Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 14,696
- 32,273
👉kule wapi
👉kule wapi
Umenichekesha sana.muda wakiendelea kusahihisha madaftari na wengine wakiendelea kuzungumzia lile tukio
😂😂😂😂😂😂Umenichekesha sana.
Siku nazama darasa la kwanza nariport
mpuuzi mmoja kanikanyaga.
Nikapiga mpk kazimia.
Nikapelekwa ofisini walimu wako hapo wanasaini madaftari,
pigwa sana fimbo rudi home maza nae yumo anafundisha hapo.
Rudi baada ya wiki 2 fresh.
Yule dogo Rafael akaleta ujinga tena darasa la nne alichokipata anakijua.
E bana dingi yake mwendesha malori amemuona karudi anavuja damu kaja shule siku ya pili nikapewa kichapo safi tu.
Mi narudi home nimevimba
Dingi imekuwaje?
Namwambia babake Rafael kanipiga.
Unasema babaake kakupiga?
Dingi hata hakuuliza sababu.
Unapajua kwao ?
Ndio
Twende.
E Bana zilipigwa ngumi pale huku nna fimbo nachapa alafu nampa mori dingi badae baba Rafael nae kazima.
Mi na dingi tukatoka baru kurudi home.
Maza hata hajui tulichofanya huko.
Tumerudi piga kimya.
Hii story imenikumbusha mbali sana😅😅😅
😂😂😂😂😂😂
Gamasara Buhemba Tarime umenikunbusha kipindi hichoo Tarime SecLeo nilikua naelekea Tarime, basi tipo fika Korio nikaku kumbuka, hadi tunapita Mika.
Tulipo fika Gamasara ndio nikawa kama nakuona kabisa msani kama unatembea kwa miguu kutokea Buhemba, mgongoni ukiwa umebeba mfuko wako ile tulikuaga tunaita bob...[emoji23]
Nimecheka sana 😂😂😂Sehemu ya 3
Mwanajeshi " Nani aliyewapa ruhusa ya kuogelea lamboni?"
Aliendelea "Hakuna majibu?"
Mwanajeshi "Kila siku mnakatazwa kuogelea pale lakini kwasababu nyie ni wanaume mmegoma kabisa kusikia,si ndiyo?,sasa nadhani nyie ndiyo mtawapa wenzenu taarifa!"
Aliendelea " Haya kila mtu ainamie kichwa huku miguu ikiwa ukutani,fanya haraka wewe changamka!"
Kilikuwa ni kitendo cha haraka kila mmoja akakamata nafasi na kufanya kama tulivyoambiwa,aisee asikwambie mtu lilikuwa ni zoezi la hatari na liliomiza mbavu hatari,nakumbuka kuna madogo walianza kulia na kutetemeka kwa maumivu lakini wale wajeda walikuwa hawajali hata kidogo.Kiukweli tulijiona wajinga kupitiliza kwasababu kilichokuwa kimetupeleka ni kumdaka yule dogo wa Kuruchumila ila sisi tukajipeleka wenyewe kwenye mdomo wa mamba,na siyo kwamba hatukujua huwa hairuhusiwi kuogelea kwenye lile lambo ila ni kwamba tulivyokuta madogo wanaogelea tukadhani siku hiyo ilitolewa ofa maalumu [emoji1787][emoji1787]
Baada ya kama masaa 2 kuhenyeka kwenye ile adhabu,wale wajeda walituambie tuvue zile kofia na wakaleta madude fulani huwa yanatumika kwenye ujenzi wakati wa kufunga lenta na uezekaji,tulikuwa tunayaita "MAKOA",Sikuhizi haya madude yamepotea sana hayaonekani sijajua ni kwasababu gani,miaka ya nyuma hata marobota ya nguo za mitumba yalikuwa yanabanwa na haya madude.
Wajeda wakasema kila mmoja ajikamatie KOA lake mkononi,sasa kazi ikaanza rasmi,Daaah nikikumbuka huwa nacheka kama mwehu![emoji23][emoji23]
Mjeda mmoja akatuambie tukae kila mtu na mwenzake,yaani ulikuwa unaulizwa "Wewe umekuja na nani?" ,Ukisema umekuja na fulani basi huyo ndiye mnapaswa kukaa nae huku mkiangaliana usoni.Mimi nikasema nilikuwa na mshikaji wangu Mabobo,hivyo tukatakiwa kusimama na kuangaliana,ile tumeangaliana na Mabobo nikajikuta naanza kucheka[emoji23][emoji23]
Kuna mjeda akatoa maelezo ya kwamba tuchaguane kwa wale tuliosimama na kutizamana nani awe wa kwanza,Mabobo yeye akasema ndiye atakayekuwa wa kwanza,baada ya hapo ikatolewa Amri ya kwamba wa kwanza ndiyo atakaye anza kuuliza mkononi nimebeba nini na nikitamka "KOA" inabidi nipigwe kwenzi lililoenda shule,akimaliza na mimi pia nafanya kama alivyo fanya,daaaah!
Mabobo akawa wakwanza kuniuliza nimebeba nini mkononi na mimi nikasema "KOA",Jamaa akanishushia bonge la kwenzi,baada ya lile kwenzi nikaona mambo yameshaharibika hapa na hakuna mzaha.Ikafika zamu yangu na mimi nikamuuliza Mabobo amebeba nini mkononi jamaa akasema "KOA",nikamshushia bonge la kwenzi.Tulieneelea na ile adhabu hadi kila mtu atakapolia,endapo mwenzio akiwa nunda mtaendelea hadi alie ndipo msamaha upite,tulipofahamu ya kwamba kilio ndicho kilicholeta msamaha basi hazikupita dakika nyingi kila mmoja alianza kulia,kiukweli baada ya vile vilio wale wajeda walitusamehe na kutuonya ya kwamba tusije kurudi tena kule lamboni na tukawe mabalozi kwa vijana wenzetu [emoji23]
Baada ya kutawanyishwa kila mtu alishika njia yake,sasa kazi ikaanza kumsaka yule dogo na yeye alituona akaanza kukimbia kwa nguvu zote,Mabobo akaanza kumfukuzia kimya kimya,alipoona maji yanaelekea kuzidi unga yule dogo akaanza kulia huku akipiga kelele kana kwamba tunaomfukuza ni vibaka wazoefu tunataka kumpora!,kwa mbele kidogo akasimamishwa na dingi mmoja akawa anamuuliza unalilia nini?
Dogo "Hawa wananifukuza wanataka kunipiga"
Tulipofika lile eneo nikashangaa Mabobo anapitiliza kana kwamba hakuna kinachoendelea (Jamaa alikuwa mbele ya muda).Baada ya kuona vile na mimi nikapita zangu kama hatuna muda vile,yule mzee nadhani alishangaa dogo kutushitaki na akiona washitakiwa ni kana kwamba hawana muda,tulitembea tukafika mbele Mabobo akaniambia tumsubiri yule dogo kwakuwa atakuja na ile njia,bila kufahamu kumbe dogo naye kapitia njia nyingine kutukwepa[emoji23]
Aisee ile ishu ya kumsaka yule dogo iliendelea vile baada ya siku kadhaa ikabidi tuachane nayo tu.
Sasa kuna siku tukiwa darasani kumbe jamaa alikuwa akila KUBER,mimi muda sijui kama jamaa ana KUBER amebeba kwenye mfuko wa Sportsman,jamaa baada ya kula ile kitu ikaanza kumpeleka matawi ya juu,kumbe katoka darasani kaelekea ofisini kumtongoza ticha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dadeeeek walahi!.Aisee ile nimekaa zangu class sina hili wala lile nikashangaa naitwa na mwanafunzi mmoja natakiwa kufika ofisi ya walimu,aisee enzi hizo kuitwa ofisi ya walimu ni lazima ujishitukie umefanya kitu gani hata kama ulikuwa unaitwa kwa mema,kabla ya kwenda nikahakikisha nimechomekea shati na kupandisha soksi ili nisije kupatikana na dosari nikashushiwa mbata za hatari.
Sina hili wala lile kufika Ofisini nakuta Mabobo akiwa amelala chini ya sakafu huku maticha wengine wakiwa hawana muda wakiendelea kusahihisha madaftari na wengine wakiendelea kuzungumzia lile tukio.Nilipofika tu jambo la kwanza nilipewa hela na mwalimu mmoja nikaambiwa nikanunue maziwa ya pakti!.
Nikaenda nakimbia huku huku sielewi ni kitu gani kilimkuta mshikaji,niliporudi yale maziwa yalifunguliwa na ticha mmoja wa kiume akaanza kumnywesha jamaa,alikunywa yote akamaliza na ndipo akaanza kutapika mle ofisini,sasa kumbe jamaa ile KUBER alikuwa akiila na kuimeza kama chakula,Aiseeee![emoji23].Muda huo nimewekwa mtu kati na nimeambiwa nikae chini ili nije nieleze vizuri kwasababu jamaa alikuwa rafiki yangu sana na nadhani maticha waliona mtu wa kwanza kujibu ni UMUGHAKA.
Basi bana,baada ya jamaa kutapika sana ikabidi niambiwe niende kuchukua ndoo na tambala la deki nije nisafishe mle ofisini,baada ya hali kuwa shwari ikagongwa kengele [emoji23][emoji23][emoji23]
Itaendelea......
Leo nilikua naelekea Tarime, basi tipo fika Korio nikaku kumbuka, hadi tunapita Mika.
Tulipo fika Gamasara ndio nikawa kama nakuona kabisa msani kama unatembea kwa miguu kutokea Buhemba, mgongoni ukiwa umebeba mfuko wako ile tulikuaga tunaita bob...😂
Kweli mkuuMaisha haya hututawanyw'a sana!
Big up sana kwako UMUGHAKA. Umekumbuka mbali sana.Sehemu ya 4
Aisee Kengele Ikagongwa kwa nguvu zote na wanafunzi kila mmoja akawahi asembo,basi bana baada ya mwalimu wa zamu kuwatangazia wanafunzi ya kwamba kuna dharura ikabidi Jopo lote la walimu likiongozwa na Mwalimu Mkuu wakatoka ofisini,mimi pamoja na Mabobo pia tukiwa sehemu ya Jopo hilo.
Mwalimu wa Nidhamu "Mnawaona hawa?"
Wanafunzi "Ndiyo"
Mwalimu " Mnawafahamu"
Wanafunzi "Ndiyo"
Mwalimu "Wanasoma darasa la ngapi?"
Baadhi ya wanafunzi darasani kwetu "Darasa la Tanooooo!"
Mwalimu "Monita wa Darasa la hawa wajinga ni nani?"
Kipindi hicho sisi Monita na Monitress tulikuwa hatujui kuwatofautisha na hatukuwaga na Monitor bali Monitress,sasa sisi hata Monitress tulimuita Monita hivyo hivyo!.Yule demu wa kuitwa Pendo akaitwa atoke mbele.
Mwalimu "Na wewe monitor utatueleza ukweli,sogea pale"
Baada ya kuongea mambo kadhaa ya kuonyesha kuna tukio baya limefanyika akakribishwa Mwalimu mkuu azungumze,Yule mwalimu hakuwaga mzungumzaji yeye alimwambia mwalimu wa zamu atukabidhi barua zetu kisha tuwapelekee wazazi.
Baada ya hapo wanafunzi wakaambiwa ya kwamba Mabobo amekutwa anakula madawa ya kulevya aina ya KUBER huku mimi nikituhumiwa kufahamu kila kitu ila nikawa msiri wa jamaa na kosa lingine kubwa kabisa ni Mabobo kumtongoza Ticha[emoji23][emoji23].Zile Barua tuliambiwa tuwafikishie wazazi,kiukweli baada ya hapo wanafunzi walitawanyika kurejea madarasani lakini mimi na ndugu yangu Mabobo tukaambiwa tupotee kuelekea nyumbani.
Kuna mahali tulifika Mabobo akaniambia tufungue zile Barua tusome kilichokuwa kimeandikwa,sasa tukakuta ni wito wa kuitwa kwa wazazi wetu haraka sana ya siku iliyokuwa ikifuatia bila kukosa,yaani kwakifupi ile asubuhi wakati tunaenda skonga tuhakikishe tunaandamana na wazazi wetu.Baada ya kusoma zile barua Mabobo yeye akasema ataenda kumshitua jamaa mmoja alikuwa rafiki yake alikuwa akiosha magari na alikuwa akiitwa Wanyancha!,huyo jamaa alikuwa amepanda hewani na alikuwa na body ingawa alikuwa hanyananyui vyuma.
Mimi niliona ile Barua ingemfikia mzee wangu ni hakika ningepigwa mpaka nichakae au kufa kabisa,kuna mwanamke mmoja alikuwaga rafiki yake na Bi Mkubwa walikuwa wote wanafanya kazi huko sokoni,nikaenda nikamualeza hali halisi na alisikitika sana akasema hilo suala hapaswi baba kulifahamu na hata mama angemwambia baada ya kulimaliza,basi bana akaniahidi asubuhi wakati anawahi sokoni tungendamana nae mpaka shule kwanza halafu ndiyo aelekee sokoni.
Kweli,Kesho yake Asubuhi kama kawa tukaelekea shule tukiwa tumeandamana na wazazi wetu hewa,tulipofika ile asubuhi wakati wa parade yakaanza kusomwa makosa yetu upya,baada ya hapo vikaletwa viboko tukaambiwa kila mzazi amchape mwanae viboko 5.Aisee yule wananyancha alikuwa akimshushia stiki Mabobo kana kwamba wanaugomvi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aisee nilikuwa kwenye hali ya kucheka lakini nilijikaza mnoo!.
Yule Bi mkubwa alinichapa lakini si ki vile kama ambavyo Wanyancha alimshushia kipondo Mabobo,halafu baadae ile jioni Tumetoka shule Wanyancha anamwambia mshikaji ya kwamba alifanya vile ili ionekane kweli ni mzazi ionekane alichukia kile kitendo[emoji23][emoji23][emoji23].
Aisee maisha baada ya hapo yaliendelea kama kawaida na tukamaliza shule kwa vituko na vihoja,ingawaje Mabobo alinifunza utukutu lakini kichwani zilikuwemo na nilifaulu fresh kuelekea Tarime Secondary na hapo ndipo ukawa mwisho wa kusoma shule moja na mshikaji wangu ingawa tulikuwa tukionana lakini kadiri siku zilivyokuwa zikisonga ndivyo maisha ya elimu yakawa yanatutenga.
Jamaa yangu popote ulipo elewa ya kwamba nakumiss sana mwanangu na mimi ni Umughaka mshikaji wako wa Kitambo.
Mungu atusamehe sana kwa yote tuliyoyafanya ikiwemo kuiba Mbuzi wa Mzee Kibasa na kwenda kumchinja na kula nyama tukiwa na kina Wamweru,Mathias,Samson na Ndago[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ni hayo tu wakuu kwa leo niishie hapa