Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 20,330
- 49,071
Mwanzilishi wa Neuralink, Elon Musk, anasema kampuni hiyo ya kutengeneza vifaa vinavyopandikizwa kwenye ubongo inapanga kupandikiza vifaa vyake vya kwanza vya kuona vinavyojulikana kama Blindsight ndani ya miezi sita hadi 12 ijayo, huku ikiendeleza teknolojia inayolenga kuwarejeshea uwezo wa kuona watu wasioona.
Kifaa hicho cha majaribio kimeundwa kufanya kazi bila kutegemea macho yaliyoharibika na neva za macho kwa kutuma ishara (signals) moja kwa moja kwenye sehemu ya ubongo inayoshughulikia uwezo wa kuona. Musk alisema vipandikizi hivyo vya awamu ya kwanza vinatarajiwa kutoa uwezo wa kuona wa kiwango cha chini, huku watumiaji, hasa wale ambao wamekuwa vipofu tangu kuzaliwa, wakitarajiwa kuhitaji mazoezi makubwa ya ukarabati na kuzoea (rehabilitation).
Aliongeza kuwa matoleo ya baadaye ya teknolojia hiyo yanaweza hatimaye kutoa uwezo mkubwa zaidi ya ule wa asili wa binadamu wa kuona, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona miale ya infrared na ultraviolet.
Kifaa cha Blindsight cha Neuralink kimepata hadhi ya Kifaa cha Mapinduzi (Breakthrough Device) kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), ambayo inakiruhusu kunufaika na mchakato wa haraka wa maendeleo na ukaguzi wa kisheria. Hata hivyo, hadhi hiyo haimaanishi kwamba kifaa hicho kimeidhinishwa kwa matumizi ya kibiashara, na bado kinaendelea na hatua za majaribio ya kitiba (clinical development).