Edward Lowassa afanya Propaganda kwenye media eti kashinda 100%

Nashukuru kwa ushauri wako,nafahamu sana kuwa kuna manabii wa uongo wanaotumia jina Na Mungu.
ila kwa kukusaidia tu ni kwamba Huduma ya Mungu hudumu na hudhihirika kwa matendo ya kimungu

Asante kwa kunielimisha pia,ila IMANI ni kitu kigumu sana.
 
Ahsante sana ndugu Tindo...
Tunaelewana kwa hoja mimi na wewe kwa kuwa tuna nia moja ambayo inafanana nayo ni kuiona hii nchi ikipiga hatua kwa namna moja au nyingine i.e Huduma bora za afya, Ajira, maji, Elimu n.k

Narudi kwenye mada, suala la nasari nimejaribu kulifuatilia kwa kina na sikuona mahali ambapo EL amehusika na kama Nasari angeliona hilo yeye anahaki ya kumpeleka kwenye chomba husika ambacho ni polisi. Kama nilivyosema mwanzoni EL ni msikivu sana mashahidi wa hili ni wakurugenzi wa hizi almashauri zetu kipindi yeye ni waziri mkuu kwa hiyo yeye ni rahisi kufanya kazi na wabunge wa upinzani.
Mpaka sasa kwa uelewa wangu EL ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi. Lakini kama nilivyosema mwanzoni CCM inauozo wake waouvu wake lakini pia inawatakatifu wake pia hii ni sawa na wewe kua na watoto sita alafu wanne wakawa wezi alafu wawili wakawa safi hauwezi wahukumu wote kwa hiyo yeye kutumia CCM kama platform ya kuingia ikulu sioni kosa kwa kweli. Kingine mimi na wewe tumeona mapungufu ya hii katiba pendekezi na tuwajuzevwasioielewa kwende kuipinga hapo Aprill mwakani.

Naomba nieleweke mimi kama Carina simtetei kwa vile namjua binafsi bali kwa fikra zangu naona kama ni mtu anayefaa kuliongoza taifa hili. Kikubwa cha mwisho bwana Tindo tujue kila binadamu anamapungufu yake na yeye kama binadamu anayo pia lakini overrall hauwezi fananisha na watangaza nia wengine wa CCM. Ni mtazamo tu

Nashuru bwana carina kwa ushirikiano wako, hebu tufikie mahali tukubali tu, mtu akishalitumikia taifa kwa muda fulani ifike mahali aachie na wengine kwa nia njema kabisa kwani sasa tunaanza kuwa na wasiwasi na yeye, kwanini alazimishe kuwa Rais wakati kuna vijana wengi tu tena wenye uwezo? Ama na yeye ndio walewale waliolewa methali za upendeleo kwamba vijana ni taifa la kesho? Yeye EL kama EL walipaswa kuweka mazingara mazuri ya kupokezana uongozi baada ya muda fulani kwa kuweka mfumo sahihi wa kuachiana madaraka na sio kulazimisha kukaa wao tu madarakani hata kama wakati umewatupa mkono.

Kuhusu suala na Nassari unasema vyombo vya dola, ukweli ambao ni mchungu ni hivi, vyombo vyetu vya dola hapa vilipofikia unadhani vinatenda haki sawa katika makundi ya jamii haswa wapinzani? Sitaki kukulazimisha kwenye hili bali wewe mwenyewe na dhamira yako kweli unaona wapinzani na ccm wanahaki sawa kwenye vyombo vya maamuzi? Hapa tuwe wakweli tu. Sitaki uumnyime kura EL kwani tayari una imani naye na ni haki yako kumpa kura mtu unayemuamini. Lakini mwambie haya mambo ya yeye kukaa kimya kwenye mambo ya kitaifa hasa yenye maslahi kwa taifa na wakati ana mahali muafaka pa kusemea kama bungeni tena kuishauri na kuisimamia serekali, akangoje kusemea sehemu ya wachungaji na masheikh atakua haitendei haki nafsi yake wala ya wananchi wake. Nasema tena hongera hongera sana ndugu yangu kwa michango yako yenye tija.
 
Ndugu Tindo mimi ni mdada na si bwana kama ulivyosema...
Kiukweli mpaka sasa naona muelekeo wa mada unapoenda naona unanivuta upande wako ambapo mpaka sasa sijajua niendapo haujakuwa muwazi kama mimi..
Taja kijana ambaye unahisi anafaa na sifa zake 5 kama nilivyoeleza mwanzo
 
Naombe niombe samahani kwani wanawake huwa mnajiweka nyuma sana japo mnafanyiwa upendeleo kiasi cha mimi kudhani kila aliye humu ni mwanaume. Samahani kwa hilo. Kimsingi sina kijana maalum lakini nadhani sasa ni wakati wa vijana, hao wapo wengi kuanzia wa ccm mpaka wa upinzani. Itategemea vijana wataaminiwa vipi na vyama vyao na jinsi watakavyomwaga sera zao. Lakini ili tupate mabadiliko chanya sasa ni wakati wa vijana. Hao akina EL watumike kama washauri tu na sio urais tena. Huu ni mtazamo wangu ambao sikufungi nao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom