Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,276
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,276 2,000
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,276
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,276 2,000
VIUNGANI DC WIKI HII
RAIS Trump aselelea (Hit rock bottom)
Nyuma ya Pazia anataka mazungumzo na Iran, ngoma nzito

Kama kuna anayemfanya Rais mstaafu Obama aonekane kiongozi bora ni Rais Trump.

Rais Trump aliwahi kumwita Rais Obama ''stupid leader'' na kwamba dunia iliwacheka Wamarekani kwa uongozi wake.

Kama hilo lilikuwa kweli, kwasasa dunia haicheki tena bali imepigwa ganzi, butwaa na kutundawaa

Wiki hii baada ya kuahirisha safari ya Poland kuhudhuria maadhimisho ya vita ya dunia, Rais Trump alionekana akicheza golf huku tishio la dhoruba Dorian likizidi kurindima.
Ni Trump aliyemshambulia sana Obama kwamba anacheza golf kuliko Tiger Woods
Katika miaka 3 ya utawala Trump amecheza golf kumzidi Obama ndani ya miaka 8.

Habari kubwa ni ya kiongozi huyo kutofahamu habari zinazotolewa na serikali yake kuhusu hali ya hewa akiwa pia hajui ramani ya nchi yake na kuwa gumzo la kitaifa na kimataifa.

Trump alidai Dhoruba ya Dorian itaikumba Alabama huku akibadilisha ramani ya mamlaka za hali ya hewa ili kukidhi haja yake na si uhalisia wa kitaaluma.

Tatizo si kufanya makosa bali kuyatetea kwa njia za kitoto chini ya hadhi ya ofisi hiyo kubwa.

Rais ametumia kila aina ya ushawishi kuthibitisha madai yake ya uongo bila mafanikio.
Dhalili anayoipata mbele ya jamii yake ni kubwa na ya kusikitisha kwa namna yoyote ile.

Ukuta
Rais Trump anatumia pesa zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za jeshi na miradi mingine ili kujenga ukuta. Ikumbukwa Rais aliahidi ukuta utalipiwa na Mexico, kwasasa unalipiwa na Wamarekani. Haya tuliwahikuyaeleza na kwamba Trump alikuwa akilaghai wafuasi wake.

Hali ya uchumi
Takwimu zinaonyesha kudorora kwa ajira, mwezi wa 8 ukiwa umetengeneza ajira 130, 000 kati ya hizo 25,000 si za kudumu. Vigezo vingine havina mabadiliko makubwa lakini kwa kulinganisha na muda na hali ya uchumi aliyopokea, namba hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na mtangulizi wake Obama. Vita yake ya uchumi haionekani kumsaidia

Trump amemshambulia mkuu wa Bank kuu (Reserve Bank) aliyemtea mwenyewe kwa madai kuwa anaongeza riba na hivyo kuathiri uchumi.

Trump anasema wakati wa Obama viwango havikuongezwa bila kufikiri wakati huo uchumi ulikuwa katika recession na kwamba alikabidhiwa uchumi ulioimarika tofauti na mtangulizi wake.

Meli ya Iran
Zipo taarifa za Afisa wa WH kumshawishi Nahodha wa meli iliyokuwa imeshikiliwa na UK aipeleke Marekani. Kama tulivyowahi kusema, UK ilitumika tu na US kuishikilia meli hiyo.

Nahodha aliahidiwa Pesa na kutukumbusha Trump alivyomsema Obama kupeleka pesa Tehran zilizokuwa mali ya Iran kama sehemu ya deal ya Nyuklia, Trump anafanya kile alichokilaani.

Iran Deal
Nyuma ya pazi taarifa zinaeleza maafisa wa Marekani wana haha kuishawishi Iran irudi katika meza ya majadiliano kuhusu silaha za nyuklia.

Trump alikumbana na wakati mgumu wakati wa G7 alipojaribu kuwashawishi wanachama waungane naye kuhusu Iran huku wakimueleza alijitoa katika deal bila kuwaeleza.
Sasa Trump anarudi kule kule kwa Obama kuhusu Deal

Iran yaahidi kurutubisha Nyuklia
Iran nayo imesema sasa haitatekeleza sehemu kubwa ya Deal na nchi za Ulaya na kuanza kurutubisha mitambo yake ya Nyuklia.

Uamuzi wa Iran ni baada ya kuona udhaifu wa Marekani na kwamba Iran inataka nchi za Ulaya zifanye jambo kurahisha maisha magumu yanayotokana na vikwazo.
Hoja yao ni kuwa ndani ya deal hawaoni matokeo yoyote.

Mpango wa US kuishambulia Iran kwa kushirikiana na Israel unaonekana kukwama.
Tatizo linalojitokeza si nguvu za kijeshi za Iran, bali ushawishi wa Iran katika eneo la mashariki ya kati na kwamba kinachotokea kinaweza kuwa kikubwa zaidi ya kinachoendelea Afghanistan

Deal na Talibani
Serikali ya Trump imekuwa katika mazungumzo na Talibani na imekubaliana nao kuondoa askari wake kwa kiwango kutoka nchi hiyo. Mazungumzo na Talibani hayakuanza leo, Republican na Trump walimkashifu sana Obama alipojaribu kukaa mezani na Telebani.
Leo Republicans na Trump wamerejea kule kule kwa Rais Obama

Kwa hadhi ya jengo jeupe la viungani DC Rais Trump kaselelea chini ya Mwamba(hit rock bottom). Kwa siasa za kimataifa sasa anafuata nyayo za Obama. Kwa hali ya uchumi hofu kubwa ni mdororo mikononi mwake.

Hayo yote yanachigiza sehemu ya jamii kuhoji utayari wake kuongoza Taifa hilo wakitilia mashaka uwezo wake kiakili, lakini pia kumfanya Obama ang'are

Tusemezane
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,263
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,263 2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,276
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,276 2,000
VIUNGANI DC WIKI HII

Habari ya Taliban kuzungumza na utawala wa Trump imethibitika na hilo lilikuwa litokee katika nyumba ya Rais ya mapumziko ya kikazi 'Camp David''

Kwa kumbukumbu, Camp David ni eneo muhimu la majadiliano kuhusu hali ya usalama wa nchi ya Marekani iwe kisiasa au kiuchumi.

Ni eneo ambalo Waziri mkuu wa Israel Menachem Begin na Rais Anwar Sadat wa Misri walifikia makubaliano ya amani chini ya usimamizi wa Rais Jimmy Carter kwa kile kinachojulikana kama Camp David accords.
Misri ilitambua Israel na Israel ikarudisha Sinai Peninsula lililotokana na vita iliyoanza mwaka 1948

Ni makubaliano hayo ndiyo yaliyoplekea kifo cha Anwar Sadat kwa baadhi ya Waarabu kusema Sadat amewasaliti.

Kwa upande wa Israel huo ulikuwa ushindi mkubwa kwasababu Misri ni Taifa lilikokaribu sana na lenye nguvu za kijeshi.

Tangu wakati huo Misri imekuwa msuluhishi wa mgogoro kati ya Wapalestina na Israel.

Katika hali isiyo ya kawaida, Rais Trump aliwaalika Taliban kwa mazungumzo ya amani Camp David, siku 4 kabla ya maadhimisho ya 9/11 ambako Talibani wakiwa washirika wa Alqaeda walifanya yao dhidi ya Taifa kubwa.

Kuwaalika Taliban ilikuwa kofi la uso dhidi ya Republicans ambao siku zote hawakuta kusikia Rais Obama anaingia majadiliano nao.

Mbaya Taliban walialikwa Camp David kama wageni mashuhuri siku chache kabla ya 9/11

Kufuatia mashambulizi Afghanistan, Rais Trump alikatisha mazungumzo hayo.

Hata hivyo habari za ndani ni kuwa VP Pence na Mshauri wa Usalama John Bolton hawakukubaliana na hatua ya Rais Trump hasa kuelekea 9/11

Nyuma ya pazia kulikuwa na mtifuano kati ya Secretary of state( huku kwetu waziri wa mambo ya nje) na John Bolton mshauri wa Usalama.

Bolton inaelezwa kuwa na misimamo mikali hasa siasa za Korea Kaskazini na Iran na kwamba Pompeo ni mnyenyekevu kwa Trump aliyemtimua John Bolton leo hii.

Bolton kabla ya hapo alikuwa balozi wa Marekani UN na baadaye kuwa mwanasiasa nguli katika Televisheni akimnanga Obama kuhusu siasa za nje.

Leo akitazama nyuma, Bolton atajisikia mnyonge kwani kutimuliwa kwake hakukuwa na stara.

John Bolton ni mshauri wa 3 wa Rais Trump kutimuliwa na katika muda wa miaka 3 .
Rais Trump anaelekea kuwa na mshauri wa 4.

Hili linaeleza siasa za nje za Marekani zilivyo shaghabala chini ya Make America great again.

Ni haki kusema hakuna anayejua Rais Trump anasimamia nini na ana mkakati gani kuhusu siasa za nje. Korea kaskazini hali ni ile ile, Iran hali inazidi kuwa mbaya, huku kukiwa na fukunyuku Japan na Korea kusini.

Vita ya uchumi na China haionekani kusaidia hali wakati nchi washirika wa Ulaya zikionekana kujitenga na Mtawala Trump. Mashariki ya kati hakuna kinachoendelea !

Hayo yote yakiendelea hakuna ushahidi wowote kwamba siasa za Trump zimeweza kufanya mabadiliko aliyoahidi zaidi ya kuvuruga hali ya mambo.

Wakati huo huo Rais wa Taifa hilo lenye nguvu za kiuchumi na ulinzi ameendelea kuwa na malumbano ya hovyo kabisa na kudhalilisha na Raia wa kawaida.

Kwa sehemu kubwa Rais Trump amekuwa kichekesho cha dunia na kama alivyowahi kusema ikiwa dunia iliicheka Marekani kwa siasa za Obama, kwasasa haicheki tena, dunia imepigwa ganzi na kutunduwaa ikijuiliza hii ni Marekani wanayoijua ?

Tusemezane
 
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,993
Points
1,500
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,993 1,500
Kila siku huwa najiuliza ile kauli ya "we do not talk to terrorists" au "we do not negotiate with terrorists" sijui imeishia wapi. The Donald ni kituko sana, ashukuru Mungu yeye ni mzungu,. Kila siku huwa najiuliza ingekuwaje kama Obama angefanya robo ya aliyofanya Trump.

Issue ya Bolton ni wazi kabisa, unajua ukiangalia kwenye maswala ya sera ya mambo ya nje Trump na Obama kimisngi hawana tofauti, japokuwa Obama kama rais kwa kiasi fulani alikuwa kulia sana.Naamini Bolton angeweza kudumu kwenye serikali ya Obama kama angekuwepo, kuliko ya The Donald.
 

Forum statistics

Threads 1,335,209
Members 512,271
Posts 32,499,212
Top