Habari wakuu.
Poleni sana kwa majukumu, Hoja yangu ni kwamba imefika wakati nataka kuoa sasa, ila sasa imebidi niulize kwa mliooa. Mmepataje wake wakuoa? Maana toka nipate wazo la kuoa nimekua nazurula sana maeneo mbalimbali nikiamini nitakutana na anayenifaa, hii hali imenifanya hata nikiwa nyumba ya ibada nisiwe makini na ibada bali nakagua mke, hata nikiwa kwenye daladala yaani akipanda Dada nakuwa makini sana nikiamini labda ndo huyu..!
MSAADA WENU TAFADHARI...
Aiseee kuwa makini sana mkuu katika hiyo sekta.
Unamuona mwenzio gwajima na skendo zake zote bado anatetewa na mkewe,si umemuona mkewe alivyokuwa na msimamo thaibiti Ndugu?
Alafu chonde chonde usiyafite mke wakati una genye zimekupanda,kila mke utamuona mzuri sana kwa sababu ya tamaa za mwili.
Mke ambae unaweza kudumu nae ni yule ambae ukimuona tu yanakujia mawqzo ya kumuoa zaidi ya kufanya nae mapenzi tu.maana yake ni kwamba kuna wanawake ukiwatazama tu mavazi yao basi wanakuvutia upate hamu ya kuzini nao.sasa mke akiwa hivyo tahadhari sana.
Nakumbuka wakati nipo kijana nasoma kabla sijaoa kulikuwa na dada falani anavaa hijabu vizuri sana ikawa namzimia sana kwa kweli mpaka nikimuona napata picha ameshakuwa mke wangu tayari na tunaishi vizuri sana,lakini kuna wadada wengine nikiwaona nawaza uchafu tu moja kwa moja.sasa wewe angalia sana sana sana.
Alafu angalia dini yako mkuu,kama ni mkristo basi pahala safi pa kupata mke ni kanisani.sasa kanisani NAKO UCHAGUE,SIO KWA KUWA NI KANISA BASI UNACHUKUA YEYOTE.utajuta na kuleta uzi hapa.kuwa makini kanisani uangalie na kuwashirikisha wazoefu wa sehemu hiyo.
Lakini pia naomba kama una mama basi mtumie kumuulizia akutafutie binti mwenye tabia njema sana anayemjua,wanamama wanajuana sana mtaani wanajua kabisa kwamba nyumba flani yule binti ametulia au hajatulia.kwa hiyo wanajua sehemu sahihi.
Alafu badala ya hapo sasa umwambie akutafutie mke,mama hawezi kukuimgiza chaka hata siku moja,ataeatumia wenzie wamtafutiee nyumba gni kuna binti mzuri.
Akipatikana unawaambie wasiambiwe hapo kwa binti kama una lengo fulani,wewe ufanye mipango kumuona huyo binti na kumtafakari nama alivyo,huku na wewe ukiulizia wadau mbali mbali juu ya mwenendo wake,ukiona umempenda namna alivyo na tabia ziko fressh basi hapo anza kutupa ndoana na kupeleka taarifa rasmi kwa huyo dada mdogo mdogo ili naye tuone kama atakuwa amekukubali.
Ila tu mkuu...
Ukitaka mke mwema basi kuwa wewe mwema kwanza.anza kutengenea mda huu tulie na kutuliza akili sio useme utatulia ukioowa shauri yako