Elon Musk : Vipofu sasa wataanza kuona

Elon Musk : Vipofu sasa wataanza kuona

Kule Malawi MWAMPOSA angekuwa Trilionea Kwa huu uvumbuzi
Huu udongo unaponya na upofu pia
sisi tuko mbele ya muda

1785884589191.png
 
Mwanzilishi wa Neuralink, Elon Musk, anasema kampuni hiyo ya kutengeneza vifaa vinavyopandikizwa kwenye ubongo inapanga kupandikiza vifaa vyake vya kwanza vya kuona vinavyojulikana kama Blindsight ndani ya miezi sita hadi 12 ijayo, huku ikiendeleza teknolojia inayolenga kuwarejeshea uwezo wa kuona watu wasioona.

Kifaa hicho cha majaribio kimeundwa kufanya kazi bila kutegemea macho yaliyoharibika na neva za macho kwa kutuma ishara (signals) moja kwa moja kwenye sehemu ya ubongo inayoshughulikia uwezo wa kuona. Musk alisema vipandikizi hivyo vya awamu ya kwanza vinatarajiwa kutoa uwezo wa kuona wa kiwango cha chini, huku watumiaji, hasa wale ambao wamekuwa vipofu tangu kuzaliwa, wakitarajiwa kuhitaji mazoezi makubwa ya ukarabati na kuzoea (rehabilitation).

Aliongeza kuwa matoleo ya baadaye ya teknolojia hiyo yanaweza hatimaye kutoa uwezo mkubwa zaidi ya ule wa asili wa binadamu wa kuona, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona miale ya infrared na ultraviolet.

Kifaa cha Blindsight cha Neuralink kimepata hadhi ya Kifaa cha Mapinduzi (Breakthrough Device) kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), ambayo inakiruhusu kunufaika na mchakato wa haraka wa maendeleo na ukaguzi wa kisheria. Hata hivyo, hadhi hiyo haimaanishi kwamba kifaa hicho kimeidhinishwa kwa matumizi ya kibiashara, na bado kinaendelea na hatua za majaribio ya kitiba (clinical development).
Mungu ametupa uwezo mkubwa sana binadamu imagine mtu mmoja tu huyo ametumia akili vizuri amekuja nabugunduzi wa ajabu kabisa yaani tunapoelekea huko mbelenii vipofu, viziwi sijui watu wenye mtindio wa ubongo watapata tiba na kukaa sawa kabisa kama binadama wa kawaida..
 
Wenzetu wanahangaika kutatua matatizo ya Watu .
Sisi tunahanhaika na...


1. Utekaji.
2. Kumbambikia watu kesi.
3. Uhaini.
4. Ugaidi.
5. Kuzima Mitandao.
6. Kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
7.Kulipa watu kumchafua Heche.
 
That's the power of AI inawaeza siku moja ku replicate life.. Na hapo ndo tutamalizana wenyewe kwa wenyewe
 
Mwanzilishi wa Neuralink, Elon Musk, anasema kampuni hiyo ya kutengeneza vifaa vinavyopandikizwa kwenye ubongo inapanga kupandikiza vifaa vyake vya kwanza vya kuona vinavyojulikana kama Blindsight ndani ya miezi sita hadi 12 ijayo, huku ikiendeleza teknolojia inayolenga kuwarejeshea uwezo wa kuona watu wasioona.

Kifaa hicho cha majaribio kimeundwa kufanya kazi bila kutegemea macho yaliyoharibika na neva za macho kwa kutuma ishara (signals) moja kwa moja kwenye sehemu ya ubongo inayoshughulikia uwezo wa kuona. Musk alisema vipandikizi hivyo vya awamu ya kwanza vinatarajiwa kutoa uwezo wa kuona wa kiwango cha chini, huku watumiaji, hasa wale ambao wamekuwa vipofu tangu kuzaliwa, wakitarajiwa kuhitaji mazoezi makubwa ya ukarabati na kuzoea (rehabilitation).

Aliongeza kuwa matoleo ya baadaye ya teknolojia hiyo yanaweza hatimaye kutoa uwezo mkubwa zaidi ya ule wa asili wa binadamu wa kuona, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona miale ya infrared na ultraviolet.

Kifaa cha Blindsight cha Neuralink kimepata hadhi ya Kifaa cha Mapinduzi (Breakthrough Device) kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), ambayo inakiruhusu kunufaika na mchakato wa haraka wa maendeleo na ukaguzi wa kisheria. Hata hivyo, hadhi hiyo haimaanishi kwamba kifaa hicho kimeidhinishwa kwa matumizi ya kibiashara, na bado kinaendelea na hatua za majaribio ya kitiba (clinical development).
Huyu vipi! Aje huku agombee urais aachane na hivyo vijimambo visivyolipa.
 
Back
Top Bottom