Edward Lowassa on ITV!-Dakika 45 Part II!.

Edward Lowassa on ITV!-Dakika 45 Part II!.

Nevertheless, bunge la mwaka 2015, ataunguruma sana kumbomoa JK na mtandao wake, atahakikisha walomtundika msalabani kwa Richmond, wanasulubiwa!, yeye atasafishwa, atatakatishwa, atakaswa, atapakwa mafuta tayari kwa 2015, kama ni kweli yuko fit, basi mkae mkijua, kama CCM watamsimamisha Lowassa, 2015, ni CCM Tena!.

Mkuu Pasco,

Najua wewe ni mfagiliaji wa El toka zama! Nakuhakikishia hapo kwenye red, "over JK's dead body" Hawa jamaa wamekwisha patanishwa na ikashindikana, kisa unafiki na ukigeu geu wa JK. JK ameshajulikana msimamo wake si kumuunga mkono EL, and this is very open to themselves! At the same time, EL anaapa it is either him or CCM dies! Hapa ndipo ninapoungana na wewe kwenye post yako juu kuwa kwayo EL, upinzani utaingia madarakani!!!

My opinion is, EL ni mgonjwa na kwa hali ile hawezi kabisa kugombea 2015, ninachoweza sema anaweza kuweka kijana wake muaminifu, possibly Dr. Nchimbi.
 
Mh.
lowasa nadhani wa tz wengi tunakujuwa mkuu kwa mamuzi nadhani ingekuwa wewe ni pinda au kwenye suala la jairo kila mtz angefurahia mamuzi yko cha msingi m4c ni waelewa sana!
Amna mtz mwenye shaka na m4c ushauri wangu panda kwenye jukwaa na m4c ungama sina shaka wewe ni mjuzi wa kujieleza unaye pendwa na wtz.
sina shaka na wewe waweza kulikomboa taifa hili teule linalo fanywa shamba la bibi na babu ambao hvi sasa ni marehem
 
Mkuu Pasco,

Najua wewe ni mfagiliaji wa El toka zama! Nakuhakikishia hapo kwenye red, "over JK's dead body" Hawa jamaa wamekwisha patanishwa na ikashindikana, kisa unafiki na ukigeu geu wa JK. JK ameshajulikana msimamo wake si kumuunga mkono EL, and this is very open to themselves! At the same time, EL anaapa it is either him or CCM dies! Hapa ndipo ninapoungana na wewe kwenye post yako juu kuwa kwayo EL, upinzani utaingia madarakani!!!

My opinion is, EL ni mgonjwa na kwa hali ile hawezi kabisa kugombea 2015, ninachoweza sema anaweza kuweka kijana wake muaminifu, possibly Dr. Nchimbi.
Mkuu Nyunyu, hakika wewe uu miongoni mwa ma great thinkers wachache sana tulionao humu jukwaani, keep on reading me in between the lines, we'll finally reach there, japo jina la jf ni home of great thinkers, hawa ma great thinkers wengi tulio nao humu, I doubt, if some have even that brain to think, let alone thinking great!.

Mimi nitaendelea kugawa dose humu humu na siku za usoni, nitakwenda extra mile to reach the masses, kuhamasisha CCM imsimamishe Lowassa ili kupitia kwayo, litimie lile neno, "Rais wa 2015 lazima atoke Kaskazini" na taifa letu liupate ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Pasco.
 
Henge,
Mtandao wa Lowasa serikalini ni kama vile umemalizika sasa baada mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, maRC na hivi karibuni maDC. Tatizo limebaki BUNGENI tu ambako wakati uchaguzi linavunjwa na kila mbunge kulilia nafsi yake zaidi baada ya hapo.
Kwenye CCM nako huu utaratibu mpya wa kuwapata wajumbe wa NEC toka ngazi ya wilaya nako kumeharibu sana mitandao sugu ya akina Lowasa. Wagombea wa NEC-CCM wametakiwa kikanuni wasiwe wanashikilia nafasi nyingine za kudumu kama UBUNGE.
Sekretarieti ya akina Mukama, Nape, January, Mwigulu,..., nayo haitabiriki na kuingilika kirahisi kama ile ya Mzee Makamba.Nguvu kubwa aloobaki nayo Lowasa na washirika wake ni PESA ambayo watapata taabu sana kuitumia kwa taratibu na kanuni za sasa ndani ya chaguzi za CCM zinazoendelea sasa.

Mkuu sidhani kama wamemaliza woote kwenye wakuu wa wilaya na mikoa!
Ninahakika kwa jinsi lowasa alivyojijenga ni Ngumu sana kwa ccm kumaliza damu ya lowasa ndani ya CCM,
Huyu jamaa anapendwa ndani ya chama na anaogopwa sana mkuu, Na ukumbuke lowasa anapesa nyingi na ndani ya ccm wenye tamaa na njaa ya pesa niwengi sana, kumbuka kama 70% ya kina mama wa ccm wanampenda sana huyu ndugu.
 
Wanabodi,
Mtanzania, vinginevyo kama ni Lowassa ndie angekuwa rais, Tanzania isingekuwa hapa ilipo, na kusingalikuwepo hata hilo hitaji la ukombozi wa pili wa Mtanzania maana Tanzania ingeshakuwa peponi!.

Hivyo wale wote wenye kulitakia mema taifa hili, mshukuruni sana EL na JK, vingenevyo 2015, ingekuwa ni hadithi ile ile tulioizoea!.

Pasco.
Pasco
Raisi wako mtarajiwa atakuwa anaweza kutembea na kusema ifikapo 2015?

Una moyo, Pasco. :redface:

Kwa hiyo,EL akiwa Rais Tanzania itakuwa peponi?
Au motoni?
EL aliwahi kuwa no.2 hapa Tz na kweli tulionja utamu wa pepo yake!!! Alijiuzulu kwa tuhuma ipi vile?
 
Rais wangu 2015 ni Shamsi Vuai Nahodha kama tutalazimika kuendelea na CCM. Amekuwa WaziriKiongozi SMZ; akawa waziri wa Mambo ya Ndani na sasa ni Waziri wa Ulinzi na JKT. Atapata mtu kama Dr Asha Rose Migiro kumsaidia kama Makamu wa Rais au Waziri wa Mambo ya Nje

kosa litakaloizamisha ccm 2015 ni kumsimamisha mzanzibar, ccm inatakiwa kufanya uamuzi mgumu wa kumuandaa mtu mmoja kuanzia sasa mwenye record nzuri na anayekubalika kwa watz wengi wenye elimu kubwa na ndogo. Kati ya wote ni mwakyembe pekee ambaye naona anaweza kuuzika mijini na vijijini .. nguvu ya pesa na mtandao vitafanikiwa kwenye kura za maoni tu na si mbele ya wapiga kura.
 
Jamaa ni mwanasiasa na nasikia kuwa ni mwanamuziki na ukiunganisha hizo kazi mbili unapata picha kuwa hii ni sanaa tu.Kwa hesabu za harakaharaka jamaa keshapata wafuasi lakini kwa mtazamo wangu kama EL ni mwanasiasa basi hakuna tofauti na Sidhani kama ikulu itamfaa.

ELIMU KWANZA ilishawekwa kwenye majaribio tukapata hizo shule maarufu za KATA
Kuhusu hilo swala la huo utajiri wetu ambao anasema kwamba tuugawe taratibu sifiki bei nahisi anajichanganya or kwa lugha nyingine anasema wambakishie hivyo vitalu na yeye or wamgawie 'cunajua hayupo kwenye mgao kwa hiyo wakimaliza'

Nadhani haya ni maneno ya mkosaji.Ila I appreciate his perspective ana mtazamo mzuri ila bado ni mwanasiasa

Watanzania tutakombolewa pale tutakapokuwa na mapinduzi ya wafanyakazi,'workers whose blood and sweat ndo inajenga hii nchi tuwatoe wanasiasa katika uongozi then tuwaweke wafanyakazi;watu wenye maslahi ya umma.Patriots
 
Akija huku atakuwa mvamiza,ataharibu mgao tu,M4C ni kwa ajili ya kizazi kipya tunahitaji kura yake 2015.Ila co atutie doa.
 
Huyu anatambulika hata kwa utendaji wake pindi akiwa waziri mkuu maana hata alipokuwa akitembelea halmashauri za wilaya wakurugenzi walikuwa hawalali kwa either kukemewa jukwaani au hata kusimamishwa asiendelee kusoma utekelezaji hewa( wa kubumba) ila kwa sasa hivi hakuna kiongozi hata huyo aliyepewa nafasi yake hana lolote tofauti na kufungua mawe ya msingi pamoja na kutoa maagizo yasiyotekelezwa na wasaidizi wake wa chini.
 
ipo siku watu wataelewa kuwa EL hausiki na richmond? sisi wachache ndio tunaojua fact za richmond, tunamlaumu sana EL kwa nini alijiuzuru. Wenye kumbukumbu siku EL alipojiuzuru Bungeni alihojiwa na Tido mhando wa TBC kwenye mazungumzo ambayo yalirekodiwa akiwa kwenye nyumba ya waziri mkuu ya Dodoma. yale mazungumzo yalikuwa yarushwe na TBC alhamisi usiku. Tido alitaka airushe kama ilivyo bila kuedit. wapambe wa JK walizipata taarifa very late kwamba EL anamwaga mboga, kipindi kilipotaka kwenda hewani tu yaani tido anamtambulisha EL, kikakatwa hapohapo. anayetaka kujua Ngoyayi aliongea nini amuulize Tido atamweleza vizuri, kwa kuwa Tido hayupo tena kifungoni(TBC) yupo huru (mwananchi).

Najua EL hawezi kuongea tena hii issue mpaka JK atakapomaliza uraisi wake, ila issue ya richmond itampa tabu sana katika harakati za uraisi. Haitoshi tu kusikia kuwa EL amemweleza JK kwenye vikao vya kamati kuu dodoma kwamba yeye JK ndio aliyekuwa anampa maelezo kuhusiana na Richmond, wananchi wanataka wamsikie yeye EL mwenyewe.

I WILL ALWAYS BE THE TRUTHFUL DISCIPLE OF NGOYAYI
Hiyo ni haki yako na huo ni msimamo wako, nakubali.

Lakini ujue kuwa Lowassa hana chembe ya usafi kama na CCM ilivyo kinyaa ktk macho na mioyo ya Watanzania walio wengi.

EL ni mwanasiasa. Hapo alikuwa anafanya siasa, ndio maana akasema maneno kama eti hakubaliani na sera yao ya kilimo kwanza. Of coz, anavyo vipaumbele vyake vikubwa na umuhimu ni:-
1) Yeye na Urais (ili akamilishe mishe mishe zake na kulipiza kisasi pale anapotaka)
2) Kukilinda chama chake kwa gharama ya Taifa
3) Kuirithisha ego yake kuwa jina lake limewekwa ktk historia ya Tz. (hii ni pamoja na wanamtandao wake kufaidi nchi kwa kwenda mbele)

Je hivyo ndivyo Watanzania wa leo wanavyovihitaji? Je nchi hii ktk miaka 10-20 ijayo itakuwa wapi na huyu mlafi?

Ninyi mashabiki na wapambe wake mshaurini boss wenu kuwa, hali ya nchi ilivyo na kwa siasa za sasa na zijazo HAFAI.
Mngemshauri tu atafute pa kukimbilia maana CHADEMA wakiingia kunako nguvu 2015 huyu jamaa yatampata makubwa.
 
Pasco nimekuelewa, ili yatimie J. K alitakiwa kuwa Rais na ili tufunike mazima EL anatakiwa kuwa mgombea urais kw tiketi ya CCM 2015. J. K ni chaguo la Mungu
 
Nimeipenda hii...ha ha ha, hata mimi the same, kimoja kinachonikumbusha huyu mtu ni kuwa Nyerere alimkataa
Bro, hivi nikweli mwalimu alimkataa au chumvi imetiwa ktk hili, naomba nijulishwe huyu jamaa namkubali sana.kwa misimamo yake.
 
Kwa hiyo,EL akiwa Rais Tanzania itakuwa peponi?
Au motoni?
EL aliwahi kuwa no.2 hapa Tz na kweli tulionja utamu wa pepo yake!!! Alijiuzulu kwa tuhuma ipi vile?

Mkuu hapo kwenye red bold kuna siri kubwa sana. Na nina kuhakikishia wajuayo siri hii ni watu watatu tu, EL,JK na RA. Pasco aliwahi sema kwenye tundiko lake humu ndani kuwa and I quote "...kwa yeyote yule anayesema EL ni fisadi ataje ufisadi wake..." That time nakumbuka wengi tuiishia kusema "Richmond"

Hakika nakwambia haya hatuyajui ni usiku wa giza! Mwenye makshfa mengi Nishati na Madini si EL ni mwengine kabisa na RA na EL wanamjua! Sema kwa usalama na heshima plus weledi, linabaki kuwa "fumbo la imani" Kati ya mambo yanampa EL drive ya ku-fight mpaka kielewe, hili ni moja wapo, ili siku ile aje awahakikishie waTZ si yeye!!

Hakika mnyukano wa 2015 utakuwa mkali kuzidi maelezo!!
 
Kauli ya Mh. Lowasa ktk kipindi cha dk 45 ITV si ya kubezwa na kudharauliwa. Kwani elimu ktk suala lolote ni muhimu, huwezi ukawa na mkakati wa kuondoa kupanua njia za uchumi bila kuwaandaa watu wake kielimu na kisaikolojia jinsi ya kufanikisha na kuishi kwenye hayo mafanikio. Watanzania wa zamani walilima kwa kutizama majira ya mvua (mpaka leo bado wapo).
Naomba tuheshimu kauli yake na tuijadili kwa mapana.
 
Mkuu hapo kwenye red bold kuna siri kubwa sana. Na nina kuhakikishia wajuayo siri hii ni watu watatu tu, EL,JK na RA. Pasco aliwahi sema kwenye tundiko lake humu ndani kuwa and I quote "...kwa yeyote yule anayesema EL ni fisadi ataje ufisadi wake..." That time nakumbuka wengi tuiishia kusema "Richmond"

Hakika nakwambia haya hatuyajui ni usiku wa giza! Mwenye makshfa mengi Nishati na Madini si EL ni mwengine kabisa na RA na EL wanamjua! Sema kwa usalama na heshima plus weledi, linabaki kuwa "fumbo la imani" Kati ya mambo yanampa EL drive ya ku-fight mpaka kielewe, hili ni moja wapo, ili siku ile aje awahakikishie waTZ si yeye!!

Hakika mnyukano wa 2015 utakuwa mkali kuzidi maelezo!!

Mkuu Nyunyu, sio kweli kuwa siri ya kujiuzulu kwake, naijua mimi tuu!.

1. Kwenye Ripoti ya Mwakiembe, kuna vitu aligundua lakini alimezea!.

2. Hawakumuita EL kumhoji, hii ni kinyume kabisa cha "principles of natural justice", "no one is condemned unherd"!.

3. Sitta alimbrief JK ile ripoti kabla haijawasilishwa bungeni, na JK akatoa go ahead ya kumtwika EL!.

4. Ndio maana maazimio yote ya kuwawajibisha watendaji wa serikali, yalipuuzwa!.

5. EL wakati akiliaga bunge, alisema najua issue ni u-PM, hivyo nawapeni mlichotaka!.

6. Kuna watu walifanya sherehe na ile step down, wakijua sasa njia ni nyeupe, kwa sasa wanahakikisha EL harudi,
maana kwao itakuwa ni kilio cha kusaga meno.

7. All the key players wanajua na name of the game, RA aliingia tuu na Dowans just to save face ya Richmond, as long
as sasa ni Simbion, now the picture is very clear, kila mtu kimya!.

8. Hujanisikia nikimtaja Sitta wala Mwakiembe kwa urais wa 2015 kwa sababu they are "gone case"!.

9. Bado EL is the one ond only best CCM has for 2015 akifuatiwa na Membe!.

10. Naamini wewe Mkuu Nyunyu pia unaujua ukweli, jf tunaujua ukweli, na tukifikia darajani, Watanzania wataujua
ukweli na ndipo tutavuka daraja!.

Pasco.
 
Huyu anatambulika hata kwa utendaji wake pindi akiwa waziri mkuu maana hata alipokuwa akitembelea halmashauri za wilaya wakurugenzi walikuwa hawalali kwa either kukemewa jukwaani au hata kusimamishwa asiendelee kusoma utekelezaji hewa( wa kubumba) ila kwa sasa hivi hakuna kiongozi hata huyo aliyepewa nafasi yake hana lolote tofauti na kufungua mawe ya msingi pamoja na kutoa maagizo yasiyotekelezwa na wasaidizi wake wa chini.

Mimi si mshabiki sana wa siasa za tz ila ni mfuatiliaji mzuri ingawa sina mrengo wa chama chochote,ki ukweli mzee wetu EL kwa muda mfupi aliokuwa PM alithubutu kuwanyoosha watendaji wazembe,labda kila mmoja ajaribu ku-recall namna alivyowakimbiza wakuregenzi wazembe wa halmashauri,ni mtu wa KUTHUBUTU na akiamua kusimamia jambo anaweza,labda wadau mjaribu kufananisha uwezo wake wa maamuzi na aliyemtangulia kisha mtaelewa ninamaanisha nini,mzee EL hakuwa mtu wa ''kulia lia'' katika utendaji wake, all in all akiamua jambo he has that courage to push it forward!
 
lowassa-top-safi.jpg
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ..........:A S 465:HAHAHHAHHAHHAHHAHHHA
 
Lowassa: Siungi mkono Kilimo Kwanza
"Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza," alisema Lowasa na kuongeza:Alitoa mfano wa nchi ya Indonesia akisema inaendesha uchumi wake kwa kilimo cha michikichi, ambayo mbegu zake zimetoka Tanzania... "Lakini Tanzania iliyotoa michikichi hiyo sasa ni moja ya wateja wa mafuta hayo yanayotoka Indonesia.""Ningelikuwa na uwezo wa kutoa uamuzi, vijana wetu wa JKT (Jeshi la Kujenga Taifa), ningewapa kazi ya kuanzisha mashamba ya michikichi nchi nzima kwani nchi yetu imejaliwa kuwa na ardhi kubwa na yenye rutuba, mapori yapo mengi," alisema Lowassa.
 
Mkuu hapo kwenye red bold kuna siri kubwa sana. Na nina kuhakikishia wajuayo siri hii ni watu watatu tu, EL,JK na RA. Pasco aliwahi sema kwenye tundiko lake humu ndani kuwa and I quote "...kwa yeyote yule anayesema EL ni fisadi ataje ufisadi wake..." That time nakumbuka wengi tuiishia kusema "Richmond"

Hakika nakwambia haya hatuyajui ni usiku wa giza! Mwenye makshfa mengi Nishati na Madini si EL ni mwengine kabisa na RA na EL wanamjua! Sema kwa usalama na heshima plus weledi, linabaki kuwa "fumbo la imani" Kati ya mambo yanampa EL drive ya ku-fight mpaka kielewe, hili ni moja wapo, ili siku ile aje awahakikishie waTZ si yeye!!

Hakika mnyukano wa 2015 utakuwa mkali kuzidi maelezo!!

Unapojua uovu na mwovu na ukachukua jukumu la kumficha na kujibebesha ovu hilo, hapo tutampa jina gani?
Tafuta lililo zuri tu, je tutamwita malaika? mlafi? msafi? maridadi?rais mtarajiwa? mpenda madaraka?mhanga?mbuzi wa kafara?
Halafu nisaidie hapa...anayemsaidia mwizi kuiba ............. !!!!!

Kama aliamua au alishawishiwa kujipakaza kinyesi halafu apite mbele ya kadamnasi ya watu, kila mtu ataziba pua!!!!

Tutasubiri mpaka hapo atakapoitoa/ atakapoitema hiyo siri, in the mean time, sifa inayomfaa ni kuwa alifisidi taifa kwa hiyo ni f..........!
 
Mimi si mshabiki sana wa siasa za tz ila ni mfuatiliaji mzuri ingawa sina mrengo wa chama chochote,ki ukweli mzee wetu EL kwa muda mfupi aliokuwa PM alithubutu kuwanyoosha watendaji wazembe,labda kila mmoja ajaribu ku-recall namna alivyowakimbiza wakuregenzi wazembe wa halmashauri,ni mtu wa KUTHUBUTU na akiamua kusimamia jambo anaweza,labda wadau mjaribu kufananisha uwezo wake wa maamuzi na aliyemtangulia kisha mtaelewa ninamaanisha nini,mzee EL hakuwa mtu wa ''kulia lia'' katika utendaji wake, all in all akiamua jambo he has that courage to push it forward!

Mkuu with all due respect hapa napingana na wewe, huwezi kuwanyoosha watendaji wako kwa kuwadhalilisha na kuwatukana! Kwa uzembe wao upanda mmoja unaona ni sawa lakini haikuondoa tatizo!! Pamoja na mazuri yake na nia yake nzuri, EL alishindwa kupanga team yake kutekeleza mipango yake, it seems his plans was on his minds, and so, soon as he left all went with him!!!

Somehow, ndhani kwa sababu za kisiasa, EL lacks some of managerial skills!!
 
Back
Top Bottom