Mkuu WildCard, Nyerere alikuwa mjamaa wa ukweli, ugomvi wake na EL ni baada ya kusikia EL ndie landlord wa jengo la ubalozi wa Afrika Kusini pale Masaki, by then azimio la Zanzibar, halikuwepo, baada ya kuwepo kwa azimio la Zanzibar, kumemsafisha kabisa EL, kwa sasa sio kosa tena viongozi wa CCM kumiliki mali, ndio maana hata Chenge hajafanywa chochote licha ya kukutwa na vile vijisenti vyake kule UK na hata hizi kelele za mabilioni ya Uswisi, ni kelele tuu, nothing will be done to anyone!.
Enzi za CCM ya Nyerere, sifa kuu ya uongozi ilikuwa ni uwezo na uadilifu, enzi hizo, utajiri, ulikuwa unawapotezea sifa za uongozi!, baada ya Azimio la Zanzibar, sifa kuu ya uongozi wa CCM ya sasa ni pesa!. Haijalishi hizo fedha umezipataje, "the end justfies the means", the bottom line is money, Lowassa anayo sifa hii na hivyo ni very strong candidate ukiondoa afya tete!.