Chadema Mnajua Madhara ya Kuita Uwekezaji ni Kuuza Nchi au Kugawa Rasilimali za Taifa kwenye Economic Perspective?

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Kuna trend imezuka ya Chadema Kwa makusudi kuamua kuwapotosha Wananchi wasio na uelewa kwamba Uwekezaji ni wizi,kugawa rasilimali za Nchi au kuuza Nchi.

Tabia hii ni mbaya sana kwenye ulimwengu wa biashara na Uchumi na inafanya wawekezaji wawe na mashaka na sera za biashara na Uchumi za Nchi.Aidha wafanyabiashara wanakuwa na mashaka na mwelekeo wa Kisiasa wa Nchi kama inasimamia sera za Kijamaa au sera za soko huria.

Uwekezaji uko Dunia nzima na Tanzania Tukianza huo uwekezaji baada ya sera za ujamaa wanazohubiri Chadema Sasa hivi wakimtolea mfano Magufuli kama mlinzi wa Rasilimali za Nchi.

Magufuli was there,Kwa miaka yake yote 6 Mamilioni ya watu walirudi kwenye umaskini huku Serikali Ikichukua hatamu Kwa Kila kitu.

Hakuna sekta ya uchumi hata Moja ilikuwa na Afya awamu ya 5 kuanzia Kilimo,Ardhi na nyumba, biashara na uwekezaji Hadi Huduma za jamii zote zilikwenda chini na watu walikuwa wana starve,Chadema wanajua vizuri hili.

Kwa Sasa Nchi inapokea maelfu ya wawekezaji kwenye sekta zote kuanzia Kilimo Hadi majengo,viwanda Hadi Utalii ila vyote hivi Chadema wanawaambia watu kwamba Serikali inauza na kugawa Mali zao huku hao Wananchi hawanufaiki Kwa lolote na hapa wanawataja kabisa wanasema Waarabu.

Ukiacha kwamba ni Ubaguzi wa msingi wa rangi ambao wanamhusudisha Rais ila hii ni mbaya sana Kwa Nchi ambayo ndio imeanza kupata nafuu ya Kiuchumi kutokana na Hali mbaya.

Kama Chadema hamtaki Uwekezaji mbona hamsemi namna gani maelfu ya Vijana wanaomaliza vyo watapata kazi? Kama hamtaki Uwekezaji mnategemea Serikali itatoka wapi pesa za Kuendesha Nchi? Kama hamtaki Uwekezaji nyie kama Chadema mnataka nini au mnawasaidiaje Wananchi?

Nawakumbusha tuu Machadema kwamba hakuna rasilimali ambayo Tanzania inayo haipatikani kwingine kwamba Dunia itababaika saana na Tanzania.Kwa swala la uwekezaji ni ushindani Dunia nzima na huko kwenye ushindani sio tuu Baadhi ya Nchi zinawapa wawekezaji Ardhi Bure Bali wanawapa tax holidays za miaka na mfano mzuri ni Rwanda, Ethiopia nk hapo.

Mwisho kulaumu Serikali na kupotosha Umma Kwamba Serikali inagawa Mali Kwa wawekezaji sijui inatoka wapi,Wakiwa Watanzania matajiri ni shida ,Wakiwa Wageni ni shida.Kuna mwekezaji hata mmja ambae halipi Kodi Tanzania hapa au amepata Ardhi bila Kufuata taratibu? Tusilazimishe madaraka Kwa upotoshaji.

My Take
Nawakumbusha watu Hawa wanaosema Nchi inauzwa watakapokuwa kwenye madaraka wao na familia zao hakuna shida watapata wakati maelfu ya watu wa kawaida Wakiwa wanapata shida na ni wakati huo watakuwa wanawasingizia Mabeberu.

Kama hizi ndio Sera za Chadema hapo hakuna Watu,Kuna matapeli wa Kisiasa.
 
Hakuna aliyesema kuwekeza ni kuuza nchi! Tatizo ni sisi kama Taifa tumeuza rasilimali zetu muda mrefu na kama ingekuwa ni uwekezaji wenye tija basi Tanzania ingekuwa number 1 kiuchumi Africa.

Tumevurunda mno kwenye madini tukafikiri tumepata somo lakini ndio tumezidi kuvurunda hadi kutishia uhai wa Taifa na mfano mzuri ni gesi! Gesi tumeharibu beyond repair ndio maana JPM akaona apiganie bwawa la Nyerere.

Baada ya ujinga wa kutisha kwenye mikataba mingi alafu tunaingia tena mkataba wenye sura ile kwenye bandari? Hivi kwanini tusiamini ndani ya CCM kuna usaliti uliofikia kiwango cha uhaini? Mnavuruga rasilimali zote mnataka kurudisha nchi utumwani?
 
Sasa kama mkataba hauonyeshi ukomo unafikiri ni lugha gani itumike kuwaambia wananchi? Na kwa hili CHADEMA wamewapiga counter attack si mjini wala vijijini raia wanajua samia ameuza bandari, kama huamini nenda kuna kijiji kipo inyonga wilaya ya mlele kinaitwa songambele kule hata mtandao wa simu hamna lakini wananchi wana taarifa kuwa Samia kauza bandari.
 
Sijaona wala kusikia sehemu yoyote wanasema uwekezaji ni wizi, lakini wachopigia kelele tangu nyuma huko hua ni utata au ubovu wa vipengele vya mikataba, usipotoshe hata kama huwapendi
 
Mikataba ya kuua na kuwabaka wamasai , kwa ajili ya uwekezaji unao wanufaisha viongozi na watoto wa CCM pamoja na wageni. HAPANA KWA KWELI, haina tija kwa watanganyika.

sana sana tozo tu zinazidi
 
Mikataba ya kuua na kuwabaka wamasai , kwa ajili ya uwekezaji unao wanufaisha viongozi na watoto wa CCM pamoja na wageni. HAPANA KWA KWELI, haina tija kwa watanganyika.

sana sana tozo tu zinazidi
Wakiuawa kama unavyosema hao wawekezaji ni Wana ccm au? Wa masai ndio WA kwanza kuondolewa sehemu Zenye potential?

Maelfu ya watu walioondolewa kwenye migodi sio Watanzania? Harafu ukiacha mambo ya uwekezaji yanayoleta pesa,hao masai kwenye mbuga wanaharibu wameshakuwa wengi.

Tanzania hii imeisha Hadi iwe issue Kwa Wamasai? Nyerere alihamisha watu maeneo tofauti na Asili Yao na kuwapeleka sehemu nyingine hao hawana Haki ila Wamasai?

Acheni upuuzi usio na Tija, doesn't make sense
 
Umeuliza maswali ya msingi sana na umetumia muda wako mwiiingi kueleza mafanikio na sera za uchumi za sasa hasa hasa kwenye uwekezaji na FDI. Shida iliyopo kuna Makundi 2. Moja ni wapinzani nje ya CCM wakiongozwa na CHADEMA hawa hawawezi kusifia lolote maana watakuwa wamejimaliza kisiasa. Watadandia kila hoja mpaka 2025.
Kundi la pili ni CCM wenyewe waliokuwa hawaamini kama Raisi Samia would deliver na wana chuki nae personally as humanbeing,as mwanamke, mswahili na regrettably as Muslim anejielewa. Alichokifanya for 2 years na kidogo ni zaidi maradufu ya kilichofanywa ndani ya miaka 6 ya Mzee Baba. Takwimu zinathibitisha hili.
Hivyo pole kaka. Tutafika tu
Hao wa kundi la pili ndio wanatunga uongo na kuwapa hao machadomo Sasa sijui wao wanakuwa na maslahi gani hasa.

Nchi hii inahitaji pesa na bila pesa haiwezi kwenda na mbaya zaidi watu wanazaa sana na kuzidisha maelfu ya mahitaji ila njia ambazo Dunia nzima inatumika kukuza uchumi Chadema na wapuuzi wao wanawaambia watu eti Rais anauza Nchi,hivi hao wawekezaji hawalipi Kodi? Hawajaariji watzn? Hawatumii malighafi za Tanznaia? Huu ushenzi ukome mara Moja
 
Sasa kama mkataba hauonyeshi ukomo unafikiri ni lugha gani itumike kuwaambia wananchi? Na kwa hili CHADEMA wamewapiga counter attack si mjini wala vijijini raia wanajua samia ameuza bandari, kama huamini nenda kuna kijiji kipo inyonga wilaya ya mlele kinaitwa songambele kule hata mtandao wa simu hamna lakini wananchi wana taarifa kuwa Samia kauza bandari.
Imagine. Sijui wanataka tuseme nini.? Actually, hakuna uwekezaji watakaoufanya zaidi ya kupiga pesa. Hawa Waarabu wamekaa Loliondo kwa zaidi ya miaka 30 na hakuna tulichopata zaidi ya wao kufunga Kangorongoro huko Dubai kwa kutumia wanyama wetu.
 
Simple tu bro uwekezaji usio na manufaa kwa jamii au tanzania , hauna maana

Unawekeza kwa ajili ya ustawi wa jamii, ila kinyume chake ni kuua na kubaka?

Ccm wamewekeza au wameuza madini,gesi nk nenda mtwara kuna nini cha maana wanacho jivunia kutokana na gesi?

Nenda migodoni yamebaki mashimo tu, ila wananchi sasa wanapigika tu na tozo .mafuta juu

kwa ujumla ccm hawawezi kutukwamua na uwekezaji, wanawaza uchaguzi na ufisadi
 
Imagine. Sijui wanataka tuseme nini.? Actually, hakuna uwekezaji watakaoufanya zaidi ya kupiga pesa. Hawa Waarabu wamekaa Loliondo kwa zaidi ya miaka 30 na hakuna tulichopata zaidi ya wao kufunga Kangorongoro huko Dubai kwa kutumia wanyama wetu.
Kwani kazi ya Waarabu wa Loliondo wanaowinda Wana wajibu wa kugawa pesa Kwa watu wa Loliondo au kulipa Kodi Serikalini?

Maeneo mengine yote ambayo Yana wawekezaji Huwa wanagawa pesa Kwa wanavijiji?
 
Hakuna aliyesema kuwekeza ni kuuza nchi! Tatizo ni sisi kama Taifa tumeuza rasilimali zetu muda mrefu na kama ingekuwa ni uwekezaji wenye tija basi Tanzania ingekuwa number 1 kiuchumi Africa.

Tumevurunda mno kwenye madini tukafikiri tumepata somo lakini ndio tumezidi kuvurunda hadi kutishia uhai wa Taifa na mfano mzuri ni gesi! Gesi tumeharibu beyond repair ndio maana JPM akaona apiganie bwawa la Nyerere.

Baada ya ujinga wa kutisha kwenye mikataba mingi alafu tunaingia tena mkataba wenye sura ile kwenye bandari? Hivi kwanini tusiamini ndani ya CCM kuna usaliti uliofikia kiwango cha uhaini? Mnavuruga rasilimali zote mnataka kurudisha nchi utumwani?
Cheki huyu,unaabudu rasilimali kama vile ndio kitu pekee kinachotajirisha. Waulize Venezuela na mafuta Yao kama yamewapa faida yoyote?

Taiwan ni nchi ndogo Haina rasilimali,Singapore na nyeginezo zote hizo ziliwekeza kwenye skills na ujuzi ndio nguzo muhimu kwenye ukuaji wa nchi. Nchi nyingi za Africa watu mbumbumbu kama wewe halafu wanaabudu rasilimali ambazo hawawezi hata kuziutilize vizuri then wanategemea utajiri. 😀😀
 
Tanzania na Venezuela Nchi ipi imeendelea?

Kama unajua rasilimali sio kitu pekee Kwa nini Sasa useme wawekezaji wanaiba Mali? Si ufanye kitu kingine kinachotajirisha?
 
Siku ambayo utajadili hoja bila ushabiki kivyama, unaweza ukawa na jambo la kuhabarisha umma, mbali na hapo bora ukae kimya. Tofautisha kati ya uwekezaji na kukabidhi rasmali za nchi kwa wageni. Kwa mwendo tulionao ni kuuza nchi chini ya mwanvuli wa uwekezaji. Inawezekana wewe ndiye uelewi usisingizie kuwa wananchi hawana uelewa!!
Achaga upuuzi.Mali zipi zinakabidhiwa Kwa Wageni na Kwa sababu ipi?
 
20141018_MAP004_0.jpg

Watanzania hawajaridhika na mkataba wa Bandari yake Salama. Serikali isione aibu kuachana na Waarabu.Tunaposema Bandari Imegawiwa, maana yake Imegawiwa,
 
Wawekezaji ni Lugha nyingine ya kusema Wakoloni mamboleo.

Hatahivyo tujiulize

Kuna Uhaini Tanzania?

Kama Uhaini upo hao wawekezaji wakome huko huko, manake vuta nikuvute haijamalizika na Dola ipo kushughulikia wahaini, ni kwamba, hawana muda wa kuwalinda wawekezaji majambazi.
 
Back
Top Bottom