El Jefe
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 293
- 364
Nimeangalia baadhi ya hizo unazoita 'uongo' kwenye hizo links mbili, na nimegundua kuna maneno mengi tu ambayo yametafsiriwa kimakosa kama uongo. Inawezekana sio kimakosa bali ni kwa makusudi kabisa ili kutimiza ajenda fulani.(a) Kwa uwongo kuna ripoti kila sehemu: Pitia website ya Politifact au Washingtonpost uone.
Kama mtu anaorodhesha na kuweka kumbukumbu ya maneno ya uongo ya mtu mwingine, halafu katika mchakato huo na yeye anasema uongo, nadhani mtu huyo anakuwa sio wa kutegemewa kama chanzo cha taarifa.
Huo unaouita "utapeli" (fraud) ulithibitishwa mahakamani? Maana kama mtu ametapeliwa ana-file 'civil lawsuit'.(b) Kwa utapeli alifikia kunyimwa mikopo na subcontractors wakawa hwataki kumfanyia kazi bila malipo kwanza:: Pitia historia yake ya utapeli na bankrupticies utajua kwa nini alikuwa hakopeshwi tena na mabeki yote ya Marekani isipokuwa Deutsche Bank tu?
Bankruptcy ni mchakato wa kawaida kwa biashara, mtu au taasisi zinazopitia hali ngumu kifedha!
Kampuni zinapo-file bankruptcy mahakamani (chapter 11 protection) ina maana haziwezi kulipa madeni yake kwahiyo zinauza assets ili kulipa madeni na kuanza upya au kusuka upya deal la kulipa madeni (restructuring debt) na sheria inayalinda makampuni hayo.
Madhara ya zoezi hili pamoja na mambo mengine ni kuongeza 'credit risk' kwa aliye-file, na kusababisha ugumu kupata mikopo mipya na kupata huduma au bidhaa kwa mkopo!
Kwahiyo ku-file bankruptcy kama Trump alivyofanya, ni mkakati mzuri tu na wa kawaida wa kulipa madeni katika 'corporate America'.
Mazingira (circumstances) yanayozunguka hali fulani yanaweza kuhalalisha matumizi ya maneno makali.(c) Kwa roho mbaya hilo liko wazi kabisa: Ukiacha hiyo ya birther na ya McCain kutokumshukuru kwa mazishi ya kitaifa, angalau nadhani unalijua hili
Kwa mfano, hiyo link inazungumzia Trump kutumia maneno makali dhidi ya watu waliotuhumiwa kwa ubakaji. Trump aliguswa na kitendo cha kikatili cha kubakwa kwa mwanadada Trisha na hivyo kupelekea kusema anahitaji kurudishwa kwa hukumu ya kunyongwa hadi kufa (death penalty) New York dhidi ya waliohusika.
Jimbo la New York halina hukumu ya kunyongwa hadi kufa. Kama kuhitaji hukumu hiyo katika hali hiyo maana yake ni roho mbaya, basi watu wengi wana roho mbaya.
Kuna States 30 Marekani bado zinaruhusu hukumu ya kunyongwa hadi kufa. Tanzania bado kuna hukumu ya kunyongwa hadi kufa.