Enyi mliooa, mlipataje wake?

Enyi mliooa, mlipataje wake?

Asante sana mkuu nitalifanyia kazi
Una pesa kweli wewe....? Tongoza acha uoga, kikubwa jichanganye na watu hasa kanisani, msikitini kazini, rafiki za marafiki zako wa kike au rafiki kabisa hawa ndiyo wake wazuri kabisa.
 
Habari wakuu.

Poleni sana kwa majukumu, Hoja yangu ni kwamba imefika wakati nataka kuoa sasa, ila sasa imebidi niulize kwa mliooa. Mmepataje wake wakuoa? Maana toka nipate wazo la kuoa nimekua nazurula sana maeneo mbalimbali nikiamini nitakutana na anayenifaa, hii hali imenifanya hata nikiwa nyumba ya ibada nisiwe makini na ibada bali nakagua mke, hata nikiwa kwenye daladala yaani akipanda Dada nakuwa makini sana nikiamini labda ndo huyu..!
MSAADA WENU TAFADHARI...
Una mpenzi?
Kama unaye fanya upgrade from girlfriend to wife !
 
Ukitaka mke mzuri mwangalie tabia za Mama wa Mke unae muoa,

Before ya mke wangu, nilikuwa na Binti mmoja tukienda kula tunaagiza Sato wawili na tulipo bakisha haangaiki kuomba afungiwe na mbaya zaidi alikuwa anaagiza vitu vyenye bei harafu vinamshinda.

Oohoo Mungu wangu... Nakumbuka first time nipo out na huyu ambae ni Mke wangu.. Alisema tuagize Sato mmoja na chip's Mbili... Na tulibakisha kwa sababu stori zilichukua nafasi kubwa.. Aliomba afungiwe kisha akaniambia chukua ukifika Home utakula... Nilimuona huyu vipi aoni noma hii sehemu tulivu hivi harafu mambo ya kufunga funga.. Ilikuwa saa nne usiku.

Nilivyo fika home nikavuta bangi kisha ndio nikazama kwenye tathimini juu yake... Ganja inaisha kichwani saa nane usiku njaa ya hatari.... Nikakumbuka ooohoo I have something. Mke mwema utamjua kwa Matendo na tabia zake.
 
Acha ujinga ndoa hufungwa na mungu binadamu ni mashahidi tu, so muombe mungu but mungu hadhihakiwi!
 
Nashukuru kwa huu uzi mana Leo tu nimetoka kupigiwa simu na mzee mwanjisi ananiuliza naoa lini mana umri umeenda anahitaji kushuhudia harusi yang. ...sasa kaka mkubwa hata mwanamke sina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom