Enzi ulipokuwa boarding

Enzi ulipokuwa boarding

jamaa waliamua kuchukua wali kwenje ndoo na maharage kuweka kwenye loka,mbabe mmoja c akalipindua loka juuu chini,ndanio ya loka kulikua na nguo daflari nk,plus wali na MAHARAGE SITASAHAU SIKU IYO MMBABE WA KIKURYA KAPATA MJANJA WA KIFIPA C UNAJUA WANAANZA KUSOMA WAKIWA WAKUBWA ,
 
jamaa waliamua kuchukua wali kwenje ndoo na maharage kuweka kwenye loka,mbabe mmoja c akalipindua loka juuu chini,ndanio ya loka kulikua na nguo daflari nk,plus wali na MAHARAGE SITASAHAU SIKU IYO MMBABE WA KIKURYA KAPATA MJANJA WA KIFIPA C UNAJUA WANAANZA KUSOMA WAKIWA WAKUBWA ,
Ahahaah!story kama hii nilipewa na mdogo wangu aliyesoma pale Iyunga kwa kisusange!
 
Kuna jamaa alikuwa anaweza kubeba madishi mawili kwa pamoja, moja mkono wa kulia na lingine mkono wa kushoto. Jina lake Lobilo. Mwalimu mmoja alikuwa anafanana naye, hivyo akabatizwa hilo jina la Lobilo. Miaka mingi baddaya akabakia na hilo jina, analichukia, lakini bado wanamwita Lobilo. Akajaribu kila kitu, akalia parade ground, bado haikusaidia, amabakia Lobilo.
 
Me niliambiwa nenda bweni(jina kapuni) ukwamuulizie jamaa anaitwa Bunsen burner!!! LOH! Nilipofika hapo bwenini jamaa wanistukia kuwa

nimeingizwa mkenge nao wakanambia ametoka nimsubiri kama dakika sita hivi atarudi!! ndugu niliuza chai mpaka nikakoma, baadae ndo

wakanielewesha.. nilimind we acha tu.

Unaambiwa PULIZA TAA IZIMIKE (tube light hiyo; thanks MUNGU haikuwa ngeni kwangu)...unapuliza jamaa anazima kupita swichi!! Dlk 3 baadaye jamaa anawasha na anakwambia tena PULIZA IZIMIKE..............Mashavu yanaweza kukutoka kama mgonjwa wa SAFURA kwa kupuliza Jamaa ya FORM 2 inakuaangalia na kucheka saaaaana!!!!!
 
Unapewa SAFARI BOOTS zimechooooka; PIGA SIMU NYUMBANI WATAARIFU UMEFIKA SALAMA BOARDING NA MAISHA NI SWAFI KABISA🙂

Kosa kubeba sanduku la mbao au chuma!!! Wanakutania JENEZA.....Godoro la SUFU wanakwambia MAREHEMU!!!!!
 
Waliosoma KIZUNGUZI miaka ya 1985-1990 wanayajua haya🙂 Waficha TOP LAYER ndiyo ilikuwa MEDICINE YAO!!! VITABU; NGUO; VIATU NK VYOTE WALI NA TOP LAYER!!!!! Waliokuwa engineers wa zoezi wandai ilikuwa njia ya kuondoa uchoyo na urafi...Nadhani wanasiasa wetu wa siku hizi hawakumwagiwa misosi katika LOCKER ZAO🙂
 
dah issue kama hii tushafanyiwa na msukuma mmoja(maduhu jilili),tena ilikuwa siku ya sikukuu,jamaa ali sepa na pilau lote,mayai,matunda na nyama za vyuku zooote!

Hii jina kidogo inanistua!!! Wajina hilohilo tulikuwa naye shule sisi akiwa COUNTER anabweka kuwa kwa form 1 ratio anayogawa ya mboga ni KIKOMBE KIMOJA CHA MCHUZI KWA MAHARAGE MAWILI (2) punje!!!!!! Alikuwa anatekeleza asemayo; hivyo akigawa chakula unakuwa na maji ya harufu ya maharage (kuuita mchuzi kidogo si haki) na punje kama tatu za maharage!!! Huyu jamaa sijui kwake inakuwaje kwa sasa kwenye MENU (yuko hai nimekutana naye mwaka huu......)
 
Nakumbukuka niko sec Siha ,siku moja jioni kuna jamaa kutoka kigoma alienda kujisadia ,na alikuwa na Ada kwenye walet ghafla ikadondoka chooni,alikuwa form 6,akaanza kutindua choo kwa pembeni, akaingia na kuitoa ada ,bahati nzuri kulikuwa na vyoo vya kulenga set mbili.alinyoa nywele zote mpaka kwenye kope,he had a strange personality.

Hahahahaaaaahaaaa🙂 Strange personality!!! Kuna jamaa tulikuwa naye akaitwa DALTON kwa sababu ya hiyo STRANGE PERSONALITY🙂
 
Umenikumbusha chaka langu huko daah! Yaani ilikuwa ukitaka kutoka nje (kwenda town) lazima usingizie ugonjwa, hapo unaenda huko na barua kibao jamaa wameagiza upeleke kuzipost, so fan kupokea barua nyingi shuleni ilikuwa ndo umaarufu wako kila mtu atakufahamu, basi ilikuwa nikufanya juhudi kuwa na madem kibao ili upate barua nyingi! SIJUI KAMA SIKU HIZI KUNA MAMBO HAYO. WALE WA CHAKA LA TOSA WATAKUMBUKA PIA!

hahahahahaha....mzee wa kuosha...dah! barua zenyewe ziwe zinatoka iringa girls, bonge la ujiko! au list ya waliotumiwa pesa ikiwekwa ubaoni, duh! hahahahaah....umenikumbusha sana tosa kwa wanyama pori.
 
kwa wale wa MAGAMBA BOYS a.k.a GAMBIAN BULLS kule lushoto, kulikuwa na mtindo wa kupigwa fundo form 1 usiku, yaani jamaa anafunga peasi kwenye taulo halafu usiku ukiwa umelala unabondwa nalo kisha ukishtuka mtu keshasepa, ili kuepuka hilo inabidi daily uwe bundi darasani usome, au form 1 (njuka, ndama....kz) mnaamshwa saa6 usiku kwenda kuoga na kuna baridi ya kufa mtu, wengi sana walishindwa yale maisha ya unyanyasaji wakahama na wengine kuacha shule, tulivyofika form 2 ndio na sisi ubabe ukaanza. kwa kifupi shule nyingi sana za boarding enzi hizo zinafanana kitabia kabisa, shule za private nyingi zilikuwa hazina sifa coz waliokuwa wanaenda huko ni wale waliofeli msingi, gvnmt ilikuwa shule za vichwa tu, maskini asaiv shule za serikali zinaonekana majalala.
 
Nakumbuka jangwani enzi hizo, chakula kinapopakuliwa kinawekwa kwenye mabakuli makubwaa na kuwekwa kwenye kidirisha cha jikoni/dining. Sasa kile kipindi cha nzi wengi, mnapoenda kula, mabakuli ya mboga layer ya juu nzi watupu kama mchuzi na kama maharage, nzi na wadudu wametanda juu, so unaengua nzi, unatia msosi unaendelea kupiga menu, si mchezo. Na yale madisco ya welcome form five, wadada tunaalikwa kwa wakaka, ilikuwa poa sana.
 
Enzi hizoooo tupo makoko seminari tulikuwa tunasubiri kwa hamu kubwa ruhusa za kwenda mjini. Kila mwezi tulikuwa tunaruhusiwa mara moja tu. Basi siku ya siku ruksa ikishatoka ni kupiga mguu hadi town kama kilometa 6 hivi (hakukuwa na daladala) na siku hii ilikuwa ni kula tu migahawani kwa fujo ati twachenji dayati.
Kingine nakumbuka walivokuwa wanakuja wasichana wa kowak girls kwa debate nk aisee siku hiyo mesini ni mshike mshike manake watu tulikuwa twashindwa kula kushiba kisa mezani kuna masista du.
 
enzi hzo ndan ya ikizu.kipindi cha kiangaz maji yalikuwa ya shida sana.ikawa tunaoga mtoni,kwa kuwa hatukuwa na taulo tunatembea naked kuelekea skonga ili mkaukie njian mvae nguo hii ndiyo ilikuwa tabia.day moja tukiwa kama ppipo kumi na tana tuko naked tume tumejipanga njiani tumetoka kuoga na kufua mton kama kawa tukakutana na akinamama nao wanaelekea mtoni wako na watoto wao wa kike na kiume,hakuna aliyepisha njia walivyoona tuko naked halafu hatupishi njia wakakimbia.
 

Me nakumbuka 2livyokuwa golan(school) cku ya wal na nyama kuna jamaa 1 albeba wal wake akiendw dom kuula bas kuna jamaa mwngne akamgonga kwa baat mbaya bas ile saan yake ikadondoka na kujifunka chini,basi jamaa akamalizia 2 kumiminia mchuz palepale chini na akaanza kula mpaka anakalibia chini akaacha,daaaaaaaaaaah nlcheka balaaaaaaaaa
 

Me nakumbuka 2livyokuwa golan(school) cku ya wal na nyama kuna jamaa 1 albeba wal wake akiendw dom kuula bas kuna jamaa mwngne akamgonga kwa baat mbaya bas ile saan yake ikadondoka na kujifunka chini,basi jamaa akamalizia 2 kumiminia mchuz palepale chini na akaanza kula mpaka anakalibia chini akaacha,daaaaaaaaaaah nlcheka balaaaaaaaaa

Dah ebana ndiyo nimekubali, wali una heshima yake boarding schools hasa zile za serikali
 
Nakumbuka kwa raphael,kuna siku ticha aliniomba kwenda kumuuzia mchicha wake pale sokoni kituo cha kwa rafael,sijawahi kufanya business kama hiyo nakuambia ilikuwa noma sana kwangu.nilianza asubuhi kufika mchana saa sita nikarudi shuleni maana nilikuwa boarding pale Lyamungo.
 
pande za Kilosa Mkono wa mara sec nilianzia form one pale miezi sita tu nikakimbia. siku ya kwanza mdingi kanipeleka akaniacha na shs 200 hiyo ilikuwa 1989 dah kumwambia naogopa anasema si mnakula bure! imefika saaya kula mchizi km home na sahani ya plastic za kawaida kila nnaye pishana naye ana bakuli zile kuubwa za kuwekea maji basi wananishangaawe form one sasa hivi utakufa njaa kisahani gani hicho na kweli wiki moja tu na mie nikawa na bakuli hilooo. msosi wenyewe sasa ni dona na dagaa always, ule ugali uliitwa makana. dagaa hakuna kuchambua linafunguliwa gunia nusu linamwagiwa kwenye pipa la kupikia wakiiva wakati wa kula mnakutana na zile shells za konokono mchizi unatupa tu huko unaendelea kumanga. kulikuwa na jamaa yeye hana sahani wala bakuli la uji.miezi miwili ya kwanza uji ulipata sukari baadaye sukari ikaisha basi jamaa wanatuambia form one leo uji sumu wote lazima mfe! basi tunagwaya kwenda kuchukua hee punde jamaa wanaibuka na ndoo zile za lita kumi wamewekewa uji nusu ndoo kila mtu eti form one wamegoma kunywa uji sumu dah mpishi akatuambia uji sumu ni uji usio na sukari ikawa imekula kwetu.
 
Mkono wa mara tena kuna jamaa alikuwa hana sahani wala kikombe ila kaja na masanduku km manne hivi yale ya chuma. sanduku moja kajaza sukari km kilo kumi blue band na mazagazaga mengine km roiko mchuzi mix jingine jamaa kajaza samaki flani wanakaangwa na mawese halafu wanapakwa chumvi nyiiingi almaarufu km nguruka so wanakuwa wakavu. mchizi anachofanya wakati wa uji yeye anakuja mesini na blue band yake na sukari watu wanamgombania balaaa masharti yake anawawekea blue band na sugar mnamgawia uji bakuli zima. ikifika mcha time za dona mchini anakuja na nguruka wake wawili au mmoja mchizi atagombaniwaa balaa so mwisho wa siku jamaa ananawiri tuu.
 
Back
Top Bottom