ni ukweli. Wakali wa lugha nijulisheni ili siku nyingine nijitete.
Huu ukabila mama naomba unisaidie. Mie najua tatizo lipo na inabidi liongelewe ila kuna wengine wanadai kuwa hiyo imesababishwa na HISTORIA ya nchi katika devide and rule..... Au mie nina KIHINDIHINDI nini? Maana Kizunguzungu Tanzania hakipo tena na sasa kwa mbali nahisi Kichagakichaga. Just asking.
Historia kwa kweli inachukua mkondo wake katika hii kitu, ila waliopata nafasi wakatake into advantage hasa kwa siku za karibuni ambapo wasomi wamekuwa wengi.
Na katika historia ya wachaga kuna mawili, moja ni kwamba walienda shule na hata ukiangalia hadi kufikia miaka ya mwanzo wa tisini, mkoa wa kilimanjaro ulikuwa ukiongoza kwa kuwa na shule nyingi za seko. Shycom ilikuwa ina idadi kubwa ya wachaga, sasa unategemea nini Bcom na na maexpert kwenye fani za fedha?
Pili, wachaga wanaweka mbele kujuana, na hivyo wenyewe hawamuweki mtu wao kwa memo tu, bali wanahakikisha ana vyeti vya kufaa. Tatizo linakuja kwamba kazi nyingi zilikuwa hazitangazwi, mzazi wako anamfuata baba yako waubatizo na kumwambia kuwa kijana kamaliza kusoma na anaupper second. Baba wa ubatizo au, shemeji, au jirani kule moshi, au mwanaukoo either kwa upande wa baba au mama anafanya mambo yeye mwenyewe au anaongea na jamaa zake hata kama sio wachaga kuhusu nafasi za kazi kwenye nafasi nzuri. Basi mwisho wa siku kijana anaambiwa aandike barua aombe position fulani anaisubmit na vitu kama hivyo. God knows better!
Huku kwetu tunaita tiaraei kumbe tunakosea eeh?