Edward Lowassa hukukidhi kiu ya wanawake!

I salute you.

Indeed you are a Great Thinker.

Thank you.

Queen Esther

Queen Esther mkuu ukizungumzia katiba hata JK aliikana bungeni na ndo ulikuwa msimamo wa ccm wote bt kama kwel wanawake wa TZ mnataka kujikomboa msisubl huruma ya maguful au lowassa ni kutaka katiba ya warioba irudi hapo ndo mtakuwa mmejikomboa kiukwel na ndo ajenda ya ukawa kurudsha ktba ya warioba kuliko kusubl maneno matam ya wanasiasa na kudanganywa na viti maalum na vyeo vya kupewa pambaneni ktba ya warioba irud kwan kule ndo kuna haki zenu zote leo ata aje cuf,chadema,ccm,act kutawala bt mtabaki wanawake kama strong institution na amtaitaji huruma ya chama au rais ili mambo yenu yaende vzr cdhan kama kuna m2 ambae atakuja kuwakata kiu wanawake kama unavyosema zaid ya mambo yenu haki zenu kuingizwa kwenye katiba leo ata akija kiongoz akasema kuanzia leo wanawake mtakuwa hv au vle au ntawapa hki au kile bt kama hakipo au havipo kwenye katiba avitatekelezeka na havitokuwa na nguvu wanawake msipiganie strong people piganien strong institution
 
Kweli wangonjwa hustahili faraja lakini kwa hawa wa ukawa do! Nisawa nakumraghai mgonjwa....ukawa poleni sana yote haya mliyatafuta na kuyakaribisha wenyewe poleni sana.
 
Ndio maana mnsishia kudanganywa na ndugu CCM tu kwani ndio mafundi wa kuongea zaidi ya masaa mawili mwishowe mnaendelea kuwa maskini na kuitwa malofa kwa miaka 50. Amkeni huko usingizini...
 
Yaani wewe hata kuusikiliza hukusikiliza,mkutano ulikuwa ni kwa mama Regina,wacha kujitoa akili

Wana masikio watasikia hawataelewa. wana macho hawaoni.

Magamba wamebaki kulia lia tu. Halafu maneno yenu hayo mkajidanganye vijiwe vya Lumumba, redio, magazeti.

Hamtauona ukweli mpaka mtakapodondoka chini na anguko litakuwa kubwa.
 
Yapo maneno yanazungumzwa kuhusiana na badhi ya Wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu wa 2015 kuwa ni MABUBU, HAWEZI KUJIELEZA NA HWAWEZI KUTUMIA MUDA MREFU KUZUNGUMZA NA WANANCHI
Sababu nyingi sana zinatolewa, kwamba kwa sababu ya afya zao kutokuwa thabiti, kwamba ni asili yao, kwamba ni watu wa vitendo siyo wazungumzaji, kwamba wana viburi kwa sababu ya jeuri ya pesa walionayo.
Naomba niongelee hili la viburi kutokana na jeuri ya pesa. Siyo wote wenye utajiri hususan wa pesa ni MABUBU, la hasha. Sitataja sina la mtu, ila nataka niwakumbushe kuwa Nchi yetu imejaliwa kuwa na Watu matajiri wa pesa/mali nyinginezo wengi tu wengine wakiwa wafanyabiashara, wengine watumishi wa Serikali n.k
Nataka pia tutambue wote hao historia za utajiri wao zinajulikana, mahusiano ya wao kwa wao yanajulikana. Wapo ambao utajiri wao hauna mashaka hata kidogo, lakini wapo ambao hata mtoto mdogo anajua utajiri wao ni wa mashaka kabisa(wana pesa haramu). Pesa zao zimetokana na ufisadi, rushwa, biashara haramu n.k.
Utafiti wa unaonesha kuwa Watu wote(narudia wote) ambao utajiri wao ni wa mashaka wanayo laana ya MUNGU, hawezi kabisa kujieleza na hata wakiongea mbele za watu, hawawezi kuwatazama wananchi machoni kwa kujiamini. Hii ni Laana ya Mungu kudhihirisha kuwa wana VIBURI vinavyotokana na matendo yao haramu.

Hii siyo kwa mtanzania tu, ni kwa Binadamu yeyote anayeyaishi maisha haya. Mali Haramu wanazomiliki zinachukua nafasi katika kufikiri ni kama mwanafunzi aliyezoea kuibia mtihani Darasani, hawezi kujibu hata swli rahisi bila ya kuwa na majibu pembeni au kuigilizia kwa mwenzake. Hiyo ni hulka na haina mjadala.

Sasa hili ni la mhimu sana:
Ukikubali kurubuniwa na watu wa aina hii, dhambi hiyo inaendelea kwako, huwezi tena kujitambua . Kwa nje nje unaona kama UMEPATA lakini kwa ndani unabaki Dhamira inakusuta, unakuwa kama umelaaniwa vile

Ni hayo tu kwa leo, tuchukue tahadhari na hawa Mabubu hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Hatudanganyiki!CCM weka kando, umeshindwa kuwahudumia watanzania miaka 54, ndo anaendelea kutuhadaa na ilani zenu za wongo! Rais lazima atoke UKAWA!
 
Una maana gani unaposema anacheza na akili zetu. Mbona hiyo ni kazi ya Wasanii. Je unamaanisha mzee wetu ni msanii??

Queen Esther

Jamani sikuwa na mpango wa kukujibu ila naona nikupe angalizo, Lowasa si wa hivyo yule anacheza na akili za CCM kuliko unavyofikiri. Mipango yake haikamatiki kwa uelewa mdogo hata kidogo, anatulia na kutafakari karata zake azichezeje. Kama unataka kuamini ninachokisema subiri hiyo jumamosi alafu uje uniambie mwenyewe nini atasema. Narudia tena Lowasa sio kama mnavyotaka awe. Anawasomeni bila kujielewa
 
Toka enzi za akiwa shule si muongeaji ila ni mtu mwenye maono na mtendaji makini. Na kwa sasa tunahitaji mtu wa namna hii
 
Kuna watu walitaka waambiwe wanapewa milioni hamsini kila kikundi cha vikoba!!!
Matatizo ya WANAWAKE yatamalizwa na WANAWAKE wenyewe!! Lowasa yupo sahihi kabisa, mtafutieni kura halafu mtakuja kukaa chini na kutoa mapendekezo yao nini kifanyike kutatua changamoto hizo!!!
 
Tatizo bado ukawa hawajazidua kampeni!maana magufuli anatumia mikakati ya Lowassa,sasa utafurahi jumamosi paleeee,waliposhindwa magamba kujaza watu
 
Unamaanisha mzee anapiga USANIII????

Fafanua tafadhali sijakuelewa.

Queen Esther

Huyu Lowassa ningeshndana naye urais lazma angenishnda,,,jamaa hatabiriki,,style ya kuanzia kampeni kwenye daladala,leo Katoa kaz ya kutafutiwa kura badala ya kutoa hotuba na bado watu wanamkubali,,,,ajabu magufuli anatumia nguvu nyingi na fitna juu lakini hali ni ngumu,,,Duuh!
 
Yaani leo nimeamini kwamba Lowasa hana uwezo wa kujena hoja. Leo kaishia kusema kuwa anadeka kwa akina mama waliohudhuria mkutano wa BAWACHA

Subiria octoba ndo utajua tulimuelewa ama vp. Na ivi wamama wa ukawa sio wakubebwa kwenye mafuso kama wale wa kwenu....hahahahaaa.

Alafu we mzee njaa zitakua. Jifunze kutumia akili basi
 
Hebu mtafute mama au dada angalau mmoja halafu muulize Mhe. Lowasa amesemaje?????

Au agenda ya kongamano ilikuwa ni nini na amejifunza au anakumbuka nini kwenye hilo kongamano halafu urudi humu kutetea.

Queen Esther

mkuu mbona una haraka kama mkojo wa asubuhi ?, kwanza ya Ukawa hayakuhusu fuatilia Pombe wenu anavyozunguka na maneno ya kukaririshwa. Ya Ukawa waachie wenyewe watajua wenyewe nini wafanye na kwa wakati gani. Naona mmechoshwa kusikiliza sera zilezile za ccm mpaka mnapata hamu kusikiliza sera mpya za ukawa
 
Mbona jamani Mzee alisema mwanzoni kabisa mwa salamu zake?alisema kuwa leo hajakusudia kutoa hotuba...bali anawatuma kina mama wakamuombee kura!!Sisi wengine hatutaki maneno zingiiiiiii za kina Magufuli...hayo hayo ya Eddo yanatosha,maana kama kuongea tu,CCM wametuambia sana sana na hakuna walichafanya
 
Mipasho na matusi ya Mhe. Mbatia aliyoitoa kwa baba Yake Leo hukuiona??

Queen Esther

Si ni bora Lowassa kuliko yale Matusi na Mipasho iliyotolewa na Wazee wa CCM mbele ya umati wa watu? Mtawakoma watanzania ifikapo October 25.
 
Labda nikuulize wewe.

Mimi ni Queen Esther. Uwanja wa kina mama ndio haswa unaonihusu. Nitafungua Uzi mwingine wa Madame Samia wakati ukifika. Kwa hapa zingatia kichwa cha habari tafadhali. Usitoke nje ya mada.

Queen Esther
Note alichoanza kusema baada ya kushukuru nk..."Mmi leo sikusudii kutoa hotuba"......na akawakaribisha woote na kuwaomba wawahimize wengine kuja jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni hapo Jumamosi...then he went on kuwapa hiyo kazi ya kumtafutia kura nk!...upo hapo?
 
Back
Top Bottom