Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,191
- 10,925
Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Baraka amemwambia waziri mkuu wa sasa,Bejamin Netanyahu kuwa kwa jina la Mungu aondoke madarakani.
Ehud Barak amesema kwa kuendelea kuwepo madarakani kwa Benjamin Netanyahu basi Israel itaendelea kuzama kwenye tope la Gaza. Akahimiza wakati wa kuondoka ni sasa.
Kama alivyosema mmoja ya wajumbe wa baraza la vita hapo juzi,Gadi kwamba kusidhinda Hamas si jambo rahisi.Ehud Baraka naye amesema Israel ina uchaguzi wa ama kuzama kwenye tope kwa kutaka kuishinda Hamas au kusitisha vita na kuokoa mateka.
Kutilia nguvu hoja zake akihojiana na Telegraph, Ehud amekumbusha kuwa muda wa siku 100 wa vita tayari umeshavuka muda wa kawaida katika historia kwa Israel kuendelea na vita.
Kauli hizi za washirika wa Netanyahu zimekuja huku wanafamilia wa mateka wakiendelea kuvamia nyumba ya Netanyahu na bunge la nchi hiyo kiasi cha kuvuruga vikao huku wakidai kuokolewa kwa ndugu zao.