Enzi ulipokuwa boarding

Enzi ulipokuwa boarding

Hii mada inanikumbusha Nyakato sec.bukoba,tulikua na majina ya walimu kama,mwl.miloso, mwl.cadastro,headmaster(ndondocha) mwl.pokati,mwl.kamanda,mwl.zolo,mwl.kikonwe(mwalimu wa math) na mwanambuzi.sitasaau siku ya kuitumu tulipikiwa pilau bila CHUMVI! Tena tulikua tumewaalika Rugambwa girls,walituzomea na kuaidi kutorudi Nyakato.
 
bana nilikua kiranja sasa kuna kipindi tulikua 2nakagua vyoo wa2 wanaojisaidia bila kuflash bana. Ilikua ukikamatwa ni kesi unafukuzwa shule. Siku hiyo niko na mwenzangu tunapita 2kamcheck dogo m1 anatoka chooni tukawa 2naenda kucheck pale dogo alipotoka. Dogo alikua anasepa ku2ona aliruka akarudi akasukuma kinyesi na mkono ndani,nilibaki nimeachama 2kabidi 2mwache tu dogo..
 
Nakumbuka wakati nipo form 2 tulikua na tabia ya kuwatesa,kuwasumbua na kuwanyayasa form 1 ili kulipiza yale yaliyotukuta b4,kulikua na dogo wa form 1 mbishi kichizi kiasi kwamba alikua hapendwi na kila m2 aliyemzidi kidato.kwa hiyo kukawa na kampeni ya kumuadhibu,mara kitanda chake kime mwagiwa maji,kimepakwa upupu,wa2 wanakata godoro kusafishia viatu,kuchambia nk.Ikabidi aombe uhamisho lakini kabla ya kuondoka alitaka kulipa kisasi.Basi usiku watu tumetoka prepo genereta limezimwa watu tumelala halfu mvua inayesha tukasikia m2 anapiga kelele za moto,moto,moto.utaratibu ulikua ukishasikia hiyo mbiu toka fasta bwenini,watu na mabegi yetu,magodoro,mizinga tukatoa kwa kasi kuviokoa kwa moto halaf baada ya muda tukakuta kimyaaa wala hatuoni moto wala moshi.Ikabidi tufuatilie chanzo cha hiyo sauti, tukamkuata yule dogo amewka headphone masikioni,walkman mfukoni anayarudi mangoma ya kiafrica (africa moto,moto,afrika moto).tulitaka kumtembezea kipigo lakini bahati yake patroni alikua on time.Ila sita msahau
 
Sec Nimesoma dogo ambaye babake alikuwa ni kamanda wa Polisi mkoa wa kinondoni alikua Na Tambo, maringo balaa ,anajibu wakubwa ovyo ovyo,na akasema mtu akimgusa ndo watajua maana ya Babayake kuwa polisi kamanda,tunafunga lizofupi sept skuli we had a "biogas" na huwa inatoka kutengeneza ile gesi kuna Kundi lilikuwa linajiita "Wire" walimwagia urojo wa biogas dogo usiku wa maanane Dogo aliporuka kitandani hakuunekana tena shule kaacha kila kitu!
 
ahahahahah....enzi hizo Tabora boyz..kulikuwa na chemba moja katika bweni la mkwawa inaitwa university..mle tulikuwa tunalala pipo kama kumi na moja hivi tukiwemo viongozi..mke wa headmasta jina la utan nyumelo alikuwa na tabia ya kuja kutuamsha asubuh na mapema mabwenini..siku hiyo kaja kakuta pipo zote zimelala naked chemban coz tulipanga tumkomoe...ahahah yule mama eti akasema wala hatishiki coz keshaona kubwa zaidi ya zetu..mwee..but atleast alipunguza kuja akawa anaishia bweni kuu...vituko vya mesini hasa siku za nyali aka ubwabwa we acha tu..
Yule mama kauzu kweli, siku moja alinikuta nafagia nyuma ya bweni la sina acha anizodoe,'lione form five lizima halijui kufagia' nami nikamjibu nilikotoka kulikuwa na wafanyakazi wa shule ndo walikuwa wanafagia, halafu yule mama hawapendi a-level hasa form five mara atawambia 'yaone yanazuzuka na maghorofa' wakati maghorofa yenyewe magofu sijui sahivi kama yashafanyiwa ukarafati.
 
nyingine sitasahau pale milambo walivyotuvamia, siku hiyo tulikuwa kama watatu tunatoka kuangalia mpira kwenye bar ya mrema kule chini karibu na majumba sita, bahati mbaya umeme ulikatika halafu kulikuwa na bonge la mvua sasa wakati tunarudi njia yote imejaa maji halafu giza radi ikipga ndo inatusaidia kuona,tulivyokaribia dispensary tunaelekea bwenini SINA tukaona watu wengi wanakuja upande wetu, wenzangu wakasema ni wanajeshi mie nikawambia wanajeshi gani hawana uniform kumbe na wenyewe wameshatuona wakaanza kupiga kelele hao! hao!, tulislide hadi bweni la lower school na bahati mbaya mmojawetu alikuwa na matatizo ya kifua alikimbia kufika kwenye lile bweni hawezi kupumua vizuri ilibidi tumpepee ili apate hewa, da ilikuwa sekeseke.
 
Kuna dogo alikuwa anaitwa Silvesta Kimati alikutwa kwenye mashamba ya shule amezimia babaake alikuwa Ticha pale. 1 april ni noma kwa form one.
 
Nakumbuka wakati nipo form 2 tulikua na tabia ya kuwatesa,kuwasumbua na kuwanyayasa form 1 ili kulipiza yale yaliyotukuta b4,kulikua na dogo wa form 1 mbishi kichizi kiasi kwamba alikua hapendwi na kila m2 aliyemzidi kidato.kwa hiyo kukawa na kampeni ya kumuadhibu,mara kitanda chake kime mwagiwa maji,kimepakwa upupu,wa2 wanakata godoro kusafishia viatu,kuchambia nk.Ikabidi aombe uhamisho lakini kabla ya kuondoka alitaka kulipa kisasi.Basi usiku watu tumetoka prepo genereta limezimwa watu tumelala halfu mvua inayesha tukasikia m2 anapiga kelele za moto,moto,moto.utaratibu ulikua ukishasikia hiyo mbiu toka fasta bwenini,watu na mabegi yetu,magodoro,mizinga tukatoa kwa kasi kuviokoa kwa moto halaf baada ya muda tukakuta kimyaaa wala hatuoni moto wala moshi.Ikabidi tufuatilie chanzo cha hiyo sauti, tukamkuata yule dogo amewka headphone masikioni,walkman mfukoni anayarudi mangoma ya kiafrica (africa moto,moto,afrika moto).tulitaka kumtembezea kipigo lakini bahati yake patroni alikua on time.Ila sita msahau

Nimecheka sana, ahsante kwa kuleta mchapo huu
 
Mambo yalikuwa Tosa na mzee mwenyewe wa maheadmaster Mkangwa nilikuwa nimenyoa style wanaita funk sasa pembeni nilikuwa nimekwangua ikawa kama upara design tukaonana mjini siku shule inafungua ile kunitazama nikajua ishakuwa soo kila siku natokea assemble nimepaka masizi kumbe bwana jamaa alishanifeed kwenye memory yake alikuja staight akanidakua nilikula makofi ya ajabu.
 
hahaaaa! siku hiyo sasa ndani ya MALANGALI HIGH SCHOOL! kitu cha wali nyama ilikua mara mojamoja kchizi, jamaangu akadokoa nyama katika sahani ya mwenzake. yule mshikaji ambae nya ilidokolewa kutok sahani yake akaachia sahani yopte ya wali na nyama zilizobaki ikadondoka chini eti kisa anangangania ile nyama moja iliyo dokolewa...........!

nimeipata hiyo mzee wa mgl........malangali shule yetu kweli tunaipenda sana.....haka kawimbo kunawakati nilikuwa namung'unya tu na ikitokea watu wanaenda ubeti wa mwingine nasikika peke yangu na sauti yangu haieleweki ni ya ngapi.....na kero zaidi bweni letu la mwaisela kuna mshkaji alikuwa na miguu inatoa harufu basi watu tukawa tunapeana zamu tu akilala tu mnavitoa viatu vyake nje.......sasa kazi akichelewa kutoka prepo na wewe ndiyo zamu yako utajiona unalazimisha usingizi usije ili kumsubiri arudi......na hata wale mabingwa wa wizi wa viatu pale ilikuwa kikomo.
 
Wazee wa mazengo Mpoooo? Kwa Kweka usiombe, Nilikuwa nakaa lile Bweni la Askofu, na yule mwalimu mwingine, yeye alikuwa anafundisha olevel Kithungu ilikuwa zero, sasa akawa anatoa Speech of a day...." Dear students, we intruce to you a new timetable of Makande, chew it then tell us" akimaanisha kaeni muijadili halafu tuambieni kama inafaa..alikuwa anafundisha drawing, akiwa na kitu cha kuchora, anavizia madent wakiwa hawaangalii then anachora faster kinoma, then anatambaa zake kama vipi madent ndo waende kuomba wachore.....Jina simkumbuki...headmaster yeye, ngoma iliwatuma madent kwenda kuiba viti dom sec, vilipoingia tu vilipigwa chapa ya mazengo, headmistress alipokuja akaambiwa angalia kama kuna kiti chako...all mazengo sec school...

mazengo complex....tupo sana tu nakumbuka yote hayo kumi ng'ombe wa shule wakati fulani aliibiwa na wezi wamifugo na tukaamrishwa saa kumi ya usiku tuanze msako cha ajabu wengine walitembea hadi msalato girls na wakaingia hadi mabwenini kutafuta ng'ombe kazi ilikuwa kurudi wakati makundi mengine yamerudi saa 2 sisi tulirudi saa 8 na njaa vijasho vikitutoka......boarding naitamani kinoma.
 
Me nakumbuka mkwawa bweni la magembe east ulifanyika uchaguz kumchagua headgirl basi 75% tukamchague mke wa mwl mgaya (baunsa) basi tulidundwa mbaya na kwenda kusomba mavi choon kwenda kumwagia shambani. Jaman those days! Ukienda makanyagio unavaa koti refu na mzula then unapiga mluzi Mgimwa asikushtukie au ngui na Masebo. Waziri wa sheria Fungamtama, Watosamaganga jmosi kuja kuvizia wali.
 
PUGU BOYZ bana kulikuwa na mwalimu anaitwa mabags...habari yake ilikuwa kubwa coz siku akivuta bange yake mnakimbizana kwanzia alfajiri hadi mda wa parade
 
Basi bwana,nakumbuka kibaha secondary,form five wakiwa wamejipumzisha kwenye nyasi,alipita mdada mmoja kuelekea nyumba za walimu.Jamaa mmoja akarusha kete akaanza mtongoza.Yule dada alikataa hata kusimama.Basi yule mshkaji pamoja na wenzie kadhaa wakaanza ku-rap matusi,'ishia uko,miguu yenyewe chaga,sura ya babu yako,hebu ishia huko na umbo lako la simba'.Yule aliondoka huku akimwaga mchozi balaa.Dah!kumbe alikuwa mdogo wa mke wa mwalimu wa nidhamu,basi tukiwa parade jioni kwa ajili ya roll call,yule dada naye tii mbele ya parade.Akaambiwa apite kuwatambua waliomtukana,yule dada sijui mawenge,'to everybody's suprise,alimtaja mshkaji mmoja bonge la mlokole miongoni mwa waliomtukana!Ikawa hana jinsi,jamaa akaenda piga adhabu bila kosa lolote!
 
dah ucpime, TARIME SEC kulikua na dogo mchawi toka ukerewe, siku moja mpirani c akakwatuana na mshikaji pande la mtu mkurya, huwezi amini alimtupia mwenzie radi, Mungu mkubwa mshkaji akapona!
 
Enzi hizo headmaster nani, mr mbao? Nakumbuka ili kutatua tatizo la purukushani za chakula mesini makanyagio ilikua kimbilio langu la kudumu asubuhi, mchana na usiku.

Enzi hizo za Mbao, makanyagio ndio ilikuwa kimbilio kweli!!
 
Mi nakumbuka mwaka 1994 tukiwa sengerema secondary a.k.a Singapore, ile tunaingia form 5 kuna mwalimu mmoja tulimkuta anaitwa mwalimu BUGA.kumbe bwana lilikuwa jina la utani...siku moja akanikamata sijaenda parade, basi akawa ananiuliza namjua yeye ni nani? me kwa kujiamini nikamwambia wewe si mwalimu BUGA.. aiseeeeeee nilichezea kichapo cha hatari..kumbe bwana BUGA lilikuwa jina la utani,,kwa vile alikuwa anavaa suruali zile BUGA..yaani ile juu imebana afu chini umemwagika..ahahaha sitasahau kabisa..

Hii imenikumbusha mbali sana, yaani nimecheka hadi basi!
 
enzi hizo Mtwara Tech. kulikuwa na mpishi mmoja Anaitwa TOZI,
Kukiwa na Muziki tunawaalika Mtwara Girls(Mangamba). TOZI lazima azamie muziki.
Wakati anatongoza msichana akimuuliza anasoma kidato gani , yeye anajibu nimwalimu
wa Chemistry..!!
Angalizo: hilo neno Chemistry , Che inatamkwa kama ilivyoandikwa si ke.
 
Mi nakumbuka nikiwa kantalamba sec. O'level, nikiwa form 1, 2. ikifika usiku saa 9, mimi na wenzangu 7 tuliokuwa tunalala bweni moja, tunaenda kuiba miwa shambani kwa mwalimu. Siku moja akawa ametuvizia, tumeiba tupo njian kuelekea uwanjan kula miwa, (ilikuwa mitamu, na ile baridi ya saa 9, 10 usiku) sisi tumebeba miwa kumbe yeye yupo nyuma yetu amebeba panga na tochi peke yake. Kutuona tupo kundi akaishia kupiga filimbi, na kupiga mayoe ya mwizi akaogopa kutufuata. Woga tukakimbia tukajikuta tumezama kwenye dimbwi la maji machafu ya choon, na maji hayatoki, Kesho yake ni j3, mwl. wa zamu ni huyu tunayemwibia miwa. Ilitubidi twende mton usiku huohuo kuoga, zaidi ya km. 2. tumetoka mbali. In those dayz
 
KWIRO HIGH SCHOOL.Visa vilikuwa vingi sana.Kikubwa ni siku ambayo ulipikwa ugali badala ya wali..,Palikuwa hapatoshi.Mwalimu wa malezi alikuwa anaitwa DARAJA alilazimisha watu wale toka sa 12 mpaka sa 2 usiku bila mafanikio.Ndipo mkuu wa shule alipoamuru wali upikwe na ugali wakachukua wafugaji wa nguruwe!Fm 5 ndo walipika wali uioliwa sa 9 usiku watu weng walikuwa wamelala.Ila wali ulikuwa mtamu sana.
 
Back
Top Bottom