Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Vita vya Israel na Palestina vinazidi kutoa matokeo hasi na ambayo hayakutarajiwa kabisa.
Mataifa rafiki na ya kiislamu yameanza kutofautiana na kuanza kupigana yenyewe mfano ni Iran na Pakistan na Iran kupiga ndani ya Syria na Iraq bila hofu ikiwinda vikundi vinavyofadhiliwa na Israel.
Hata Jordan nayo imejiamini na kupiga maeneo ya mpakani na Syria kuzuia vikundi vinavyotengeneza madawa ya kulevya ili kuilevya mashariki ya kati yote.
Matokeo hasi zaidi ni tofauti kati ya raisi Biden na waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu ambao kwa asili viongozi wote wa mataifa hayo huwa ni marafiki na wenye malengo mamoja.
Hata hivyo ubabe na kibri cha waziri mkuu wa Israel kimeendelea kumuudhi raisi Biden kwa vile anakataa mapendekezo yote ya Marekani kuhusu vita hivyo na kile kinachoitwa baada ya vita.
Raisi Biden akizingatia idadi kubwa ya wananchi wake wanaoiunga mkono Hamas na Palestina kwa jumla na pia akizingatia wapiga kura wanaoweza kumpigia kura yeye,amemtaka Netanyahu asiendelee kuua watu wa Gaza kiholea na kwamba ni lazima liundwe taifa la Palestina.
Kwa jeuri ya hali ya juu Netanyahu amekuwa akitoa matamko kupingana na malelekezo na mtazamo wa Biden.Mara kadhaa amekuwa akijibu mapendekezo hayo kwa kusema hakuna wa kuizuia Israel kuimaliza Hamas na kwamba hakuna mipango ya kuundwa kwa taifa la Palestina.
Kauli hizo zimemkasirisha sana raisi Biden na kujitenga kwa kiasi kikubwa na waziri mkuu huyo wa Israel ambaye amemsabibishia upinzani hadi ndani ya chama chake kuhusiana na Gaza.