Edward Lowassa afanya Propaganda kwenye media eti kashinda 100%

Chadema laini laini Arusha yaachia serikali za.mitaa kwa dume lake CCM.
Matokeo ni kwamba:
CCM 78-CHADEMU 75
 
Kuna wa/mpambe wake hapa jukwaani nimemchana bosi wao wameshia kutukana na wala hakuna aliyejenga hoja. Nimewauliza mbunge sio mfadhili, hebu watuambie inakuwaje huyo Lowassa anaweza kwenda misikitin/ makanisani akaweza kutoa hotuba ambayo haulizwi swali lolote lakini hawezi kuchangia chochote huku bungeni ambako ndio majukumu yake yalipo. Kama anaweza kuhutubia kanisani/msikitini kwanini asiwe sheikh au mchungaji anataka kuwa rais. Ndugu ungesikia majibu ya watu anaowalipa kumtetea hapa jukwaani mbona ungechoka. Wameishia kutukana na kukashifu.

Sikuishia hapo nikawaomba wataje mambo matano ya uhakika kwanini tumpe urais hakuna aliyerudi mpaka sasa!! Toka nimemuona alivyopoteza madaraka kwa sakata la richmond nilimsikia siku moja tu akichangia bungeni eti nchi ichukue maamuzi magumu, eti wakatokea wabunge wasiojitambua wakimshangilia rais rais!! Nikauliza mbona juzi tumeshuhudia sakata la escrow hadharani hatukumuona akichangia lolote tuliishia kuwaona akina Lisu, Zitto, Mnyika, Mdee, Simbachawene na hata huyo Chenge. Yeye msimamo wake ulikuwa upi ni pesa za umma au za IPTL. Sasa najiuliza ubora wake uko kwenye nini. Au yeye ni tajiri hivyo tumpe urais kwakuwa wanamlamba miguu wamesema.

Nasema tusipoangalia tutampa nchi hii mmoja wa viongozi wa mtandao wa kiongozi aliyeko juuambaye kaifikisha nchi kwenye kuweza kuingia mikataba zaidi ya kumi na sita kwa mpigo bila wananchi au bunge basi kujua nini kipo ndani bali genge lake tu. Na kwa bahati mbaya sana tunapewa sifa zilezile za kijinga kwamba ni mchapa kazi lakini uchapa kazi wake haufafanuliwi bali watu wanapewa pesa wanakuja kusema ni mchapa kazi. Sifa hizihizi ndio tuliambiwa tuchague rais kijana ambaye picha yake itapendeza kwenye noti. Kweli watanzania tuko tayari tena kutoa uongozi kwa kiongozi ambaye sifa zake ni za uchochoroni tena kwa nguvu ya pesa?

Mkuu yani huyo bw. EL sitaki hata kumsikia, huyu jamaa ana agenda ya siri na hii nchi. Yuko tayari kufanya chochote ili apate kutimiza ndoto zake ambazo wajinga wengi wanamshabikia bila kujua ni nini malengo yake huyu bwana.
 
kutoka kwa mwandishi wa lowassa abubakary liongo ametuma taarifa kwa vyombo vya habari kuwa monduli ccm imeshinda kwa aslimia 100 na anataka dunia iamini hivyo ,eti monduli ni kama kilindi, na hilo ni jambo la uongo wa dhahiri kwani anajua wazi kuwa maeneo yafuatayo ccm imeshindwa ;

1. Kitongoji cha kambi ya mkaa ccm 13 na chadema 27

2. Loswira kitongoji , ccm 34 na chadema 56 tena hapa alishinda mlemavu .

3. Kijiji cha mgombani chadema imeshinda vitongoji vinne ...

4. Kijiji cha nanja ccm imeshindwa .....


Liongo njoo upinge ukweli huu ndipo wahahriri watumie story yako kesho ........


kama ccm washaanza kufurahia wenzao wakishindwa basi tutegemee mwakanj ccm wengi watapigia kura chadema za urais kwakuwa wameshindwa chimwaga
 
na iv ndo itakavyo kua kwenye matokeo ya jumla utashanga ccm imeshinda kwa 97% kesha wana wa yesu UKAWA watabak na malalamiko yasio na tija mana sis tumezoea kushinda mtandaoni

Sasa watakuwa wanamdanganya nani wakati wananchi wanajua kila kitu.
 
Chadema laini laini Arusha yaachia serikali za.mitaa kwa dume lake CCM.
Matokeo ni kwamba:
CCM 78-CHADEMU 75

ETI CHADEMA YAACHIA...wewe kama mwana ccm kama unaridhishwa na hayo matokeo UNASTAHILI KUFUTWA UANACHAMA.
 
Wenye upeo mpana kwasasa hatuzungumzii haya matokeo ya mtaa momoja mmoja yakiwa tayari yote tukutane hapa hapa jf.
Maswali muhimu kuliko yote... Je,CCM ni winner au ni Loser...??
CCM imeshuka au imepanda...?
Je, Graph ya Kupanda au Kushuka ni Gentle au Steep..?

Nape Nnauye alisema UKAWA watasambaratika,je ni kweli wamesambaratika au wamekua wamoja..?
Alisema pia kua Tusubiri mafuriko ya Ushindi..Je,kwa matokeo haya ndio mafuriko au Chemchem...?

Jibu,kwanza hayo maswali ndo tujue kama tunazungumza na mtu,isije kuwa ni Robbot...linasubiri liwe Monitored/ controlled...
 
Kutoka kwa mwandishi wa Lowassa Abubakary Liongo ametuma taarifa kwa vyombo vya habari kuwa Monduli CCM imeshinda kwa aslimia 100 na anataka dunia iamini hivyo ,eti Monduli ni kama Kilindi, na hilo ni jambo la uongo wa dhahiri kwani anajua wazi kuwa maeneo yafuatayo CCM imeshindwa ;

1. Kitongoji cha Kambi ya Mkaa CCM 13 na CHADEMA 27

2. Loswira Kitongoji , CCM 34 na CHADEMA 56 tena hapa alishinda mlemAvu .

3. Kijiji cha Mgombani CHADEMA imeshinda Vitongoji vinne ...

4. Kijiji cha NANJA CCM IMeshindwa .....


liongo njoo upinge ukweli huu ndipo wahahriri watumie story yako kesho ........
mzeee haya mapinduzi hayaepukiki, hata watu wa nyumbani kwa Lowasa wamemtema, kwa Magufuli nako wamemtosa, na bado. Mwambieni Lowasa kuwa kuzuia UKAWA ni kama kuzuia maji ya mto kwa mkono.
 
Ukawa imekuwa ukiwa.

Ukhut,
twende mbele turudi nyuma kiukweli uchaguzi huu ni challange kwa ccm. Hamkutegemea upinzani wa perform hivi walivyoperform.
Sikufichi wananchi wanamalalamiko mengi juu ya wanaccm kujifanya Tanzania ni yao wao na watakacho wananchi hakina nafasi.
Msipo rekebisha mambo fasta ile tahadhar iliyotolewa na PAC kwa wanaccm juu ya muwekezaji wa escrow mjiandae nayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom