gracious86
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 437
- 55
Nakumbuka enzi za afande miraji makongo basi kulikuwa na mti wa maembe karibu na canteen ya shule ile kuona maembe yameiva akajua kuna madenti waroho wa maembe basi akaandika kibao 'ANGUA EMBE' akakitundika juu yake. Looh hakuna hata dent aliyedhubutu kusogea karibu. Kulikua na matoz wa pre form 5 walikuja kurudia masomo kuona kile kibao wakajua ruksa wakapanda kuangua embe afande miraj akawakamata kwenda kuwapa adhabu wakajua ni kwenda kupewa msitu kufyeka cha kushangaza kawapeleka kwenye ofis yake ilikuwa banda la mabati mbele yake kulikuwa na kisima cha taka basi kawaambia nisubirin hapa aingia ndan karudi na redio kaweka Taarab(mipasho) akawaambia haya vidole juu na muanze kuimba atakae onyesha mautundu atasamehewa.ilkuwa very funy
mbavu sina jamani! Daaaah R.I.P miraji