Pasco Heshima mbele!
Naomba unijuze kama kweli CCM watakuwa tayari kumsimamisha EL kuwa mgombea wao wa nafasi ya urais!
Mkuu Skills4ever, hili ni swali zuri kwa sababu linahusu utayari wa CCM kumsimamisha EL,
1. Kwa kuanzia, naomba kwanza nisisitize kuwa CCM kama chama tawala, ndicho kimelifikisha taifa letu hapa lilipo, CCM yenyewe tuu is not an entity, hivyo CCM haina matatizo, wenye matatizo ni viongozi wa CCM, hivyo wabaya wetu waliotufikisha hapa sio CCM bali ni viongozi wa CCM na hao ndio tutakao waadhibu kwa kuwachapa bakora vilivyo, come 2015!. Lakini pamoja na ubaya wote wa viongozi hawa wa CCM, miongoni mwao, bado kuna watu safi CCM, watu wenye impecable integrity ya kuliongoza taifa hili kwa uadilifu wa hali ya juu na kuondoa uoza wote uliomo ndani ya chama chao!.
2. Hakuna ubishi CCM kama chama tawala, kimechokwa, Watanzania wanalijua hilo na CCM wenyewe pia wanalijua hilo, tena in fact kilichokwa siku nyingi, na udhibitisho ni idadi kubwa ya Watanzania wanaojiandikisha kupiga kura halafu hawapigi kura kutokana na kukata tamaa na CCM lakini pia kulikuwa hakuna any serious mbadala kwa upande wa bara, hivyo CCM imekuwa ikiendelea kuchaguliwa kwa mazoea tuu, kwa 2015, Chadema inaonyesha seriousness zake, hivyo kwa kuchaguliwa tena kwa CCM 2015 sio kwa mazoea tena, lazima ifanyike kazi, tena kazi kubwa na sio ile ya t-shirt, kofia na shibe ya siku 1!.
3. Ni kwa kuzingatia hayo, mgombea wa CCM 2012, lazima awe ni mgombea powerful, mwenye uwezo usiotia shaka kuwa akisimama, wapinzani watany'ongonyea, ndani ya CCM hakuna mwingine yoyote mwenye uwezo huo zaidi ya EL, hii inamaani CCM watake, wasitake, they have one and only option ya kumsimamisha EL, ila kiukweli, kufuatia afya yake kuwa mgogoro, kwa jinsi nilivyomuona akizungumza, anatoa maneno makali kwa sauti yenye fire on hisi ayes, and fear is the weapon on his heart, hivyo body language isaonekana wazi, "he is a sick man"!, hivyo hawezi kuhimili mikiki mikiki ya 2015, hivyo CCM kulazimika kumsimamisha Membe, na itamlazimisha EL avunje kambi yake na kuihamishia kwa Membe!.