Wanabodi,
Nawaombeni tumsikilize kwa makini sana haswa kwa kuzingatia siasa za nchi hii, hazitabiriki sana, haswa kipengele cha "Umdhanie Siye kumbe Ndiye" na pia uwezekano wa "Jiwe walilolikataa waashi, kufanywa kuwa jiwe kuu la pembeni"!.
Kipindi kimekwisha.
My Take.
Nimemsikiliza kwa makini sana, kiukweli namkubali huyu jamaa kwa 100%!.
Wale wenzangu na mimi, wenye mategemeo ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa mwaka 2015, lazima wamshukuru sana JK, kwa sababu ni kupitia JK, uwezekano wa kuwezekanika kwa ukombozi huo, kunawezekanika!.
Wale mnaolalamika kuwa miongoni mwa makosa makubwa Watanzania, waliofanya, ni kumchagua JK kuwa rais wetu!, kiukweli, uchaguzi wa JK ndio kichecheo cha ukombozi wa pili wa Mtanzania, vinginevyo kama ni Lowassa ndie angekuwa rais, Tanzania isingekuwa hapa ilipo, na kusingalikuwepo hata hilo hitaji la ukombozi wa pili wa Mtanzania maana Tanzania ingeshakuwa peponi!.
Hivyo wale wote wenye kulitakia mema taifa hili, mshukuruni sana EL na JK, vingenevyo 2015, ingekuwa ni hadithi ile ile tulioizoea!.
Asanteni.
Pasco.