Enzi ulipokuwa boarding

Enzi ulipokuwa boarding

Mkono wa mara sec baada ya miezi mitatu pale shule walinzi wa shule walikuwa wawili wote wakaugua, uongozi wa shule ukaamua kuwe na zamu ya kulinda ki mabweni pale shuleni. barabarani kabisa kulikuwa na dukacla ushirika na canteen baada ya hapo kuna ofisi za walimu na madarasa pembeni yake kuna mess hafu unapita mabweni ya wasichana mwishoni ndo wanaume. zamu yetu ilipofika bweni la uhuru mgao wa sukari ukawa umeisha so no tea usiku wachizi tukapiga akili tukagundua miezi hiyo mahindi na mihogo ndo imekomaa na mashamba yenyewe ni ya walim, na mwenyekiti wa shule tupo nae bweni moja na yeye ndo anatuchorea ramani ya shamba la mwl gani limemea zaidi tukizama tukiibuka tuna furushi la mahindi mabichi na mihogo tunachemsha usiku ni full kujiachia ikifika saa kumi wanafunzi wengine wanawahi kuamka kuja kukusanya kilichobaki. hatukuwahi kamatwa.
 
kwanza mdingi kanipeleka akaniacha na shs 200 hiyo ilikuwa 1989 dah kumwambia naogopa anasema si mnakula bure!

Hapo mkuu sina swali hahahaha lakini uchumi bado ulikuwa imara siku hizo

msosi wenyewe sasa ni dona na dagaa always, ule ugali uliitwa makana. dagaa hakuna kuchambua linafunguliwa gunia nusu linamwagiwa kwenye pipa la kupikia wakiiva wakati wa kula mnakutana na zile shells za konokono mchizi unatupa tu huko unaendelea kumanga.

Hapa sasa hata makoko seminari mambo yalikuwa ivo yani siku tukipikiwa dagaa ama samaki (vyakula hivi hata hivo ilikuwa ni nadra sana kupikwa) lazima ukutane na shells za konokono za kutosha dah

Pia hapa niyalete majina ambayo bado nayakumbuka

1 sani abacha - alikuwa form four na kiongozi wa jikoni, aisee mweusiiiii mfupiiiii kajazaaaaa kifua anatisha kama mnaijeria

2 sayusayu - form four pia mwembambaaaaa mrefuuuuuu alikua anatokea kijiji/parokia ya sayusayu hence his name

3 paroko - form six alikua balaa ktk basketball aiseee (cha ajabu hakua na mwonekano wa mchezaji wa basketball) 3points ndo ilikua zake nje ya D

Kabika - baba gombera (aka rector) wetu aisee alikua ni noma
 
enzi hzo ndan ya ikizu.kipindi cha kiangaz maji yalikuwa ya shida sana.ikawa tunaoga mtoni,kwa kuwa hatukuwa na taulo tunatembea naked kuelekea skonga ili mkaukie njian mvae nguo hii ndiyo ilikuwa tabia.day moja tukiwa kama ppipo kumi na tana tuko naked tume tumejipanga njiani tumetoka kuoga na kufua mton kama kawa tukakutana na akinamama nao wanaelekea mtoni wako na watoto wao wa kike na kiume,hakuna aliyepisha njia walivyoona tuko naked halafu hatupishi njia wakakimbia.
Dah!mlikua makauzu zaidi ya dagaa!
 
Mi nakumbuka wakati nipo Azania form one mwanzoni kabisa wakati bado ningali mgeni, kunu kibaba cha form IV kikaja kikanambia pale Azania wanaokwenda ni wale wenye akili nyingi na wanaojua English. Then kikaanza kuniongelesha vocabulary za Biology Chemistry na Physics ambazo sikuwa kabisa na ideasnazo, kilipoona sizijibu kikanambia nikipe sh 50 kabla hakijaenda kunireport kwa teacher on duty. Nilipokipatia kikasepa mazima, baadae sana ndio nikaja gundua lilikuwa ni changa la macho.
 
enzi hzo ndan ya ikizu.kipindi cha kiangaz maji yalikuwa ya shida sana.ikawa tunaoga mtoni,kwa kuwa hatukuwa na taulo tunatembea naked kuelekea skonga ili mkaukie njian mvae nguo hii ndiyo ilikuwa tabia.day moja tukiwa kama ppipo kumi na tana tuko naked tume tumejipanga njiani tumetoka kuoga na kufua mton kama kawa tukakutana na akinamama nao wanaelekea mtoni wako na watoto wao wa kike na kiume,hakuna aliyepisha njia walivyoona tuko naked halafu hatupishi njia wakakimbia.
Ahahahaaah!! Hii ni kali aisee...
 
Ebwana nimekumbuka, form one tulikuwa tunalala wa mwisho, ukifika muda wa kulala form one mnaanza kuimba wimbo wa Taifa huku unamshushia jamaa neti kama vile bendera.
 
Nyegezi seminary pale..kulikua na ticha mmoja kwa jina la Pasu..kwavile alikua anapenda msosi huyo kiasi kwamba alikua anataka kwenda pasu kwa pasu na wanafunzi haswa siku za wali kwa nyama au siku za sikukuu...basi siku moja alinikamata nimetoka kuvusha wali jikoni (baada ya kucheza deal na mpishi) kabla ya muda, akataka niende nae pasu..nikagoma. Kwa vile mwalimu Pasu pia alikua mpenda sifa, eti akataka mimi na sufuria langu la kichele twende kwa mkuu wa seminari (rector) ili nikajishitaki, hapo tifu likatoke, nikamkunja shati, kumtupia sufuria na kutokomea....ila usiku nikapata bakora za kutosha kutoka kwa rector!!!

maisha ya boarding kwa kweli yalikua si mchezo.
 
Ebwana nimekumbuka, form one tulikuwa tunalala wa mwisho, ukifika muda wa kulala form one mnaanza kuimba wimbo wa Taifa huku unamshushia jamaa neti kama vile bendera.
Ahahahahaaah!! Wapi huko?
 
Mi nakumbuka pale kibaha sec alikuwepo kiranja wa msosi mnoko na mbabe balaa.Alikuwa akikufuma unavusha msosi atakufukuza,atakukamata na kumwaga msosi wote kisha unapewa adhabu ya kudeki jikoni.Kuna siku kwa makusudi nilitoka na ki-sadolin kitupu chenye mfuniko nikajifanya navusha msosi mbele yake.Tulifukuzana umbali mrefu mpaka uwanja wa shule ndo akanikamata.Alipogundua chombo changu hakina msosi alimaindi ile mbaya,mi niliamua kumchosha tu!
 
dah! hii kali
 
Tehe tehe heeeh!! Ulimkomoa kwa kweli...
 
kwa wale walioxoma Ilboru kabla ya mgomo wa 2005 juu ya mxoc, ,. nadhani wanaikumbuka siku J4,., Hiyo ndo ilikuwa sikuu pekee ya wali(kitei). kwa member wengi hiyo ndo ilikuwa siku ya kuoga,,. maana baridi kipindi hicho ilikuwa si mchezo hasa kuanzia jun had agost,,. msox ni saa 12:30 lkn 11 njuka washapanga lyn,., ilikuwa ful burudani,,. chiefffff,.,. Kitemango,.,
 
Mh sitaki kabisa kukumbuka Rungwe sec.., majina kama mikia, salamanda, njuka yalikuwa yananikera mbaya, nakumbuka kuna viongoz walikuwa na tabia ya kuficha nyama. Sasa kuna siku 2nd master-Senya. Alizibamba na akatuita watu kama kumi hivi tuzile., asikwambie mtu tulizifakamia hzo nyama kama nusu ndoo ndogo,, wale viongozi walipokuja jion, waliduwaa kukuta nyama hazipo, waligawa msosi kwa hasira sana jioni hiyo.
 
Me niliambiwa nenda bweni(jina kapuni) ukwamuulizie jamaa anaitwa Bunsen burner!!! LOH! Nilipofika hapo bwenini jamaa wanistukia kuwa

nimeingizwa mkenge nao wakanambia ametoka nimsubiri kama dakika sita hivi atarudi!! ndugu niliuza chai mpaka nikakoma, baadae ndo

wakanielewesha.. nilimind we acha tu.

Ulikuwa shule gani Mkuu? Ya wazazi? Au kata
 
Nyegezi seminary pale..kulikua na ticha mmoja kwa jina la Pasu..kwavile alikua anapenda msosi huyo kiasi kwamba alikua anataka kwenda pasu kwa pasu na wanafunzi haswa siku za wali kwa nyama au siku za sikukuu...basi siku moja alinikamata nimetoka kuvusha wali jikoni (baada ya kucheza deal na mpishi) kabla ya muda, akataka niende nae pasu..nikagoma. Kwa vile mwalimu Pasu pia alikua mpenda sifa, eti akataka mimi na sufuria langu la kichele twende kwa mkuu wa seminari (rector) ili nikajishitaki, hapo tifu likatoke, nikamkunja shati, kumtupia sufuria na kutokomea....ila usiku nikapata bakora za kutosha kutoka kwa rector!!!
maisha ya boarding kwa kweli yalikua si mchezo.

Mkuu hiyo seminary ilikuwa na mashart ya namna gani ambayo ni rahisi kiasi hicho! Rafiki yangu Karumuna alisoma Rubya Seminary, yeye alikamatwa anakula embe moja bila ruhusa akaamriwa kula debe zima na alikula mpaka hsptl! Kwakuwa hakumaliza debe basi alipopona aliambiwa atakula maembe muhura mzima.......
 
Boarding, Musoma Alliance au Tec, nakumbuka Deputy HM Fundisha, alilkuta tunaoga wakati wa pared akatunyanganya nguo kisha akaanza kutuchana stick, mimi nilikimbilia upande wa Musoma mjini na wenzangu wakaelekea Mutex, jamaa lilinichagua mimi na kunifukuza hadi barabarani wakuu. Takribani 1.2 km huku watu wanashangilia kwa kuniona niko uchi. Sitasahau, kurudi ilikuwa issue. Afu jamaa halikumind tena
 
Ha ha ha ha haaaah!!! Pole sana mkuu!
 
IFUNDA TECH huko nako balaaa nakumbuka POLI/MSITU ambapo watu waliamishia madawati huko, tifu lilikuwa pale wanakijiji wanapochoma moto misitu mara SAA 9 USIKU Mnasikia king'ora cha shule kwenda kuzimaa motoooooooooo nyooo
 
<br />
<br />
 
duh ni noma kaka hasa ukijichimbia Kwenye msitu kule uwanjani pamesimama sana kaka, mi nilikuwa member mzuri
 
Back
Top Bottom