Habari wakuu.
Poleni sana kwa majukumu, Hoja yangu ni kwamba imefika wakati nataka kuoa sasa, ila sasa imebidi niulize kwa mliooa. Mmepataje wake wakuoa? Maana toka nipate wazo la kuoa nimekua nazurula sana maeneo mbalimbali nikiamini nitakutana na anayenifaa, hii hali imenifanya hata nikiwa nyumba ya ibada nisiwe makini na ibada bali nakagua mke, hata nikiwa kwenye daladala yaani akipanda Dada nakuwa makini sana nikiamini labda ndo huyu..!
MSAADA WENU TAFADHARI...
Huo ni mchakato mgumu na mara nyingi ni kama kuna hali ya kubahatisha hasa pale mwanzo. Ila cha msingi hakikisha unakuwa na VIGEZO vyako mwenyewe binafsi vya mtu unayetaka awe mama wa watoto wako weka vigezo bila kushinikizwa na mtu yoyote. Mimi niliangalia vitu hivi-
Mosi, kwa kuwa kipindi hicho nilibahatika kufika kidato cha nne lengo langu la kwanza kabisa ni mtu walau aliyefika elimu hiyo, niliona mtu mwenye elimu chini ya hapo tungesumbuana. Na kweli nilikuwa sihangaiki kabisa na mtu wa chini ya elimu hiyo.
Pili, nikasema piga ua mke wangu hawezi kuwa wa makabila dulani. Ni hivi. Kwetu kutokana na uzoefu wa miaka mingi kuna makabila 'hayakubaliki' kirahisi kwa wazazi. Kwa wao kuna makabila yanahesabika kama ni watu wakorofi, wasio na ubinadam n.k. Hukatazwi moja kwa moja kuleta watu hawa ila kwa hakika ujiandae kupata mapokezi hasi. Kwetu mke hasa wa kwanza anahesabika kuwa sio tu wa kukutunza wewe peke yako bali anatunza familia yenu nzima.
Tatu, mke lazima awe wa kuvutia machoni KWAKO. Najua kwa wengine wanaweza kuipuuza hii pointi lakini ni muhimu sana. Usizoe tu mtu huko mtaani. Mke ni mtu maalum sana. Sio kila mwanamke anafaa kuwa mke. Kumbuka huyu ni mtu wa karibu sana utakula nae, utalala nae utashea naye karibia kila kitu lakini kubwa zaidi utaishi naye maisha yako yote hapa duniani. Na kwa baadhi ya imani mke huwa mmoja tu. So ni lazima auzike vizuri kwa vigezo vyote, usijekujuta baadae.
Nne, pata mke kutoka kwenye mazingira sahihi. Kuna hatari zake kuoa mwanamke tu maadam mmekutana tu huko mtaani. Mazingira mazuri ni maeneo ya ibada (makanisa, misikiti), makazini, mashuleni. Hawa mara nyingi wanakuwa kwenye mwelekeo fulani 'kutazama' maisha ya baadae. Kama ni lazima uchukue mtaani hakikisha unaifahamu vema familia yao!!
Hayo ni msingi kwangu, lakini kiujumla hakuna mtu mkamilifu kwa 100% mapungufu yanakuwepo la msingi ni kuvumiliana na kurekebishana.
==KILA LAKHERI KUSAKA MWALI==