Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

Kaaya unahangaika nini, ulipata kura zako 205, ungerudi zako Mwanza kuendelea na kazi zako, ona sasa na unadhifu wako wote umeishia lumande.
Mbona Lowana na huyo freddy hawaitwa na takukuru ili wahojiwe, kesi gani hii ya upande mmoja?
 
Mh! Sidhani. Hauna "mandate" ya kutusemea WATANZANIA woote. Halafu, AruMeru wana vigezo vyao kwenye mambo haya ya kuchaguana. Chama gani mgombea anatoka sio mojawapo ya vigezo hivo.
Na sidhani vile vile kama una Mandate ya kuwapangia vigenzo vya aina ya mgombea wanayemhitaji watu wa Arumeru.
 
Nilishasema, hakuna uchaguzi unaowashirikisha wanaCCM wasihonge. Na huu ni uchaguzi wa wao kwa wao. Vipi ule wa kupambana na wapinzani!?
 
Tupatieni kidogo WASIFU wa Joshua Nassari.
Waulize wanachama wa CHADEMA waliompitisha kwa kura nyingi ndio wanaojuwa wasifu wake, au kama tume ya Uchaguzi ina data base nzuri basi wasifu wake uko pale.
 
Bila shaka unamzungumzia Papa King mmiliki wa Tripple A,Mwarusha mjinga huyu ndiyo mweka hazina na mchangishaji mkuu wa fedha za rushwaa hasa wakati wa uchaguzi.Papa King alimponza Dr Batilda na sera za ukabila eti Arusha ni ya waArusha.(umenikumbuka Ditopile kipindi kile Temeke Dr Mrema aliwasumbua CCM wakaja na mipasho ya alo alooo mara Mrema hajuia kula chapati mwisho wa siku mgombea wa CCM akaangukia pua)

Na wale masai wa Tripple A hawapo kwenye hiyo grupu?
 

Mkuu KGBtz, na wadau wengine,

Mimi nadhani Joseph Peter si mtoposhaji kwa bandiko lake aliloliweka hapa jukwaani, kwani kwa kiasi kikubwa taarifa iliyo kwenye bandiko lake imethibitishwa na Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU katika taarifa ya habari ya saa 7 mchana huu.

Source: TBC1 Habari [Dira ya Mchana]
 
Tatizo lililopo ndani ya makundi ya CCM; Ni sawa na wachimbaji wawili ndani ya shimo la choo wanachafuana ndani kwa ndani baada ya mmoja kumchafua mwenzake anafikiri yeye akitoka nje ataonekana msafi.

Badala ya kundi moja kujisafisha ili adui wao aonekane mchafu, wanamchafua adui ili wao waonekane wasafi bila kwanza wao kujisafisha hivyo kuendelea kuonekana wachafu nje ya CCM.
 

Undugu wenu utawaponzeni enyi Lowassa senior na Junior!
Mkwe na shemeji...mnataka taifa zima mlitawale? Huyo Sioi si ni mkwe wenu ..inatosha.
Waachieni wengine nao washiriki katika uongozi.
Diversity ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
 
Kama kweli taarifa hizi zina mashiko then nakubali kwamba JK is the silent killer. EL out of the game.
 

inatia hasira sana mkuu matola, mi nadhani mashabiki wa Lowasa wanapewa zaidi ya pesa, pengine jamaa anawapa vitamu zaidi ya tunavyodhani, haiwezekani ukawa na roho chuma kiasi hiki
 
Pamoja JF kujulikana kama Home of Great Thinkers lakini nasikitika sana inapotumiwa kama sehemu ya propaganda
Sitaki kusema mengi lakini sijona hata mtu mmoja kujaribu kudadisi hii habari inaukweli kiasi gani, kila mtu anrukia kwenye hitimisho tu
 
Hii ni kama kawaida Chama cha Wasanii na afanyaye usanii zaidi ndiye anayeonekana bora zaidi.Msanii bora kati ya wasanii na Chairman Msanii then sera zote ni usanii
 
sasa kama watu wanahonga hivyo kwaajili ya kuupata ubunge inakuwaje Anna makinda na Makinda yake wanasema ubunge ni umaskini?
Wana Arumeru nawapa uashauri wa bure mkihongwa chukueni wakati wa kuchagua chagua ambaye hajatoa rushwa.
 
Afu uyo katibu wa uvccm monduli ezekiel mollel ni darasa la saba mkazi wa ngaramtoni,chadema 2songe mbele wacha magamba wajizike.mamvi ameisha
 
Ezekiel huyo katibu wa uvccm jimboni kwa mamvi ni darasa la saba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…