Eeeh Mungu nisamehe mimi na Mshikaji wangu Mabobo

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!

Aiseee leo nimekumbuka vituko vya miaka ya nyuma wakati nasoma shule ya msingi pale Rebu!.

Ni miaka mingi nimepotezana na rafiki yangu kipenzi wa miaka hiyo aliitwa Emmanuel Matiko Masanda a.k.a Mabobo, Daaaah , Popote ulipo jamaa yangu kama uko hai basi naamini ipo siku tu tutaonana. Nimejaribu mwaka fulani kwenda mahali mlipo kuwa mkiishi wewe na familia yako nikakuta lile eneo siku hizi limekuwa gereji ya kupaki magari ya ZAKARIA(Peter Zakaria) it means mlihama, mliuza au mlihamishwa, kiukweli sielewi!.

But kuna jamaa mmoja aliwahi niambia Mabobo yupo hapo kwa Madiba na amekuwa jamaa mwenye uwezo wake huko! Mungu akusimamie kama ni kweli kaka naamini kama upo hai tutaonana!.

Sasa leo nimeona nikumbikie yale tuliyoyafanya enzi hizo.

Jamaa yangu huyu(Mabobo) siku moja akaniambia

Mabobo "Mwanangu kuna hela nailia taimingi, nikiipata hiyo nataka twende kwa yule mzungu nikatoe mahari kwa kale katoto kake kazuri nikaoe"

Daaaah haya maisha huwa nakumbukia nabaki kucheka sana, hapo Jamaa ananiambia hivyo hata bado hajabalehe(Mtoto wa kiume niwa kiume tu, dadeeeeki).

Kuna mzungu mmoja miaka hiyo tulikuwa tuna muita "Mnorway" alikuwa ametokea huko Norway yeye na familia yake walikuwa wakiishi hapo mtaani na sikujua alikuwa akifanya ishu gani, miaka hiyo tulikuwa tunafurahi kuwaona tu wazungu, sasa Mabobo alikuwaga mtundu sana bana, alikuwa na mazoea na binti wa yule mzungu.

Mabobo nakumbuka mpaka alijifunza kuendesha vile viatu vya matairi(Roller skates) na aliyekuwa akimfundisha ni yule binti wa kizungu hivyo kuzoeana kiasi kwamba tusipokuwa tunaonekana pale kwao yule binti ni kama alikuwa mgonjwa.

Pale kwao kulikuwa na Mbwa mkali lakini kutokana na yale mazoea ya kuwa pale yule mbwa akatuzoea kama wenyeji wake.

Sikufahamu siku zote kumbe mshikaji wangu Mabobo alikuwa anawinda box la kuhifadhia pesa(KIBUBU) cha jamaa mmoja aliyekuwa akifanya kazi benki pale Tarime mjini (National Microfinance Bank), yule jamaa alikuwa ni jirani na kina Mabobo hivyo alikuwa akimla dada yake Mabobo. Sasa mabobo kuingia kwa jamaa ilikuwa ni kama kawa, hivyo kumbe kila wakati anapopata fursa za kuingia kwa jamaa kwa mgongo wa dada yake alikuwa akichunguza wapi jamaa anaweka pesa!.

Siku moja Mabobo alinisanua kwamba kuna safe ameipata mahali ikiwa na vumba kama loote! Nikamuuliza kaitoa wapi ile safe jamaa akaniambia ameikota mtaroni kumbe aliipiga kwa shemeji yake

Safe yenyewe ilikuwa ya chuma na tulifanya kazi sana mpaka kuivunja,na tulipoivunja tulikuta kulikuwa na elfu 16000/=, aisee kwa miaka ile sisi tulikuwa wafalme wa mji na shule!.

Kwa kuwa hatukutaka kufahamika kwamba tuliiba ile hela tulienda kuificha kwenye shamba la mugomba la mzee mmoja wa kuitwa kuruchumila,ile hela jamaa aliniambia tuiweke kwenye mgomba mmoja ambao kila siku tungekuwa tunachukua ndogo ndogo na kufanyia taizi shuleni huku chopstick na vibaragala vingetukoma!.

Eeeh bana kiukweli tulikula maisha sana, nakumbuka ile ikifika saa 4 muda wa mapunziko sisi ndo tulionekana madoni wa shule, mademu na wapambe nuksi kama wote yaaani!.

Kwa yale maisha ya skonga jamaa akasahau kupelekea mahari kwa Mnorway kama alivyokuwa akisema mwanzo,daaaah!.

Sasa kumbe kipindi kile tunapoenda kwenye lile shamba kuchukua mpunga kuna mtu alikuwa akitulia chabo, daaaaah

Itaendelea kama kutakuwa na umuhimu!
 
Tarime ulikua unakaa mitaa gan.....?
Me nlikua pale Cafetelia kwa nyuma.
Bibi yangu alikua anakaa kwa Mzee makaranga kule chini
Mkuu mbona nimesema mitaa ya Rebu ndiyo kwetu.

Mkuu kwani Kwa Makaranga ilikuwa nyuma ya Cafteria? Cafeteria iliyokuwa inaonyesha muvi za Arnod shwazneger na Vandamme au Cafteria ipi?

Kwa Makaranga si kulikuwa kule chini kama unaelekea CMG motel!
 
Mkuu mbona nimesema mitaa ya Rebu ndiyo kwetu.

Mkuu kwani Kwa Mkaranga ilikuwa nyuma ya Cafteria?,Cafeteria oliyokuwa inaonyesha muvi za Arnod na Vandame au Cafteria ipi?

Kwa Makaranga si kulikuwa kule chini kama unaelekea CMG motel!
Mkaranga n njia ya kwenye CMG. Kule ndio alikua anakaa Bibi na Babu.
Nyuma ya Cafetelia karibu na Mwalimu Gimugu ndio kulikua Home
 
Back
Top Bottom