Dutch Disease: Ugonjwa unatokea kwenye nchi ambayo imebarikiwa na rasilimali

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
DUTCH DISEASE

Huu ugonjwa ni effect ya resource curse.

Dutch disease ni ugonjwa ambao unatokea kwenye nchi ambayo imebarikiwa na rasilimali kama mafuta, gesi, madini nk

Huu ugonjwa unatokea kama ifuatavyo

Nchi ikigundua imebarikiwa na rasilimali flani, nchi ambazo hazijabarikiwa na hiko kitu huja kwa kasi kujitahidi kunufaika na hio rasilimali.

Nchi za kigeni zikija kwenye nchi iliyobarikiwa zinafanya thamani ya fedha ya io nchi kupanda.

Thamani ya fedha ikipanda, hufanya kuagiza vitu kutoka nje ya nchi kuwa bei nafuu kuliko kununua vitu vinavyotengenezwa nchini.

Sasa watu wa nchi iliyobarikiwa wakianza kuagiza kuzidi kununua vitu vya nchini kwao basi hufanya viwanda vya nchini kwao kushindwa kwenye ushindani wa bei na bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ya nchi, mwishowe viwanda hivyo hufa.

Viwanda vya nchini vikifa basi hufanya wananchi kukosa kazi na mwishowe kukosa maendeleo katika nchi husika.

Mfano:
Kama South Africa ilivyogundua ina madini, watu wengi waliacha shughuli zao na kukimbilia kuchimba dhahabu wakiamini ndio kuna pesa zaidi. Kwaio kilichotokea ni kwamba sekta nyengine za biashara zikafeli kwasababu watu wote wamekimbilia kwenye sekta moja ya madini. Kwaio hata mishahara ya sekta nyengine hupanda na sekta nyengine zinashindwa kuwalipa na mwishowe running cost zinakuwa kubwa na zile sekta zinakufa.

Mfano 2:
Ujio wa Network marketing, baada ya watu kuona faida ambazo waliotangulia kujiunga na network marketing basi watu wengi kuacha shughuli zao na kukimbilia kujiunga na network marketing.

Hivyo kufanya bidhaa nyengine kukosa soko, kufanya sekta nyengine kukosa wafanya kazi pia wengine huacha mpaka shule kukimbilia kujiunga na network marketing.

Kinachotokea sasa ni wauzaji wa bidhaa hizo za network marketing kuwa wengi kuzidi soko, na kufanya sekta nyengine za biashara kufeli.

JINSI YA KUEPUKA DUTCH DISEASE
  • Nchi kuweka vikwazo kama kodi kwenye imported goods ili kulinda viwanda vya ndani.
  • Kufungua ajira kwenye sekta nyengine za biashara
  • Kutoa elimu ya umuhimu wa seka nyengine za biashara
  • Sovereign wealth fund management (hili darasa la siku nyengine)
  • Kujifunza kuwa sekta zote za biashara ni muhimu na zinategemeana, hatuwezi wote kufanya kitu kimoja.

Karibuni kutoa comment na mifano mengine

#southafrica #resourcecurse #dutchdisease #oilandgas #naturalresources

#management
#comment

dutch disease.jpg
 
Waafrika wengi ni wajinga ,malofa ,wabinafsi na wapunbavu hivyo waache visingizio na roho zao mbaya.

Ajira Gani kama watoto wanaachwa wafuge ngombe pamoja na pundamilia badala ya kwenda shule ili waweze kuendesha viwanda na uchumi wa nchi.

Karne ya 21 Bado watu wanajadili suala la kutoka porini kuishi na wanyama ili watoto waende shule! Halafu mnabaki kulaumu mifumo na theory za watu waliokufa zamani.
 
Back
Top Bottom