nimeshakujibu, ila pia kwani watanzania huwa tunachagua nini?!. Sisi watanzania sio kweli kuwa ni wepesi wa kusamehe na kusahau, bali hatunaga hata kumbukumbu tumetendwa nini, ndio maana kila siku ccm inakuja na ahadi mpya, hakuna kumbukumbu yoyote ya iliahidi nini zamani na nini kilitekelezwa, sisi tunaendelea kuichagua tuu na kuichagua na kuichagua!. 2005, ccm ilikuja na kauli mbiu ya " maisha bora kwa kila mtanzania" kwa kutumia "kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya!", 2010, tukaletewa " maisha bora kwa kila mtanzania, yanawezekana " kupitia kwa "kasi zaidi, ari zaidi na nguvu zaidi!" ila hakuna tathmini wala kumbukumbu ya tulichoahidiwa na kilichofanyika!, sisi ni watu wa kupokea tuu!.
Amini nakuambia, kama afya ya el sio mgogoro, na ccm ikamsimamisha lowassa, hakuna mpinzani yoyote atakaefurukuta kwenye urais, ubunge yes!
we pasco unavyonikunaaa, we acha tu. Ngoyayi go