Jinsi ya kuweka akiba kwa wale tunaoanza maisha

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,941
7,937
Habari zenu wakuu, ni jioni sasa, akili yangu inaniambia wacha nishee nanyi Watanzania wenzangu kitu kimoja kuhusu kusave pesa ili kuweza kufikia uhuru wa kiuchumi na kutimiza ndoto zetu iwe kujenga, kununua gari au kuanzisha kampuni.

NB: This is not financial or life advice, za kuambiwa changanya na zako

#1 Kodi ya nyumba
Ukitaka kusave pesa hapa ndio pa kuanzia, angalia unakaa nyumba ya kodi kiasi gani. Sheria zote za uchumi zinasema kuwa hakikisha kodi ya nyumba yako haizidi 10% ya kipato chako cha mwezi, kwa maana kwamba, kama unalipwa laki tano basi hakikisha kodi ya chumba chako kwa mwezi haivuki Tsh. 50,000/-, Kwa sababu pesa hii haizalishi chochote kile, na uzuri kwa Tanzania yetu maeneo mengi tu vyumba utapata hadi vya 20k, kikubwa ishi kwenye kipato chako.

Ubaya wa kukaa nyumba ya gharama kubwa itakuacha na % chache za kutumia kwenye vitu vingine vya lazima, chumba unachoishi kikubwa kiwe livable tu, (nazungumzia bachelors).

#2 Nauli ya kwenda kazini kwako
Hapa sasa tazama vema, unafanya kazi point A ila unakaa point C inabidi uanze kupanda magari mawili kila siku kwa nauli ya zaidi ya Tsh. 2,500/- sawa na Tsh. 75,000/- kwa mwezi, na wengi wetu tunatumia nauli kubwa ili kukwepa kodi ya chumba ambayo utakuta ni Tsh. 20,000 au Tsh. 30,000.

Chukulia mfano, mtu anaefanya kazi Ubungo kisha akaamua kukaa Kiluvya ambako unapata Master nzuri ya Tsh. 70,000 ukakwepa kupanga maeneo ya Kimara ambako ungetembea kwenda kazini kwenye kodi ya Tsh. 100,000/ kwa chumba chenye hadhi hio hio.

Mtu huyu kwa mwezi anatumia nauli ya Tsh. 75,000 + Tsh. 70,000 ya kodi jumla ni Tsh. 145,000, wakati angepanga Kimara gharama ingekuwa Tsh. 100,000 kodi + 0 nauli jumla ni Tsh. 100,00 tofauti Tsh. 45,000 ambayo kwa mwaka ni Tsh. 540,000/- (hii pesa unanunua shamba heka 5 Njombe huko upande miti ya mbao). Panga karibu na kazini, utasave nauli.

#3 Chakula
Kula wakuu ni muhimu tule sana, ila kwenye kusave sasa kuna vitu nakushauri uvifanye ili uweze save pesa ya chakula;

~ Pika chakula chako mwenyewe kwa ladha na usafi wa hali ya juu.

~ Nunua chakula kwa bei ya jumla, mfano mchele kg 10, Unga kg 5 na kama unaweza.

~ Kama unaweza nunua fridge, litakusave sana kwenye mboga. Mjini hapa mboga majani ni jero ila ukinunua huwezi imaliza mara moja au 2, cha kufanya nunua fridge, nunua nyanya kwa bei ya jumla sokoni eg kisado, nunua karoti kwa bei ya jumla, hoho vile vile kisha ziweke kwa fridge, ukinunua nyama 1/2 kilo utaweza kula hadi mara 6 achana na matajiri wa JFwanaokula kg nzima mara moja), chemsha maharage yako hata kilo nzima (hapa utasave pia cost ya gas kama kwenye nyama pia) kisha yajaze kwa fridge utakula mwezi mzima, (usiyaunge, utayaunga unapotaka kula).

Hapo kwenye chakula tunategemea usave mpaka 80,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na 960,000 kwa mwaka, na ile 540,000 hapa tunakuwa tumesave Milioni 1.5 kwa mwaka.

#3 Mavazi
Hapa ndugu zangu, nunua nguo kali za kudumu, kwa wanaume, nunua shati zako za dukani japo 5 nunua suruali zako kali japo 5, kisha nunua kiatu cha ngozi kikali, utakuwa smart muda wote na pia itakuepusha na gharama za kununua nguo kila mwezi. Hapa utasave walau Tsh. 300,000/ kwa mwaka, na ile ya juu basi jumla utakuwa na Milioni 1.8.

#4 Kuendekeza wanawake
Hapa kukwepa vizinga simply unashauriwa ufanye yafuatayo;
~ Kuwa na mwanamke mmoja anaetoa mzigo bila kubania, usiwe na michepuko sabisa, pakuvuja pakiwa pengi itakuwa balaa.

~ Kuwa na mwanamke mpambanaji, usichukue beki tatu aisee, usibebe mwanamke wa kumlipia kodi aisee, mwanamke awe anajimudu, wew uwe unaweka chachandu na mahitaji madogo dogo. Bora kuwa single ila sio na beki tatu (Ukweli unauma najua).

~ Tenga bajeti ya mpenzi wako, eg ukisema kwa mwezi umpe mpenzi wako Tsh. 50,000 ya mahitaji, ikizidi hapo tangaza huna hela hadi mwezi ujao, kama ni muelewa wewe mwambie mapema kabisa, mimi kwa mwezi nakupa Tsh. 20,000 ya kusuka, Tsh. 10,000 ya vocha na Tsh. 20,000 ya extra then kila mwezi wewe mpe hiyo pesa halafu usisumbuane nae.

Mwambie kwa level yangu mama mi nakupa Tsh. 50,000 kila mwezi basi, ila kama uwezo wako wa Tsh. 10,000 mwambie kabisa (Hapa sheria ni isizidi 9.8% ya kipato chako, kama mnakumbuka Mungu tunampa 10% kwa hiyo hatuwezi mpa mwanamke kiwango kinachozidi hapo.

~ Usigongee mwanamke lodge (haitaki maelezo hii) mlete geto.

~ Mwana akija apike mwenyewe asinunue chakula, hataki afie mbele.

~Usiwe na mwanamke wa mbali mfano mkoa mwingine, hata kama upo naye mji mmoja hakikisha nauli kumleta geto haizidi Tsh. 2,000 kwa bodaboda na Tsh. 1,000 kwa daladala. Hili halina maelezo wote tunajua kauli ya sina nauli.

~ The best of all kama ukiweza kuwa single tu, kikubwa usiwe Punga au Chaputa

#5 Pombe
Simply acha pombe utasave at least Tsh. 200,000 kila mwezi na kwa mwaka Tsh. milioni 2.4, hivyo na ile Tsh. milioni 1.8 tunafika Tsh. Milioni 4.2 ambayo unaweza fanyia kitu kikubwa sana, hapo bado sijasemea kwa pesa utakayosave kwa mwanamke.

#6 Michango ya harusi na Misiba
Ndugu yangu michango ya sherehe ni muhimu kwa umoja wa taifa, lakin hakikisha unapunguza sana idadi ya michango. Epuka kwenda kwenye sherehe zisizo na umuhimu, mtu akikuletea kadi ukaona huyu humtaki, usipokee kadi, mpe kiasi fulani cha kuzugia kisha ondoka.

Mfano kama kadi ni Tsh. 50,000 wew mpe Ths. 20,000 kisha mwambie akatafute mbele (make sure unasave ya kutosha kwa ajiili ya harusi yako au usifunge kabisa maana watarudisha tena 😂). Same kwenye misiba, usiwe pedeshee ndama mtoto ya ng'ombe (hapa sheria ni michango ya kadi haitakiwi kuzidi 3% ya kipato chako cha mwezi)
Ukifanya hivo utasave kiasi cha kutosha, kuweza kufanya maendeleo.

Mpaka wakati mwingine tena, ulikuwa nami Beberu J,
Bye bye 👏
 
Naungana na ww kwa baadhi ya vitu vingine siafiki;

Msosi kupika labda jioni na chai ya asubuhi mchana unakula huko huko kazini!

Umesema usigongee demu lodge 🤔🤔aisee siwezi peleka demu geto hawa wa kwa chalamila wanatabia za kuzoea au kung'ang'ania, Kuja mara Kwa mara napenda kuyamaliza lodge

Pombe kama unapenda tumia ila kwa umakini

Harusi na misiba hapa inategemea, usipawekee sheria kiasi hicho ni sehemu ya kudeal nayo kimkakati
 
Naungana na ww kwa baadhi ya vitu vingine siafiki;

Msosi kupika labda jioni na chai ya asubuhi mchana unakula huko huko kazini!

Umesema usigongee demu lodge 🤔🤔aisee siwezi peleka demu geto hawa wa kwa chalamila wanatabia za kuzoea au kung'ang'ania, Kuja mara Kwa mara napenda kuyamaliza lodge

Pombe kama unapenda tumia ila kwa umakini

Harusi na misiba hapa inategemea, usipawekee sheria kiasi hicho ni sehemu ya kudeal nayo kimkakati

Shukran kwa kuja,
Suala la chakula cha mchana unaweza beba, au ukaamua kununua ila pale unapopata chance pika msosi
Suala la demu nimesema uwe na demu mmoja tu, ko inabidi uhakikishe unaye mwenye sifa zako, sasa mkuu lodge hizi za 15K ukigonga mara 6 kwa mwezi ni 90k kwa mwaka ni 1.06M, huoni kama ni loss kubwa sana, na ukienda lodge jua mtanunua msosi tena wa gharama tofaut na geto ambako angepika ?
Harusi na misiba, hapa deal kwa wale watu wa karibu, usitoe kwa kila mtu
 
Habari zenu wakuu, Ni jioni sasa, akili yangu inaniambia wacha nishee nanyi waTz wenzangu kitu kimoja kuhusu kusave pesa ili kuweza kufikia uhuru wa kiuchumi na kutimiza ndoto zetu iwe kujenga, kununua gari au kuanzisha kampuni,

Nb. This is not financial or life advice, Za kuambiwa changanya na zako

#1. Kodi ya nyumba, ukitaka kusave pesa hapa ndo pa kuanzia, check unakaa nyumba ya kodi kiasi gani? Sheria zote za uchumi zinasema kuwa hakikisha kodi ya nyumba yako haizidi 10% ya kipato chako cha mwezi, kwa maana kwamba kama unalipwa laki tano basi hakikisha kodi ya chumba chako kwa mwezi haivuki 50,000/-. Kwa sababu pesa hii ni isiyozalisha chochote kile, na uzuri kwa Tz yetu maeneo mengi tu vyumba utapata hadi vya 20k, kikubwa ishi kwenye kipato chako.
Ubaya wa kukaa nyumba ya gharama kubwa itakuacha na % chache za kutumia kwenye vitu vingine vya lazima, chumba unachoishi kikubwa kiwe livable tu, (nazungumzia bachelors)

#2. Nauli ya kwenda kazini kwako, hapa sasa tazama vema, unafanya kazi point A ila unakaa point C inabidi uanze kupanda magari mawili kila siku kwa nauli ya zaidi ya 2,500/- sawa na 75,000/- kwa mwezi, na wengi wetu tunatumia nauli kubwa ili kukwepa kodi ya chumba ambayo utakuta ni 20 au 30k,
Chukulia mfano, mtu anaefanya kazi ubungo kisha akaamua kukaa kiluvya ambako unapata Master nzuri ya 70k, ukakwepa kupanga maeneo ya Kimara ambako ungetembea kwenda kazini kwenye kodi ya 100K kwa chumba chenye hadhi hio hio, mtu huyu kwa mwezi anatumia nauli ya 75k + 70k ya kodi jumla ni 145k, wakat angepanga kimara gharama ingekuwa 100k kodi + 0 nauli jumla ni 100k tofauti 45k ambayo kwa mwaka ni 540,000/- (hii pesa unanunua shamba eka 5 Njombe huko upande miti ya mbao)

PANGA KARIBU NA KAZINI, UTASAVE NAULI

#3. Chakula, kula wakuu ni muhimu tule sana,
Ila kwenye kusave sasa kuna vitu nakushauri uvifanye ili uweze save pesa ya chakula

✓ pika chakula chako mwenyewe kwa ladha na usafi wa hali ya juu
✓ Nunua chakula kwa bei ya jumla, eg mchele kg 10, Unga kg 5 na kama unaweza
✓ Kama unaweza nunua fridge, litakusave sana kwenye mboga, mjini hapa mboga majani ni jero ila ukinunua huwezi imaliza mara moja au 2, cha kufanya nunua fridge, nunua nyanya kwa bei ya jumla sokoni eg kisado, nunua karoti kwa bei ya jumla, hoho vile vile kisha ziweke kwa fridge, ukinunua nyama 1/2 kilo utaweza kula hadi mara 6 (Achana na matajiri wa Jf wanaokula kg nzima mara moja), chemsha maharage yako hata kilo nzima ( hapa utasave pia cost ya gas kama kwenye nyama pia) kisha yajaze kwa fridge utakula mwezi mzima, (usiyaunge, utayaunga unapotaka kula)

Hapo kwenye chakula tunategemea usave mpaka 80k kwa mwezi ambayo ni sawa na 960k kwa mwaka, na ile 540 hapa tunakuwa tumesave 1.5M kwa mwaka

#3. Mavazi, hapa ndugu zangu, nunua nguo kali za kudumu, kwa wanaume, nunua shati zako za dukani japo 5 nunua suruali zako kali japo 5, kisha nunua kiatu cha ngozi kikali, utakuwa smart muda wote + itakuepusha na gharama za kununua nguo kila mwezi,
Hapa utasave at least 300k kwa mwaka, na ile ya juu basi jumla utakuwa na 1.8M

#4. Mademu, hapa kukwepa vizinga simply unashauriwa ufanye yafuatayo

✓ kuwa na demu mmoja anaetoa mzigo bila kubania, usiwe na michepuko Kabisa an, pakuvuja pakiwa pengi itakuwa balaa
✓ kuwa na demu mpambanaji, usichukue beki tatu aiseee, usibebe dem wa kumlipia kodi aisee, dem awe anajimudu, wew uwe unaweka chachandu na mahitaji madogo dogo, Bora kuwa single ila sio na beki tatu (Ukweli unauma najua)
✓ Tenga bajet ya demu wako, eg ukisema kwa mwez umpe dem wako 50k ya mahitaji, ikizidi hapo tangaza huna hela hadi mwezi ujao, kama ni muelewa wew mwambie mapema kabisa, mimi kwa mwezi nakupa 20K ya kusuka , 10 ya vocha na 20k ya extra then kila mwezi wew mpe hio pesa halafu usisumbuane nae abaki kuleta mzigo uunyandue tu, mwambie kwa level yangu mama mi nakupa 50k kila mwezi basi, ila kama uwezo wako wa 10k mwambie kabisa
(Hapa sheria ni isizidi 9.8% ya kipato chako, Kama mnakumbuka Mungu tunampa 10% ko hatuwez mpa mwanamke kiwango kinachozidi hapo)
✓ usigongee dem lodge (haitaki maelezo hii) mlete geto,
✓ Demu akija apike mwenyewe asinunue chakula, hataki afie mbele
✓ Usiwe na dem wa mbali eg mkoa mwingine, hata kama upo nae mji mmoja hakikisha nauli kumleta geto haizidi 2k kwa boda na 1k kwa daladala. Hili halina maelezo wote tunajua kauli ya sina nauli
✓ The best of all kama ukiweza kuwa single tu, kikubwa usiwe Punga au Chaputa

#5. Pombe, simply acha Pombe utasave at least 200k kila mwezi na kwa mwaka 2.4M hivo na ile 1.8M tunafika 4.2M ambayo unaweza fanyia kitu kikubwa sana, hapo bado sijasemea kwa pesa utayosave kwa mwanamke

#6. Michango ya harusi na Misiba, Ndugu yangu michango ya sherehe ni muhimu kwa umoja wa taifa, lakin hakikisha unapunguza sana idadi ya michango, epuka kwenda kwenye sherehe zisizo na muhimu, mtu akikuletea kadi ukaona huyu humtaki, usipokee kadi, Mpe kiasi fulan cha kuzugia kisha sepa eg kama kadi ni 50k wew mpe 20k kisha mwambie akatafute mbele ( make sure unasave ya kutosha kwa ajiili ya harusi yako au usifunge kabisa mana watarudisha tena 😂) Same kwenye misiba, usiwe pedeshee ndama mtoto ya ng'ombe)
(Hapa sheria ni michango ya kadi haitakiwi kuzidi 3% ya kipato chako cha mwezi)
Ukifanya hivo utasave kiasi cha kutosha, kuweza kufanya maendeleo.


Mpaka wakati mwingine tena, ulikuwa nami Beberu J,
Bye bye 👏
Ukitaka kusave hela kwa sie wanaume dawa ni moja tuu, jiunge chaputa basi
 
Mimi naongezea kuwa ni muhimu sana kutrack expenses zako. Huenda kuna mahala pesa ndogondogo zinaslip bila wewe kujua au kuwa makini. Mfano mm last week nimeona 7700 zimeenda kwenye matumizi ambayo ni ya ovyo, tho.. Week hii mpaka sasa kwenye matumizi ya ovyo n 500 tu. Nataka kueliminate kabisa haya matumiz ya ovyo...
 
Back
Top Bottom