sakapal ulichozungumza kina ukweli kwa upande mmoja. Mimi nadhani kuna sababu za msingi zinazoweza kuwafanya watu wajuane kwa uhalisia wao. Kuna wengine wanapenda kukutana kwa sababu ya biashara , elimu au uchumba na mambo mengine mengi ya msingi. Sasa ukiangalia huu upande mwingine wa shilingi unaona upo umuhimu kwa wanaotaka kufahamiana kwa kina kufanya hivyo. Kuna mtu kuwa na uhitaji wa mambo ya kisheria na mengine mengi tu. Nakumbuka kuna binti 1 aliwahi kuleta story yake ya kusikitisha hapa na akapewa msaada wa kukutana na member flani humu jf ili apate huo msaada nakumbuka ulikua ukihusiana na mambo ya ajira kama sikosei. Ni vizuri kupeana tahadhari lkn pia tusiwe rigid sana ingefaa tuwe positive wakati wote tena nakupa pongezi kwa uthubutu wako wa kukutana na hao uliokutana nao macho kwa macho naamini mambo yangekua mazuri pia ungetushirikisha nasema tena asante kwa taarifa. Mitandao yote ina side zote mbili kuna faida na hasara kama vilivyo vitu vingine na kwa sabababu inahusu binadamu basi haina tofauti sana na maisha yetu halisi. kwani mtaani kuna wambea, waongo ,wema , wastaarabu, wezi n.k