Eeeh Mungu nisamehe mimi na Mshikaji wangu Mabobo

Eeeh Mungu nisamehe mimi na Mshikaji wangu Mabobo

Sehemu ya 3


Mwanajeshi " Nani aliyewapa ruhusa ya kuogelea lamboni?"

Aliendelea "Hakuna majibu?"

Mwanajeshi "Kila siku mnakatazwa kuogelea pale lakini kwasababu nyie ni wanaume mmegoma kabisa kusikia,si ndiyo?,sasa nadhani nyie ndiyo mtawapa wenzenu taarifa!"

Aliendelea " Haya kila mtu ainamie kichwa huku miguu ikiwa ukutani,fanya haraka wewe changamka!"


Kilikuwa ni kitendo cha haraka kila mmoja akakamata nafasi na kufanya kama tulivyoambiwa,aisee asikwambie mtu lilikuwa ni zoezi la hatari na liliomiza mbavu hatari,nakumbuka kuna madogo walianza kulia na kutetemeka kwa maumivu lakini wale wajeda walikuwa hawajali hata kidogo.Kiukweli tulijiona wajinga kupitiliza kwasababu kilichokuwa kimetupeleka ni kumdaka yule dogo wa Kuruchumila ila sisi tukajipeleka wenyewe kwenye mdomo wa mamba,na siyo kwamba hatukujua huwa hairuhusiwi kuogelea kwenye lile lambo ila ni kwamba tulivyokuta madogo wanaogelea tukadhani siku hiyo ilitolewa ofa maalumu [emoji1787][emoji1787]

Baada ya kama masaa 2 kuhenyeka kwenye ile adhabu,wale wajeda walituambie tuvue zile kofia na wakaleta madude fulani huwa yanatumika kwenye ujenzi wakati wa kufunga lenta na uezekaji,tulikuwa tunayaita "MAKOA",Sikuhizi haya madude yamepotea sana hayaonekani sijajua ni kwasababu gani,miaka ya nyuma hata marobota ya nguo za mitumba yalikuwa yanabanwa na haya madude.

Wajeda wakasema kila mmoja ajikamatie KOA lake mkononi,sasa kazi ikaanza rasmi,Daaah nikikumbuka huwa nacheka kama mwehu![emoji23][emoji23]

Mjeda mmoja akatuambie tukae kila mtu na mwenzake,yaani ulikuwa unaulizwa "Wewe umekuja na nani?" ,Ukisema umekuja na fulani basi huyo ndiye mnapaswa kukaa nae huku mkiangaliana usoni.Mimi nikasema nilikuwa na mshikaji wangu Mabobo,hivyo tukatakiwa kusimama na kuangaliana,ile tumeangaliana na Mabobo nikajikuta naanza kucheka[emoji23][emoji23]

Kuna mjeda akatoa maelezo ya kwamba tuchaguane kwa wale tuliosimama na kutizamana nani awe wa kwanza,Mabobo yeye akasema ndiye atakayekuwa wa kwanza,baada ya hapo ikatolewa Amri ya kwamba wa kwanza ndiyo atakaye anza kuuliza mkononi nimebeba nini na nikitamka "KOA" inabidi nipigwe kwenzi lililoenda shule,akimaliza na mimi pia nafanya kama alivyo fanya,daaaah!

Mabobo akawa wakwanza kuniuliza nimebeba nini mkononi na mimi nikasema "KOA",Jamaa akanishushia bonge la kwenzi,baada ya lile kwenzi nikaona mambo yameshaharibika hapa na hakuna mzaha.Ikafika zamu yangu na mimi nikamuuliza Mabobo amebeba nini mkononi jamaa akasema "KOA",nikamshushia bonge la kwenzi.Tulieneelea na ile adhabu hadi kila mtu atakapolia,endapo mwenzio akiwa nunda mtaendelea hadi alie ndipo msamaha upite,tulipofahamu ya kwamba kilio ndicho kilicholeta msamaha basi hazikupita dakika nyingi kila mmoja alianza kulia,kiukweli baada ya vile vilio wale wajeda walitusamehe na kutuonya ya kwamba tusije kurudi tena kule lamboni na tukawe mabalozi kwa vijana wenzetu [emoji23]

Baada ya kutawanyishwa kila mtu alishika njia yake,sasa kazi ikaanza kumsaka yule dogo na yeye alituona akaanza kukimbia kwa nguvu zote,Mabobo akaanza kumfukuzia kimya kimya,alipoona maji yanaelekea kuzidi unga yule dogo akaanza kulia huku akipiga kelele kana kwamba tunaomfukuza ni vibaka wazoefu tunataka kumpora!,kwa mbele kidogo akasimamishwa na dingi mmoja akawa anamuuliza unalilia nini?

Dogo "Hawa wananifukuza wanataka kunipiga"

Tulipofika lile eneo nikashangaa Mabobo anapitiliza kana kwamba hakuna kinachoendelea (Jamaa alikuwa mbele ya muda).Baada ya kuona vile na mimi nikapita zangu kama hatuna muda vile,yule mzee nadhani alishangaa dogo kutushitaki na akiona washitakiwa ni kana kwamba hawana muda,tulitembea tukafika mbele Mabobo akaniambia tumsubiri yule dogo kwakuwa atakuja na ile njia,bila kufahamu kumbe dogo naye kapitia njia nyingine kutukwepa[emoji23]

Aisee ile ishu ya kumsaka yule dogo iliendelea vile baada ya siku kadhaa ikabidi tuachane nayo tu.


Sasa kuna siku tukiwa darasani kumbe jamaa alikuwa akila KUBER,mimi muda sijui kama jamaa ana KUBER amebeba kwenye mfuko wa Sportsman,jamaa baada ya kula ile kitu ikaanza kumpeleka matawi ya juu,kumbe katoka darasani kaelekea ofisini kumtongoza ticha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dadeeeek walahi!.Aisee ile nimekaa zangu class sina hili wala lile nikashangaa naitwa na mwanafunzi mmoja natakiwa kufika ofisi ya walimu,aisee enzi hizo kuitwa ofisi ya walimu ni lazima ujishitukie umefanya kitu gani hata kama ulikuwa unaitwa kwa mema,kabla ya kwenda nikahakikisha nimechomekea shati na kupandisha soksi ili nisije kupatikana na dosari nikashushiwa mbata za hatari.

Sina hili wala lile kufika Ofisini nakuta Mabobo akiwa amelala chini ya sakafu huku maticha wengine wakiwa hawana muda wakiendelea kusahihisha madaftari na wengine wakiendelea kuzungumzia lile tukio.Nilipofika tu jambo la kwanza nilipewa hela na mwalimu mmoja nikaambiwa nikanunue maziwa ya pakti!.

Nikaenda nakimbia huku huku sielewi ni kitu gani kilimkuta mshikaji,niliporudi yale maziwa yalifunguliwa na ticha mmoja wa kiume akaanza kumnywesha jamaa,alikunywa yote akamaliza na ndipo akaanza kutapika mle ofisini,sasa kumbe jamaa ile KUBER alikuwa akiila na kuimeza kama chakula,Aiseeee![emoji23].Muda huo nimewekwa mtu kati na nimeambiwa nikae chini ili nije nieleze vizuri kwasababu jamaa alikuwa rafiki yangu sana na nadhani maticha waliona mtu wa kwanza kujibu ni UMUGHAKA.

Basi bana,baada ya jamaa kutapika sana ikabidi niambiwe niende kuchukua ndoo na tambala la deki nije nisafishe mle ofisini,baada ya hali kuwa shwari ikagongwa kengele [emoji23][emoji23][emoji23]


Itaendelea......
 
Mkuu hii mitaa kwa mtoto yoyote wa Tarime ilikuwa lazima kuikatiza,Hapo Turwa na Nyamisangura naweza sema kwa miaka hiyo ndiyo ilikuwa kama senta ya shule zote hapo Tarime.

Mademu wakali ungewakuta kama si Turwa basi Nyamisangura.

Kuna miaka fulani kipindu pindu kilipiga haswaaa,sasa shule yetu ikafungwa kwa muda ili kuwapokea wagonjwa wa kipindu pindu,aisee wanafunzi tukaamishiwa pale Turwa na Nyamisangura,mimi nikajikuta nimepangiwa hapo Nyamisangura,aisee namna kulivyokuwa nilihisi ni mamtoni[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Nilipataga na kidemu kimoja cha kuitwa Neema,masikini sijui leo kitakuwa wapi,daaaah maisha haya[emoji1787]
2012_2014 nimepita Tarime Sec, Japo sio mzawa wa Tarime moja ya Mji mtamu sana Sabasaba Rebu, Sijui Goldland Hotel kubwa kuliko Angel House ndio ilikuwa na watoto wakali mnoo
 
2012_2014 nimepita Tarime Sec, Japo sio mzawa wa Tarime moja ya Mji mtamu sana Sabasaba Rebu, Sijui Goldland Hotel kubwa kuliko Angel House ndio ilikuwa na watoto wakali mnoo
Karibu Tarime mkuu ule raha
 
Mtu akileta story kama hii akaweka huku entertainment sina tatizo sana maana tunajua ni chai. Kuliko aweke kule aseme ni story ya kweli wakati tunaposoma tunaona ni ya uongo ila lengo ni kuwaburudisha watu ambao hawana la kufanya. So endelea kujitahidi watungie story ya maana siyo za kijinga jinga tu. Na upost kwa wakati. ANAKUSALIMIA SANA MPEMBA AMEKUMISS ANASEMA
Mtu akileta story kama hii akaweka huku entertainment sina tatizo sana maana tunajua ni chai. Kuliko aweke kule aseme ni story ya kweli

Kule wapi mkuu..?
inawezekana hatujajua chimbo lingine la mastory
 
Mtu akileta story kama hii akaweka huku entertainment sina tatizo sana maana tunajua ni chai. Kuliko aweke kule aseme ni story ya kweli

Kule wapi mkuu..?
inawezekana hatujajua chimbo lingine la mastory
Kuna sehemu nyingine ambazo huweka stories ambazo zinaonekana kama ni kweli. Huku inaonekana kabisa ni chai watu wanaburudika tu.
 
Kuna sehemu nyingine ambazo huweka stories ambazo zinaonekana kama ni kweli. Huku inaonekana kabisa ni chai watu wanaburudika tu.
Kuna mtu kasema hii stori niya kweli?

Acha kujiumiza akili mkuu acha watu wanywe chai washibe wakalale maana kwa hii baridi bila chai watu hawatoboi!
 
Kuna sehemu nyingine ambazo huweka stories ambazo zinaonekana kama ni kweli. Huku inaonekana kabisa ni chai watu wanaburudika tu.
Bahati nzuri simulizi zangu zote huwa ni chai ndiyo maana hata watu huwa hawaangaiki nazo,wanaohangaika nazo basi jua ya kwamba nao wanahamu na chai hizo wanywe kidogo wachangamke!
 
Kuna mtu kasema hii stori niya kweli?

Acha kujiumiza akili mkuu acha watu wanywe chai washibe wakalale maana kwa hii baridi bila chai watu hawatoboi!
Nashindwa kuelewa kwa nini hujaelewa nilichoandika. Na nimetumia kiswahili chepesi kabisa. Yaani unanipinga huku unakubaliana na nilichoandika. Unaponisoma soma tu kwa utulivu mbona mimi mtu wa amani na vijana nawapongeza mnapojituma kutunga stories. Sisi tunazeeka mnatakiwa nyie mchukue nafasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom