Eeeh Mungu nisamehe mimi na Mshikaji wangu Mabobo

Eeeh Mungu nisamehe mimi na Mshikaji wangu Mabobo

Amkeniiii amkeniiiii, amkeniiii jamani umughaka amerudi tenaaa amkeniiiii
 
Tarime ni sehemu hatari sana ukiwa mzinguwaji watu hawakawii kukuchinja
Mabobo kweli kiboko. Muhuni aliona jamaa hawezi kumla dada yake kizembe akaona bora achukue mahari mapema [emoji23][emoji23]
 
Tarime ni sehemu hatari sana ukiwa mzinguwaji watu hawakawii kukuchinja
Hapana mkuu hizi ni hisia tu, mji mzuri wa kuishi kwasasa nchi hii ni Tarime.

Huu mji umebarikiwa watu wakarimu, wapole na waungwana!
 
Sehemu ya 2.

Jamaa aliyekuwa akitulia chabo alikuwa amejificha kwenye ile migomba na sisi bila hili wala lile kimbe hatukujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea!

Tumechukua kama shilingi 500 tukasepa shuleni siku hiyo kumbe baada ya kuondoka jamaa mpiga na yeye alifanya yake[emoji1787]

Kweli,baada ya kufika shule ile muda wa mapumziko kama kawaida wapambe nuksi walikuwa kibwena,na kiukweli asikunadange mtu!,Hakuna Tajiri asimpenda Mpambe Nuksi(Chawa)Kila tajiri anapenda sifa,Kutukuzwa,Kumyenyekewa na kusifiwa!;Hizi sifa na sisi tulizipenda sana kupita maelezo.
Baada ya siku 3 tukaondoka na Mshikaji wangu Mabobo kuelekea kule kwenye lile shamba la migomba ili kuchukua angalau kiasi kingine cha fedha ili tuendeleze libeneke shule kama kawaida,ile tumefika wa kwanza kutazama kwenye ule mgomba na kuchukua hela alikuwaga Mabobo,sasa ile ameingiza mkono ndani ya jani la mgomba hakukuta tena ile hela,ametafuta sana na nilipoona anachana chana ule mgomba ikabidi nisogee nione ni kitu gani kilikuwa kinamsibu!,Aisee ilibidi ule mgomba tuupige chini na kuanza kuachana chana ili kujihakikishia kama kweli ile hela haipo!,mimi baada ya lile tukio ni kama nilichanganyikiwa kwasababu nilishaanza kuzoea maisha ya kishua na kusau umasikini!.

Baada ya kupekua sana na kujihakikishia hakukuwa na hela kila mtu alianza kumtuhumu mwenzake ya kwamba yawezaka akawa ameiba ile pesa,sasa uaminifu ukawa mdogo kwa kila mtu!.Aiseee ile ishu ilinifanya mimi na Mabobo kutokuzungumza kwa takribani miezi 2.

Kuna siku Mabobo alinifata Maskani akaniambia kuhusu zile hela,jamaa nilikuwa nimemzidi miaka ila naweza sema alikuwa mbele ya muda![emoji1787]

Mabobo "Mwanangu Umughaka unajua kumbe zile hela kuna jamaa ametuibia!"

Mimi " Nani alimeziiba?"

Mabobo " Ni dogo wa mzee kuruchumila"

Mimi "Sasa mbona ulikuwa ukidhani mimi niliye iba?"

Mabobo " Tuachane na hayo,mimi nilidhani wewe ndiye ulichukua kwasababu ni mimi na wewe pekee ndiyo tulielewa hili jambo"

Mimi "Huyo dogo umemuona na hizo hela?"

Mabobo " Kaka yake ndiyo kaniambaia"

Aliendelea "Hebu twende kwenye bwawa la kuogelea la Waitara,kaka yake kaniambia yupo kule anapiga mbizi"

Tukaondoka zetu kwa miguu kuelekea kwenye makao ya Aliyekuwa kuwa mkuu wa Majeshi ya JWTZ Mwita Waitara,Lile eneo lilikuwa na Bwawa(Lambo)ambalo vijana wote wa Tarime mjini ungewakuta wanaogelea kwenye lile bwawa,lile Bwawa lilikuwa ndilo bwawa ambalo namlaka ya Maji ya Tarime Mjini ilikuwa ikuchukulia maji yake pale,pia Uongozi na Mamlaka zilikuwaga zimepiga marufuku watu kuogelea kwenye lile bwawa lakini kwakuwa vijana tulikuwa vichwa maji hatukusikia,sasa ukisikia kufa kwa nyani miti yote huteleza ndiyo ilikuwa siku hiyo!.

Kilichotupeleka pale mimi na Mabobo ilikuwa kumchukua yule kijana wa Kuruchumila atueleze zile hela alikuwa amezipeleka wapi lakini badala yake baada ya kufika pale kwenye lile bwawa na sisi tukaanza kuogelea kwa vurugu zote utadhani kweli tulikuwa tunaweza kuogelea kumbe ilikuwa ni viherehere tu na ujuaji wa kijinga!.

Haukupita muda tukasikia "Hakikisha wote wanapita hapo kwenye veranda wanaingia ndani"

Aisee kuja kutahamaki kumbe kulikuwa na watu wamevaa kombati(Wanajeshi) wakiwa 4 wamezunguka lile bwawa(lambo) kwa sehemu muhimu kuhakikisha hakuna mtu atakayetoka salama,na kiukweli hakuna aliyetoka salama,kila mmoja alipotoka kwenye lile lambo alihakikisha anavaa nguo alizokuwa amevua na kuziacha kando ya lile lambo.Baada ya wote kuvaa nguo tukachukuliwa na kupelekwa kambi ya Jeshi ambayo haikuwa mbali na lile eneo.

Sema kwa miaka ile nilikuwaga siwaogopi kabisa wanajeshi,sijajua ni kwasababu nilikuwa bado mdogo au ilikuwa ni kwasababu gani!.

Sauti "Haya wote ingieni mle ndani"

Ilikuwa ni sauti ya Mwanajeshi mmoja ambaye alisikika akituambia hivyo!.Baada ya kuingia kwenye ile nyumba ambayo ilikuwa haijaezekwa kwa juu tulikuta kuna kofia kibao kama zile za Platoon,sasa baada kukuta zile kofia wale wanajeshi walituambia kila mmoja avae yake hata kama haikutoshi uvae hivyo hivyo na ajiandae kukabiliana na sheria kali.

Mjeshi mmoja "Vaeni hizo kofia!"

Kila mmoja alivaa yake.

Aliendelea "Sasa leo ndiyo mtajua kama nyinyi ni wanaume au sisi ndiyo wanaume"

Aliendelea "Nyie sini wakurya mliosarwa bila ganzi?"

Wote " Ndiyo"

Mjeshi " Sawa tunataka tuone uanaume wenu"

Itaendelea........
 
Sehemu ya 2.

Jamaa aliyekuwa akitulia chabo alikuwa amejificha kwenye ile migomba na sisi bila hili wala lile kimbe hatukujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea!

Tumechukua kama shilingi 500 tukasepa shuleni siku hiyo kumbe baada ya kuondoka jamaa mpiga na yeye alifanya yake[emoji1787]

Kweli,baada ya kufika shule ile muda wa mapumziko kama kawaida wapambe nuksi walikuwa kibwena,na kiukweli asikunadange mtu!,Hakuna Tajiri asimpenda Mpambe Nuksi(Chawa)Kila tajiri anapenda sifa,Kutukuzwa,Kumyenyekewa na kusifiwa!;Hizi sifa na sisi tulizipenda sana kupita maelezo.
Baada ya siku 3 tukaondoka na Mshikaji wangu Mabobo kuelekea kule kwenye lile shamba la migomba ili kuchukua angalau kiasi kingine cha fedha ili tuendeleze libeneke shule kama kawaida,ile tumefika wa kwanza kutazama kwenye ule mgomba na kuchukua hela alikuwaga Mabobo,sasa ile ameingiza mkono ndani ya jani la mgomba hakukuta tena ile hela,ametafuta sana na nilipoona anachana chana ule mgomba ikabidi nisogee nione ni kitu gani kilikuwa kinamsibu!,Aisee ilibidi ule mgomba tuupige chini na kuanza kuachana chana ili kujihakikishia kama kweli ile hela haipo!,mimi baada ya lile tukio ni kama nilichanganyikiwa kwasababu nilishaanza kuzoea maisha ya kishua na kusau umasikini!.

Baada ya kupekua sana na kujihakikishia hakukuwa na hela kila mtu alianza kumtuhumu mwenzake ya kwamba yawezaka akawa ameiba ile pesa,sasa uaminifu ukawa mdogo kwa kila mtu!.Aiseee ile ishu ilinifanya mimi na Mabobo kutokuzungumza kwa takribani miezi 2.

Kuna siku Mabobo alinifata Maskani akaniambia kuhusu zile hela,jamaa nilikuwa nimemzidi miaka ila naweza sema alikuwa mbele ya muda![emoji1787]

Mabobo "Mwanangu Umughaka unajua kumbe zile hela kuna jamaa ametuibia!"

Mimi " Nani alimeziiba?"

Mabobo " Ni dogo wa mzee kuruchumila"

Mimi "Sasa mbona ulikuwa ukidhani mimi niliye iba?"

Mabobo " Tuachane na hayo,mimi nilidhani wewe ndiye ulichukua kwasababu ni mimi na wewe pekee ndiyo tulielewa hili jambo"

Mimi "Huyo dogo umemuona na hizo hela?"

Mabobo " Kaka yake ndiyo kaniambaia"

Aliendelea "Hebu twende kwenye bwawa la kuogelea la Waitara,kaka yake kaniambia yupo kule anapiga mbizi"

Tukaondoka zetu kwa miguu kuelekea kwenye makao yalipokokuwa ya Aliyekuwa kuwa mkuu wa Majeshi ya JWTZ Mwita Waitara,Lile eneo lilikuwa na Bwana(Lambo)ambalo vijana wote wa Tarime mjini ungewakuta wanaogelea kwenye lile bwawa,lile Bwawa lilikuwa ndilo bwawa ambalo namlaka ya Maji ya Tarime Mjini ilikuwa ikuchukulia maji yake pale,pia Uongozi na Mamlaka zilikuwaga zimepiga marufuku watu kuogelea kwenye lile bwawa lakini kwakuwa vijana tulikuwa vichwa maji hatukusikia,sasa ukisikia kufa kwa nyani miti yote huteleza ndiyo ilikuwa siku hiyo!.

Kilichotupeleka pale mimi na Mabobo ilikuwa kumchukua yule kijana wa Kuruchumila atueleze zile hela alikuwa amezipeleka wapi lakini basala yake baada ya kufika pale kwenye lile bwawa na sisi tukaanza kuogelea kwa vurugu zote utadhani kweli tulikuwa tunaweza kuogelea kumbe ilikuwa ni viherehere tu na ujuaji wa kijinga!.

Haukupita muda tukasikia "Hakikisha wote wanapita hapo kwenye veranda wanaingia ndani"

Aisee kuja kutahamaki kumbe kulikuwa na watu wamevaa kombati(Wanajeshi) wakiwa 4 wamezunguka lile bwawa(lambo) kwa sehemu muhimu kuhakikisha hakuna mtu atakayetoka salama,na kiukweli aliyotoka salama,kila mmoja alipotoka kwenye lile lambo alihakikisha anavaa nguo alizokuwa amevua na kuziacha kando ya lile lambo.Baada ya wote kuvaa nguo tukachukiliwa na kupelekwa kambi ya Jeshi ambayo haikuwa mbali na lile eneo.

Sema kwa miaka ile nilikuwaga siwaogopi kabisa wanajeshi,sijajua ni kwasababu milikuwa bado mdogo au ilikuwa ni kwasababu gani!.

Sauti "Haya wote ingieni mle ndani"

Ilikuwa ni sauti ya Mwanajeshi mmoja ambaye alisikika akituambia hivyo!.Baada ya kuingia kwenye ile nyumba ambayo ilikuwa haijaezekwa kwa juu tulikuta kuna kofia kibao kama zile za Platoon,sasa baada kukuta zile kofia wale wanajeshi walituambia kila mmoja avae yake hata kama haikutoshi uvae hivyo hivyo na ajiandae kukabiliana na sheria kali.

Mjeshi mmoja "Vaenj hizo kofia!"

Kila mmoja alivaa yake.

Aliendelea "Sasa leo ndiyo mtajua kama nyinyi ni wanaume au sisi ndiyo wanaume"

Aliendelea "Nyie sini wakurya mliosarwa bila ganzi?"

Wote " Ndiyo"

Mjeshi " Sawa tunataka tuone uanaume wenu"

Itaendelea........
Da
 
Mkuu ulisoma Turwa au Nyamisangura....?
Nimeishi mitaa hii, chini ya uwanja wa hizi shule kuna dispensary inaitwa Ronsoti Dispensary, nilikuwa naishi mitaa ya barabara ya posta, JJ, Chriss pub, CMG hadi sabasaba kwenye kichuri nilikuwa nafika (2012-2013)
 
Jirani na kwa namba 3?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom