Kuna wa/mpambe wake hapa jukwaani nimemchana bosi wao wameshia kutukana na wala hakuna aliyejenga hoja. Nimewauliza mbunge sio mfadhili, hebu watuambie inakuwaje huyo Lowassa anaweza kwenda misikitin/ makanisani akaweza kutoa hotuba ambayo haulizwi swali lolote lakini hawezi kuchangia chochote huku bungeni ambako ndio majukumu yake yalipo. Kama anaweza kuhutubia kanisani/msikitini kwanini asiwe sheikh au mchungaji anataka kuwa rais. Ndugu ungesikia majibu ya watu anaowalipa kumtetea hapa jukwaani mbona ungechoka. Wameishia kutukana na kukashifu.
Sikuishia hapo nikawaomba wataje mambo matano ya uhakika kwanini tumpe urais hakuna aliyerudi mpaka sasa!! Toka nimemuona alivyopoteza madaraka kwa sakata la richmond nilimsikia siku moja tu akichangia bungeni eti nchi ichukue maamuzi magumu, eti wakatokea wabunge wasiojitambua wakimshangilia rais rais!! Nikauliza mbona juzi tumeshuhudia sakata la escrow hadharani hatukumuona akichangia lolote tuliishia kuwaona akina Lisu, Zitto, Mnyika, Mdee, Simbachawene na hata huyo Chenge. Yeye msimamo wake ulikuwa upi ni pesa za umma au za IPTL. Sasa najiuliza ubora wake uko kwenye nini. Au yeye ni tajiri hivyo tumpe urais kwakuwa wanamlamba miguu wamesema.
Nasema tusipoangalia tutampa nchi hii mmoja wa viongozi wa mtandao wa kiongozi aliyeko juuambaye kaifikisha nchi kwenye kuweza kuingia mikataba zaidi ya kumi na sita kwa mpigo bila wananchi au bunge basi kujua nini kipo ndani bali genge lake tu. Na kwa bahati mbaya sana tunapewa sifa zilezile za kijinga kwamba ni mchapa kazi lakini uchapa kazi wake haufafanuliwi bali watu wanapewa pesa wanakuja kusema ni mchapa kazi. Sifa hizihizi ndio tuliambiwa tuchague rais kijana ambaye picha yake itapendeza kwenye noti. Kweli watanzania tuko tayari tena kutoa uongozi kwa kiongozi ambaye sifa zake ni za uchochoroni tena kwa nguvu ya pesa?