Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki


Uzinifu huanzia ufichoni siku zinavyosonga mbele hudhani ni halali yao! Huja kujua sio halali yao watakapokutwa sebuleni na mama mwenye nyumba!
 
Hizi ni kamba wazazi mtu mzima el huwa anatwanga siyo mtu wa sms mlio arusha wekeni issue sawa tujue kama jao wazazi wako lupango
 
Lowassa mpaka leo hajui mbinu za kupanga madili? He should ve called using private number in secured line. Ye si mtu mkubwa banaa! Inakuwaje anacheza kitoto?
 
Kweli Jakaya kaamua kula hiki kichwa jumla.
Lowassa anatakiwa kutafutwa popote alipo na yeye awekwe ndani
OTIS

Anambana kila kona. Mara rushwa, mara nataka raisi kijana. . .haya tusubiri
 

Hii habari inaoneka umeitoa kwenye gazeti pendwa la udaku KIU.
Hivi Edward Lowassa anaweza kuangaika kuandika sms? Hahahahaha Chadema bana!
 
Mkuu Ngongo, kiukweli Takukuru wanajifurahisha tuu!, hakuna kesi yoyote serious ya rushwa!. Kama uchaguzi uliopita Takukuru waliwakamata watu na rushwa red handed na hakuna kesi yoyote, ndio itakuwa sms za rushwa!.

Machalii wa Arusha wanapenda kash kash za Godbless Lema type. Kushikiliwa polisi kwa wana AR ni ushujaa hivyo sasa kitendo cha kuwashikilia mahabusu hao wafuasi wa Sioi, hivyo ndio kampeni funga kazi kwa Sioi, amemaliza kila kitu!.

Kabla ya purukushani hii, CCM wangeweza kumtosa Sioi, lakini hii promo ya Takukuru sasa ndio imemrudisha Sioi at the top, hivyo sasa Arumeru ngoma bado ni mbichi, Sioi ndiye mgombea wa CCM and to my honest opinion, Arumeru is done, tuanze kupima upepo wa nguvu ya EL kuelekea 2015!.
 

Nduguyetu joseph Peter, inaonekana wewe umebobea upotoshaji na umebobea Kabisa. Mimi naomba ni toe facts Kama zilivyo na nipo tayari kuwa challenged na mtu yoyote. Kwa sasa hivi nipo nje ya ukumbi wa mkutano wa kupigia kura na wajumbe wameshaingia wote wakiwa wamependeza na mashati yao ya kijani na njano na nimefurahia Sana kumuona kamanda wangu Elirehema Kaaya akiingia ukumbini kwa nyuso ya furaha kabisa hata baada ya kupigwa msukomsuko na maafisa wa takukuru.

1. Elirehema Kaaya alikwenda Dsm kushirki vikao vya secretariat na kamati kuu akiongozana na ndugu Kisali sarakikya ambaye name anapigiwa kura leo, walikaa wote Dsm na baada ya kikao wakafanya safari ya kurudi wote arusha. Ni mjumbe halali wa mkutano wa leo na Jana wakati amekamatwa alikuwa amekaa kwenye grocery na wapiganaji wake wakibadilishana mawazo, hakukuwa na mambo yoyote ya pesa. Elirehema anajimudu kiuchumi na ninategemea ana uwezo Kabisa aw kulipia nauli zake, lakini Kama kuna wa kumtuhumu kumsaidia usafiri labda iwe sarakikya, lakini bado siamini hivyo.

2. Ezekiel Mollel ni katibu wa vijana wa uvccm monduli na ni mkazi na mwenyeji wa wilaya ya arumeru, uvccm mkoa kwa kupitia katibu wake wa mkoa Mpokwa wanashiriki marudio haya ya kura Kama jumuiya zingine zote za mkoa kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu tar 1 april. Huyu alishikwa akiwa peke yake anapanda pikipiki na inasemekana maafisa walikuwa na kijani anaitwa ammo akiwaonyesha watu wa kukamata, kwenye kundi hilo hilo walikuwepo makatibu wa wilaya zote za mkoa na katibu mwenyewe wa mkoa, napa unaona u-monduli ulitumika ili kwa Mara nyingine tena tuliingize jina la lowassa kwenye midahalo ya CCM. Mawasiliano yake na simu siwezi kuwa na uhakika, ila ukiniambia alikuwa anawasiliana na lowassa, hiyo ni PUMBA.

Tukirudi kwenye mchakato wenyewe wa kura za leo, inasikitisha na inatia aibu kubwa sana, ningekuwa mimi ndiyo Huyo kijana anaitwa sioi ningejitoa. Jana Mkuu Wa wilaya aliwaita madiwani wote wa arumeru mashariki na kuwaambia msimamo wa serikali ni ssarakikya, na ikatokea vurugu kubwa na polisi wakaweka madiwani wengine chini ya ulinzi. Tujiulize kwanza kwanini huu uchaguzi unarudiwa Leo? Hamna Majibu ya kuridhisha, na ukijiuliza tena ni watu gain walipinga matokeo ya sioi kwenye vikao? Unapata majibu ni wateule wote wa serikali na chama, sishangai kusikia haya ya takukuru leo ila inasikitisha Sana. Demokrasia ya Kweli iko wapi? Ningefikiri kazi ingekuwa kusimamia uchaguzi wa kweli na haki, na wananchi wapate fursa ya kuamua wawakilishi wao.

Namalizia,baada ya kamati kuu kuamua uchaguzi kurudiwa, wazee wawili wa kamati kuu walimfuata Sioi kumshauri ajitoe kwasababu sababu za yeye kukatwa jina hata Kama akishindwa zimeshaandaliwa na Sioi akawajibu kwamba sivyo ambavyo nimelelewa na wazazi wangu, nilifanya sala Kuomba baraka za marehemu baba, ningependa huko aliko alone kijana wake sikumuangusha na nilismamia ninachokiamini mpaka mwisho whether win or lose.

Tusubiri tuone cinema hivi inaishia wapi.
 
bye bye lowasa,
mzimu wa mwakyembe umeanza kazi
akingali hai bado.
 
Hawa magamba kwa strategy za kizamani kweli hawajambo... Yani sasa wanataka kuwaaminisha wananchi kwamba wapo vitani na rushwa ni adui yao, lakini ukweli ni kwamba nani kati yao anayeweza kumnyooshea mwenziwe kidole? kinachoendelea hapo ni mbinu tu ya kuwakoga wabongo na hasa wana Arumeru Mashariki ili waonekane wanatuletea mtu safi.

Wana Arumeru Mashariki zindukeni achaneni na sarakasi za magamba kamataneni na wanamageuzi ili mkombolewe kifikra na kiuongozi.
 




Haya bwana kwa mara nyingine tunaletewa maigizo and then we succumb in the fictious drama na kuachana na mambo nyeti. TAKUKURU have for so many days been toothless bull dogs that cannor bark. Sasa kwa kuwakamata hao watu waliotajwa tena kwa kutumia txts za simu ndio kutufanya sisi tuwapongeze? Hapana nafikiri TAKUKURU wana wajibu mkubwa kuweka efforts za kuwakamata wala rushwa kubwa kubwa ambao vitendo vyao vimeliangamiza taifa hili katika lindi la umaskini. Hatujawasikia wakitumia nguvu hiyo kukamata waliokwapua pesa toka BOT maarufu kama EPA, hajakamata list of shame ambayo haijawahi kukanushwa, watuhumiwa wa MEREMETA, Richmond, waliotorosha wanyama wetu kwenda Qartar watuhumiwa wa Kiwira na wote waliosainisha mikataba tata ya madini na kutuacha kama taifa kuambulia asilimia 3 kama mrahaba na mengine mengi yanayofanana na hayo. Sasa wanatumia reveneu za serikali zitokanazo na wananchi kukimbizana na wanaotoa pesa ya soda. Shame on you TAKUKURU. Maofsa wanaokimbiza na vijitu vidogovidogo kwa gharama kubwa ingefaa washtakiwe wao. ANy effort should pay off itself for public benefit.

Halafu wanasiasa waangalie na wajue kuwa kumchafua EL sio kwamba ndio mtasafishika. La hasha. Watanzania wa leo sio wa jana. Hivi sasa awareness yetu ni kubwa. Makosa ya EL hayawezi kuwasafisha kwa madudu yaliyoelezwa hapo juu. It's a matter of time. Saa ya ukombozi yaja na nyie mtajibu ya kwenu. EL anafanyiwa character assassination na kama mnafikiri anayo makosa mbona hamjampeleka mahakamani? Uko si ndio haki inapopatikana? Enough is enough with EL tunataka kujua walioifilisi na ambao wanaendelea kuifilisi watakamatwa lini?
 
Mimi nina maoni tofauti hii yote ni danganya toto ya takukuru ili muamini kweli wamefanya kwa nia njema kumbe kuna zaidi ya hayo. wanatumia tu hii iwe sababu kwamba wanakamata rushwa kumbe mpango mzima wa kugawa pesa unakuja baadaye. Nimeamini hivyo kutokana na CCM walivyo na njia nyingi za kutudanganya na wanajua kabisa watanzania huwa hatufikirii zaidi ya tukio. Ni maoni yangu tu
 
KK

Naona humjui Lowassa na RA kwenye nchi hii.
 
Anambana kila kona. Mara rushwa, mara nataka raisi kijana. . .haya tusubiri

Sasa makucha yameanza kunjuliwa.
Upenyo kama huu sio wa kuuachia ili apotezwe kabisa.
OTIS
 
KGBtz,
Aliyenisikitisha mimi ni Nape. Alitutangazia maamuzi ya ajabu ya kikao cha CC ya CCM huku akijua fika kuwa kanuni hiyo imekiukwa mara nyingi tu kwenye teuzi za ndani ya CCM. CCM haohao kwa kutumia wingi wa WABUNGE wao walikiondoa kipengele kinachofanana na kanuni hii ya mgombea kufikisha zaidi ya nusu ya kura ili atangazwe mshindi kwenye uchaguzi wa Rais wa JMT.
 
Wajameni tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kama issue ni rushwa, kwa CCM, its order of the day!. CCM kwa upande wa rushwa imeoza juu mpaka chini na ndani mpaka kwenye kiini, hivyo hayo yanayoendelea ni harufu tuu ya uvundo wa rushwa, rushwa yenyewe halisi, CCM ndio nyumbani kwake!.

Naendelea kusimama na EL ateuliwe kuwa mgombea wa CCM, rais atoke Kaskazini tupate ukombozi wa kweli wa Mtanzania!.

Mnaoamini kila supporter wa EL amelipwa, naomba niwasemee kabisa ili msijisumbue kusema, "mimi nimelipwa" na kwa vile takukuru pia wanashinda himu, njooni pia mnikamate tena sio na sms, but hard cash, lots of them!.

Invisible, Takukuru wakiniulizia, just disclose info and expose it!
 
Kadri siku zinavyo sogea ndivyo CCM inazidi kuwa chama kichovu zaidi. Hizi sarakasi tutazishuhudia vizuri kampeni zitakapoanza. Niko na wasiwasi vituo hewa tayari vimeisha tayarishwa ili CCM ishinde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…