Sitakuja kurudi kliniki za chanjo na maendeleo ya makuzi ya watoto peke yangu bila mke au msaidizi wa kazi

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,277
21,455
Leo kiherehere cha kujifanya msomi civilazed mwenye kupenda haki sawa kimeniisha nilivyompeleka mwanangu wa siku 42 kliniki peke yangu bila kuwa na mama yake ndani ya chumba cha kliniki kwa kumuacha kwenye gari eti alikuwa ana kizunguzungu.

Nimejikuta nimepoteza confidence/kujiamini na aibu, kwenye ile foreni ya kupima Uzito nilikuwa peke yangu mwanaume mwenye ndevu, kati ya wanawake karibia 100, unasikia sauti zao mtoto usimfanye hivi, mbebe vile kila moja anakuangalia wewe loh,

Sasa pale kwenye benchi ya kusubiria chanjo kuna stori zao wanazopiga wanazijua wenyewe mimi nimeshindwa kabisa kuchangia chochochote, nilikuwa ' odd man out' wanacheka mimi natabasamu tu sina hata la kuongea, yale masaa mawili kwangu yamekuwa kama siku nzima.

Hivi kwanini wanaumme wa ki Tanzania hawana utamaduni wa kusindikiza wake zao au ni sababu kama hii ya kwangu, nilidhani nitakutana na wanaumme wenzangu lakini wapi kumbe wale wanaume niliona kwa mbali walikuwa wahudumu wa pale sio wazazi

Mzazi.jpg
 
You did it for your own kid and your wife, nothing else should matter

Mimi nimewahi mpeleka clinic peke yangu na nilipata support kubwa sana kwa wamama wote na wahudumu, for the first time wamama walinipisha kwenye foleni, nikawa wa kwanza na kunisaidia kufanikisha zoezi nikasepa fasta.

Mama mtoto alisafiri kikazi

if chance present itself, I will definitely do it again coz it did not affect my ego at all.
 
Sawa mkuu ila it requires some degree of braveness mimi naturally nina aibu mbele ya alaiki ya wanawake nakosa confedance, i really paid the price.
 
Mkuu wanaume wengi tu wanapeleka watoto clinic labda inategemea na eneo ulilopo.
Tena wanaume wakienda clinic wanapewa kipaumbele cha kuhudumiwa kwanza.
Huku kwetu hao wa swahili bado naona sasa muwahamasisheni, mkiwa nao faragha
 
Sawa mkuu ila it requires some degree of braveness mimi naturally nina aibu mbele ya alaiki ya wanawake nakosa confedance, i really paid the price.
Linapofika swala la mtoto wako, usione aibu. Nilifanya zoezi hili la kumpeleka clinic Binti yangu, mama yake akiwa masomoni, mpaka akamaliza clinic zote. Nilihakikisha chanjo zote anapata. It's no big deal. Wale wamama walinizoea na walikuwa wakiniona wananipa kipaumbele.
 
Kumbe we mke wo ni wale wenye degree walio ajiliwa duh, loh nashangaa how you people enjoye malehood, with women of much know......
 
Back
Top Bottom