Enzi ulipokuwa boarding

Nakumbukuka niko sec Siha ,siku moja jioni kuna jamaa kutoka kigoma alienda kujisadia ,na alikuwa na Ada kwenye walet ghafla ikadondoka chooni,alikuwa form 6,akaanza kutindua choo kwa pembeni, akaingia na kuitoa ada ,bahati nzuri kulikuwa na vyoo vya kulenga set mbili.alinyoa nywele zote mpaka kwenye kope,he had a strange personality.
Du huyo jamaa kiboko...
 
Kwanjeka noma,kuna mother mmoja tulimkamata mwanae kwa wizi wa viatu,alipotonywa kuhusu mwanae kukamatwa na wanafunzi,alikuja mkuku na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine,wote tulitoka nduki tukamwacha yeye na mwanae.

Umenichekesha sana!!

Nakumbuka pale Mzumbe SEC ukiumwa Malaria unapewa SOFT DIET(Wali topetope na kabichi). Basi watu tulikuwa tunaumwa kila siku. Tatizo sasa mpaka Daktari wa shule(hata sio daktari), akuandikie(21days SD). Hapo ndugu chereko tu hahaha
 
dah!!mnanikumbushaaaa kitambo sanaaa hiyo shinga sec...ma usangi banaa,TULIKUWAA VIBAKAA SANAA,MAGODORO,MASHUKAAA,BLANGETI TUNAENDAA KUUZA KIJIJINI,day mojaa nikaa ibaa viatu banaa vya bitozii mmoja bana saa chini nilikuwa nimevyaa lapa nilivyo zama dom nikavua lapa nika pigaa viatu malapa nimeshika mkononi naenda mtoni,kufika mtoni nikavua viatu nikavyaa lapa nikazama kijijini kikweni kuuza banaa,hahaha mzee kumbe kuna jamaa mmoja mnoko kinoma aliona tukio lote...kachala na rudi na kama elfu tano,nshakunywaa denge nakuta watu wanadiskasii hiyo issue,kwavile nilikuwa mtemi nika enda kijiji nikaja na sime...nikapanda prepo,saa kumbe wame pangaa tukirudi dom wanianzishie bifu.mwananguu sitasahau...nilipigaaa watu bapaaaaa mbayaaa,dah!!ikawaa mwisho wa kusomaa hapo tenaaa
 
kwa wale wa aza boy kwa mkuu Kwayu ..tulio kuwa hostel..full kuibiana ili upate hela ya kula chips jangwani...
 
Umenikumbusha chaka langu huko daah! Yaani ilikuwa ukitaka kutoka nje (kwenda town) lazima usingizie ugonjwa, hapo unaenda huko na barua kibao jamaa wameagiza upeleke kuzipost, so fan kupokea barua nyingi shuleni ilikuwa ndo umaarufu wako kila mtu atakufahamu, basi ilikuwa nikufanya juhudi kuwa na madem kibao ili upate barua nyingi! SIJUI KAMA SIKU HIZI KUNA MAMBO HAYO. WALE WA CHAKA LA TOSA WATAKUMBUKA PIA!
 
Moshi tech enzi izo siku ya wali ukijaziwa sahani uwezekano wa kuipoteza au kukuta punjepunje ndo zimebakia ulikuwa mkubwa. Siku moja tumeingia mesini kwa kugombania tukajikuta tumeizunguka meza ila kuchukua sahani zetu ilikuwa insue,meza ikawa ina move kutegemea na upande unaokuwa weak. Nyali ikawa inamwagika na plate nyingine zinaibiwa apoapo na mwizi unamuona ila kutoka na kumkamata haiwezekani. Ku miss wali ilikuwa kawaida. Maisha ya bording ni hadithi tosha kwa wanangu
 
Mkuu umegusa penyewe, namkumbuka "Braza" Mpande na mambo yake ya kuja kuamsha watu kwenda mchaka mchaka. Kuna siku alikuja na kali ya mwaka: Eti akiwaona watu mjini alikuwa anawakariri uso, sasa watu wamegundua wakimwona tu wanageuka upesi na anashindwa kuwakariri uso, basi akasema atakuwa anakariri visogo. Baada ya majuma kadhaa akasema wanafunzi wakimwona basi wanageuka na kuvua mashati wanayafunga kichwani ili kuficha visogo, sasa akasema basi nitakuwa nakariri (ashakum siyo matusi) ******, nikiliona linaenda hivi au hivi basi nitajua ni la fulani,,, alikuja kutuacha hoi siku alipo-prove jinsi mbinu yake inavyofanya kazi kwa kumtolea mfano jamaa mmoja aliyemwona town Moshi,,

Yule Mwalimu sintokaa nimsahau aisee..
 
Nakumbuka siku moja nikiwa o-level form 1 kibaha sec,si unajua ule utaratibu wa misosi,watu kadhaa mnaunda kikosi,maybe watu 13 mnakuwa na dishi lenu moja la ugali/wali na moja la mboga.Ugumu ulikuwa unatokea ikifika zamu yako,unafuata msosi jikoni,unagawa kwa wenzio na kuosha madishi na kuyarudisha jikoni.siku moja jamaa alipojua ni zamu yake akaamua kutokuja kabisa.Tulikuwa form one 5,form two 4 na form four 2.Form four mmoja akashauri form one(nyoya,salamanda,nyoka) mmoja ajitolee lakini tuligoma wote.Wale form iv walijitolea ku-save msosi,ila walichofanya sitasahau.Waligawana msosi wao wawili wakatosheka,baada ya hapo walimwaga wali wote uliobaki chini na mchuzi wakaugeuza maji ya kunawa,kiufupi tulipigwa dash.Dah!vp wewe ulipokuwa form one,tupe kisanga kilichokukuta!
Kama kuna mtu alisomea Monfort Secondary school,,,,,, huko Rujewa kama wapo,, pls naomba PM.
 
Nakumbuka siku moja nikiwa o-level form 1 kibaha sec,si unajua ule utaratibu wa misosi,watu kadhaa mnaunda kikosi,maybe watu 13 mnakuwa na dishi lenu moja la ugali/wali na moja la mboga.Ugumu ulikuwa unatokea ikifika zamu yako,unafuata msosi jikoni,unagawa kwa wenzio na kuosha madishi na kuyarudisha jikoni.siku moja jamaa alipojua ni zamu yake akaamua kutokuja kabisa.Tulikuwa form one 5,form two 4 na form four 2.Form four mmoja akashauri form one(nyoya,salamanda,nyoka) mmoja ajitolee lakini tuligoma wote.Wale form iv walijitolea ku-save msosi,ila walichofanya sitasahau.Waligawana msosi wao wawili wakatosheka,baada ya hapo walimwaga wali wote uliobaki chini na mchuzi wakaugeuza maji ya kunawa,kiufupi tulipigwa dash.Dah!vp wewe ulipokuwa form one,tupe kisanga kilichokukuta!
Mkwawa high school kwa sisi tuliosoma o level seminari tulipata shida sana nyakati za mwanzo kusoma na mabinti hasa nyakati za prepo. Kombolela hasa siku za jumatatu katika mabweni ya wavulana...
 
Daa wanajamvi mie nakumbuka tulipo fika 2 form one pale Mazwi secondary, tulikumbana na kwataa kwa wiki sita nakumbuka jamaa walitupigasana mabuti na mitama
 
Time niko Lindi Sec, kulikua kuna miti ya Maembe dodo. Muda wa kuiva, hata uamke saa ngapi hukuti kitu kimeanguka. Unashindwa elewa washkaji wanaamka saa ngapi. Ila asbuhi kwenye uji unaona wana madodo safi wanakula na mchana hivyo hivyo. Mshikaji mmoja siku hiyo akavaa shuka nyeupe mwili mzima. Akapanda juu ya mti, naamini alikaa kama masaa hata mawili au matatu. Mshikaji alipokuja kuokota jamaa kule juu akajitingisha, kuangalia juu akajua ni shetani. Alipiga makelele, nduki bwenini. Mshikaji akashuka fasta akavua lishuka na yeye kurudi dom. Watu wakawa wanaogopa kwenda usiku tena, mshikaji akawa anakula yeye tu madodo. Watu wanaulizana kulikoni huyu mshikaji, inamaana yeye ndo haogopi? Mwishoni kabisa ndo akasema, yeye ndo alifanya ule ushenzi........

Boarding zilikua nzuri. Nikiwa table leader siku ya nyama tu nilikua napakua mm....... zingine zote na-delegate kwa nyoyaz/njukaz...........
 
hahaaaa! siku hiyo sasa ndani ya MALANGALI HIGH SCHOOL! kitu cha wali nyama ilikua mara mojamoja kchizi, jamaangu akadokoa nyama katika sahani ya mwenzake. yule mshikaji ambae nya ilidokolewa kutok sahani yake akaachia sahani yopte ya wali na nyama zilizobaki ikadondoka chini eti kisa anangangania ile nyama moja iliyo dokolewa...........!
 
pale KIBITI SEC SCHOOL Kulikuwa na ticha wa kike ambaye ilipokuwa zamu yake hupita kila dom kuwaamusha madent, basi bwana ipo cku tukakubaliana kwamba tulalapo hamna kujifunika shuka, hamna kushusha net wala kulala na nguo yoyote ile ikiwemo CHUPI, Alipokuja maadam karudi mbio akipiga makelele na toka ck hyo alikata mguu kuamsha watu
 
Mi nakumbuka mwaka 1994 tukiwa sengerema secondary a.k.a Singapore, ile tunaingia form 5 kuna mwalimu mmoja tulimkuta anaitwa mwalimu BUGA.kumbe bwana lilikuwa jina la utani...siku moja akanikamata sijaenda parade, basi akawa ananiuliza namjua yeye ni nani? me kwa kujiamini nikamwambia wewe si mwalimu BUGA.. aiseeeeeee nilichezea kichapo cha hatari..kumbe bwana BUGA lilikuwa jina la utani,,kwa vile alikuwa anavaa suruali zile BUGA..yaani ile juu imebana afu chini umemwagika..ahahaha sitasahau kabisa..
 
sijawahi cheka kama leo. yaaani
 
nakumbuka seminarini..ilikuwa huruhusiwi kuokota matunda ule mwenyewe..ukishikwa lazima ununulie shule nzima matunda..hapo ''pocket money'' yote lazima umalize..dah sitonsahau!!!
 
Mimi nakumbuka nilikuwa nasoma Lake Secondary Mwanza tulikuwa form two nilikuwa na rafiki yangu mmoja mdosi anaitwa Raju, alikuwa noma kwa kupiga nyeto kwa siku alikuwa anapiga nyeto mara tatu au mara mbili, uwezi kuamini ukimuona alikuwa mpole sana lakini kwa nyeto balaaa!!
 
Mkuu umegusa penyewe, namkumbuka "Braza" Mpande na mambo yake ya kuja kuamsha watu kwenda mchaka mchaka. Kuna siku alikuja na kali ya mwaka: Eti akiwaona watu mjini alikuwa anawakariri uso, sasa watu wamegundua wakimwona tu wanageuka upesi na anashindwa kuwakariri uso, basi akasema atakuwa anakariri visogo. Baada ya majuma kadhaa akasema wanafunzi wakimwona basi wanageuka na kuvua mashati wanayafunga kichwani ili kuficha visogo, sasa akasema basi nitakuwa nakariri (ashakum siyo matusi) ******, nikiliona linaenda hivi au hivi basi nitajua ni la fulani,,, alikuja kutuacha hoi siku alipo-prove jinsi mbinu yake inavyofanya kazi kwa kumtolea mfano jamaa mmoja aliyemwona town Moshi,,

Yule Mwalimu sintokaa nimsahau aisee..
Tanga tech kuna kiumbe mmoja anaitwa mdoe alikuwa mwalimu wa nidhamu.Yeye mkikumbana kitaa iwe makorola,kwanjeka,sahare,raskazoni beach n.k,ukimkimbia hata akikuona kisigino au kisogo,utamsikia anavyobweka nyuma,'wewe ni goodluck johnson lema,unaishi bweni la twiga,dorm C,cube namba 3,kitanda namba 245,Form V PCM 3,kesho tuonane uwanjani ukiwa na kwanja.
 
Mimi nakumbuka nilikuwa nasoma Lake Secondary Mwanza tulikuwa form two nilikuwa na rafiki yangu mmoja mdosi anaitwa Raju, alikuwa noma kwa kupiga nyeto kwa siku alikuwa anapiga nyeto mara tatu au mara mbili, uwezi kuamini ukimuona alikuwa mpole sana lakini kwa nyeto balaaa!!
Ahahahaaah!!!
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom