Enyi marafiki wa mitandaoni, huwa hatuwakwepi wala haturingi, hizi ni sababu zinazopelekea kukataa kuonana na kuwa marafiki wa kujuana zaidi

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
1. Background za maisha tofauti - mtu unakuta ni tajiri ama anajiweza kiuchumi, ni maarufu, katokea familia ya wazito, nk. anakwepa machawa na wapambe wasio na urafiki naye bali unafki, mtu huyo anaona heri mjuane mitandaoni kuepuka kero hii, lakini pia kuna wivu na chuki ya maendeleo inaweza kuchipua mkijuana vizuri, ni heri tujuane mitandaoni tu.

2. Magonjwa - kuna wengine wana changamoto za kushindwa kuwa na marafiki wa kawaida, wapo vittandani muda mwingi, wana ulemavu, introverts wenye aibu, n.k. watu hawa wanapendelea zaidi urafiki wa mitandaoni.

3. Personality - mtanashati na mtu rough hawaivi pamoja, mwaminifu na kibaka hawaivi pamoja, n.k wanaogopa kukutana na marafiki kinyume chao, mnaweza kuwa marafiki mtandaoni kumbe personality tofauti, unakuta mcha Mungu na mshirikina wanapiga story fresh kabisa mtandaoni kuhusu michezo lakini wakiwa marafiki wa kujuana basi urafiki waweza kuvunjika.
 
Back
Top Bottom