Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,639
2,000
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
8,966
2,000
Kwa ufahamisho tu, House ilipoanza impeachment proceedings dhidi ya Richard Nixon, wengi wa Republicans hawakuunga mkono lakini hizo proceedings ndizo ziliibua ushahidi uliowawezesha hata hao Republicans kubadilisha msimamo. Kabla ya hapo alikuwepo Republican mmoja tu aliyejitokeza na kuunga mkono impeachment ya Nixon lakini baada ya ushahidi wa tapes kuibuliwa kwenye proceedings ndipo na wenzake walipounga mkono.

Hali kama hiyo ndiyo ipo mpaka sasa lakini tofauti inayojitokeza wakati huu ni Spika Pelosi kutaka kabla ya hizo proceedings kuanza ushahidi zaidi upatikane na anajua utapatikana. Hivyo anawataka Democrats kwenda taratibu bila pupa ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kujua kwa nini Donald Trump awe impeached. Viongozi wengi wastaafu wa GOP tayari wanaanza kujitokeza kuunga mkono wazo la kumtaka Rais Trump awe impeached.

Katika wiki ya kesho mengi zaidi yataibuliwa kulingana na kesi zinazoendelea mjini New York chini ya grand juries zilizoundwa na Robert Mueller ambapo baadhi ya redactions alizofanya AG Barr zimeamriwa zianikwe kwa wananchi. Na hapa ndipo Trump anapopata wazimu kwa nini impeachment haianzi mara moja kama alivyotegemea yeye. Alitaka impeachment ianze huku wananchi walio wengi ikiwa bado hawajui kinachoendelea lakini Pelosi katia breki.

Hasira yote ya Trump inaanzia hapo; mipango yake na wanasheria wake imevurugika kwani hawajui ni lini House itaanza proceedings na hajui ushahidi utakaokuwa umepatikana wakati huo. Ndugu zangu Marekani mambo kama haya huenda taratibu na si kwa pupa kama wengi wananvyofikiria. Sheria ya Marekani inawalinda sana wenye tuhuma mbali mbali na ni pale tu ushahidi unatosheleza ndipo hatua huchukuliwa na hili Pelosi analijua fika.

Halafu ipo hii dhana inayoenezwa zaidi na GOP kwamba impeachment inaweza ikawaathiri sana Democrats kwenye uchaguzi ujao. Hii ni kweli inaweza ikatokea kama Democrats hawakujipanga vizuri lakini kwa style ya Pelosi ya kukataa kukurupuka bila ushahidi wa wazi na unaojitosheleza. Pia wanafuatilia matamshi yote ya Trump na kila kauli anayotoa inachunguzwa kwa umakini mkubwa kwa sababu wanajua woga wake ndio unamfanya aropoke hovyo.
Enzi hizo wamarekani walikuwa na adui mmoja tu: USSR; kwa hiyo internal politics hazikuwa tribal kama leo. Siasa za Marekani zilianza kubadilikwa mwaka 1992. Baada ya Soviet Union kubomoka, halafu Clinton (mtoto wa maskini) akaja kumshinda George H.W Bush, wamarekani walianza kugawanyika. Ile health care plan ya Clinton ilipigwa vita vibaya sana wakati huo ambayo ndiyo hii Obamacare ya leo ambayo wamarekani wanaikimbilia. Vita hiyo ndiyo iliyosababisha Republican kuwa majority kwenye Congress baada ya miaka 40. Sasa Gingritch ndiye aliyeharibu kabisa siasa za Marekani, kwani tangu alivyoanza siasa a chuki binafsi dhidi ya Clinton mwaka 1994 hali ndiyo inayoendelea tena hadi leo; wanasiasa wanatazamana kwa chama tu, hawatazamani kwa msingi wa utaifa tena.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,639
2,000
"Kichuguu, post: 31664771, member: 348"
Ina maana hufuatilii habari hizo kwa karibu na wala hujui hili hapa
Unaonyesha kutokujua namna ya kuunganisha habari za kisheria.
Mueller anasema kuwa yeye hakuwa amepewa mamlaka ya kumshitaki Trump, na pia amesema utaratibu wa fairness unamzuia kumtuhumu mtu bila kumpeleka mahakani akajitetetee.
Kwa hiyo akasema hawakumtuhumu kwa hatia, na pia hawakuona kuwa hana hatia. Hiyo ni neutral conclusion ambayo Barr asingeitumia kusema kuwa hana Trump hatia. Hana mamlaka ya kusema nani ana hatia au hana hatia; kazi yao ni kutuhumu na kuziachia mahakama kuamua kama kuna hati au vipi.
Hili lipo wazi kabisa, kwamba, kumtuhumu mtu bila kumfikisha mahakamani kujitetea si haki. Tena hoja hiyo ameitumia AG Barr anaposema '' taarifa ya Mueller itakuwa ''redacted' katika makundi manne
Intelligence info , security info, grand jury materials na watu waliotajwa ambao hawakushtakiwa
Sababu ya watu hao kuwa redacted ni kwa ukweli kuwa hawakupewa nafasi ya kujitetea''
Prosecutor anakutuhumu tu anapodhani una hatia. Iwapo wangemwona hana hatia, wangesema kuwa hatumkuta na hatia yoyote ya kumtuhumu. Kuna lugha nyingi za kutumia, kwa mfano hakuna ushahidi wowote, au ushahdi tuliopata hautoshi kumtuhumu, kama ambavyo walivyosema kwenye volume 1. Hata hiyo conclusion ya volume 1, ilisema tu ushahidi upo wa conspiracy, lakini hautoshi kuprove beyond reasonable doubts- standard ya criminal prosecution.
Mkuu Mag3 na Kigarama #816 wamesisitiza sana kuwa siasa za US zikiangaliwa kwa jicho la Tanzania mtu atatatizika sana. Kuna Wanasheria Marekani wanasubiri fursa, lugha tu inaweza kuwapa fursa wanayotaka.

Mchakato wa kumshtaki Rais wa US si rahisi, unahitaji ushahidi unaojitosheleza.

Kauli ya Mueller kuwa hakukuwepo na ''sufficient evidence'' haina maana hakukuwepo ushahidi. Mfano, Don Jr kualika Warusi Trump haiwezi kuwa kosa

Kutotoa taarifa kwa FBI kwamba Warusi walikuwa na ''dirty' za Clinton ni kukosa busara ni ''misdemeanor '' . Kuwakaribisha Warusi, kushirikiana nao kupata dirty kwa njia zisizo halali ni kosa ''criminal offence''. Sasa je, ushahidi ulikuwepo wa kutosha kuwa ''criminal offence''?

Michael Cohen alisema Trump anaongea au kutoa maagizo kwa ''code''.
Kwahiyo kunatakiwa ushahidi wa kutosha kuunganisha codes na uhalifu kama upo.

Michael Flynn yupo katika kikaango kwasababu upo ushahidi wa kutosha.

Leo simu alizokuwa anapiga simu zipo. Hiyo ndiyo sufficeint evidence na underlying evidence

Trump aliposema ''Russia if you have 30,000 email....'' na kweli zikatoka siku hiyo haitoshi kuwa ni kosa. Ni lazima kuwe na ushahidi wa kuunganisha bila shaka kauli na kitendo hata kama tunajua alitumia codes kuwasiliana na Russia, ndiyo sufficient evidence inayotakiwa
Kama unakumbuka mwaka 2016 kabla ya uchaguzi, Combey alilaumiwa sana kwa kumtuhumu mams Clinton halafu na kuishia kusemahakuna ushahidi wa kutosha kumshitaki. Hiyo inaitwa character assassination ambayo wanasheria hawafanyi hivyo mahakamani.
Kuntu, kama haelewi hataelewa tena
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,639
2,000
Trump anajivuna kuwa uchumi umekuwa imara chini yake huku ikiwa wazi kuwa hakubadilisha trajectory ya Obama, aaliingia kweye msafara wakati uko kwenye lango halafu anajivuna kuwa ni yeye aliyeingiza msafara ndani.
Mkuu hii hoja inatumiwa sana na Trump bila kuangalia ukweli au kwa nia ya kupotosha tu. Trump anajua miongoni mwa wafuasi wapo watakaomeza tu
1. Obama akiingia madarakani US ilikuwa na uchumi unaokaribia ku collapse.

Ajira zilikuwa zinapotea kwa 300K kwa mwezi. Inflation ilikuwa juu, Unemployment baadhi ya maeneo ilifikia 11%. Alikuwa anasimamia vita Iraq na Afghanistan, masoko yakipoteza thamani, Dow ikiwa 6K, GDP ikiwa negative kwa muda uliotosha ku qualify kama recession

2. Obama akiondoka ajira zilizotengenezwa zilikuwa kwa miezi takribani 74 mfululizo. Ukiangalia na ajira za kila mwezi baada ya Trump hakuna tofauti bali utofauti wa mwezi na mwezi

Sasa Trump anasema unemployment imefikia takribani 3% akiwa amepokea nchi katika 4.8%
Kumbuka Obama alitoka 11% hadi 4% katika mazingira ya kutoka recession.

Hivyo Trump anaposema unemployment imefikia all time low, haelezi ni kutoka katika kiwango gani. Kama angeanzia 11% hadi 3% tungesema, lakini kutoka 4.8% kwenda 3% siyo low kwa vigezo halisi.

Lakini namba haziongopi, GDP inakua katika 4%. Je wakati Obama akiwa na negative hesabu zimezingatia namba baina ya negative na positive kabla ya kuongelea positive inayoonekana?

Katika kuonyesha hilo, Trump na McConnel na Paul Ryan wamefuta sheria nyingi sana za Obama isipokuwa ile ya taasisi za fedha. Ni kwanini?
Jibu ni rahisi, sheria zile ndizo zilimpa leverage katika uchumi

Jambo la kuchekesha sana wakati wa Obama ni Trump huyu huyu aliponda takwimu zinazotolewa ambazo leo anazitumia.

Unemployment kushuka wakati wa Obama anasema ni fake, leo anasema ni real.

Flip flop za Trump haziishi hapo, miezi miwili iliyopita alisema Mueller ni honorable man,he conducted himself well.

Hii ni baada ya kumeza tango pori la AG Barr na kwavile hasomi hata daily briefings akajikuta anaingia mzima mzima

Leo anasema Mueller alikwenda oval office. Si kweli, yeye ndiye alimwalika oval office na ni Mueller aliyekataa kazi akisema ametumikia vya kutosha kwa awamu zote Obama na Bush

Trump anasema Mueller ni conflicted kutokana na mambo ya biashara. Ni yule yule aliyesema ni honorable man akiwa na gold standard report. Leo hakauki katika tweeter kumshambulia honorable man, Mueller

Kama alivyosema Mag3 baada ya kuhadithiwa ubaya wa taarifa ya Mueller sasa anafyatuka kulia kushoto, usiku mchana kama ilivyokuwa jana na dakika 18 pale WH

Tulipoanza uzi huu tulieleza kuwa kumfukuza Comey tena akitamba ni kwasababu ya Russia, ilikuwa ni kosa la obstruction of justice. Hilo pamoja na mengine ndiyo yanamtesa kwa sasa
Tulisema Obstruction of justice ni mbaya kuliko Russia

Namuelewa sana Nancy, Chuck na Nadler. Wanajua ushahidi lazima ujitosheleze na Mueller aliwasaidia kwa kutawanya kesi 12 ambazo kama ilivyojulikana leo Michael Flynn na Dowd mwanasheria wa Trump walikuwa katika mazungumzo

Kutawanya kesi ilikuwa mbinu kwa kujua Mueller hakuwa na uwezo wa kumshtaki, lakini sasa evidence na redacted report zinatoka kwa mlango wa Mahakama

Trump anajua, ili Flynn au Rogers Stones wajinasue ni lazima ushahidi uambatane na evidence ambazo kwa namna moja au nyingine zinamtia Trump matatani. Ndiyo maana DOJ wamekataa kutoa baadhi ya mikanda ya mazungumzo kati ya Flynn na Balozi wa Russia Kislyak

Kwa mtazamo huo, kama tulivyosema siku za nyuma ngoma ni mbichi sana. Trump atacheza na Russia kila uchao. Na kwa bahati jitihada za kufifisha mjadala wanazipiga vita wenyewe
AG Barr kuunda timu ya kuchunguza wachunguzi ni kurudisha donda la Russia livuje damu

Huwezi kusema it's time to move on wakati kuna uchunguzi wa wachunguzi wa Russia
Kwa lugha ya mabeberu hili ni self inflicted wound''

Tusemezane
 
El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
Kwa hiyo akasema hawakumtuhumu kwa hatia, na pia hawakuona kuwa hana hatia. Hiyo ni neutral conclusion ambayo Barr asingeitumia kusema kuwa hana Trump hatia.
Katika misingi ya haki, tunasema mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo (presumption of innocence). Katika misingi hiyo muendesha mashtaka hawezi kumtuhumu (indict) mtu hadi awe na ushahidi wa kutosha. Akiwa nayo, mashtaka (prosecution) yanafuata mahakamani, halafu hatia (conviction) au hamna hatia (innocence).

Mueller hakumu-indict Trump katika ripoti yake. Kwa maana kwamba hakuhitimisha kuwa ushahidi aliokusanya unamtosha kumtuhumu kwa kosa la "obstruction." Badala yake hakutoa hitimisho kuhusiana na kesi hiyo.

"..we did not draw ultimate conclusions about the President's conduct."

Ukisoma vizuri conclusion nzima ya Mueller, hakutoa hitimisho la kusema kosa limetendwa kutokana na masuala magumu (difficult issues) ya matendo na dhamira ya Rais aliyokutana nayo, ambayo amesema yanahitaji kuwa resolved kwanza.

"The evidence we obtained about the President's actions and intent presents difficult issues that would need to be resolved if we were making a traditional prosecutorial judgement"

Hakuwa na haja ya kusema hili kwenye hitimisho lake kama lengo lake toka mwanzo lilikuwa ni kutaka utaratibu mwingine utumike kufanya maamuzi. Conclusion ndipo mahali ujumbe husika unapopatikana. Hakuna neno lolote kwenye conclusion ya Mueller lenye muelekeo wa kuitaka Congress ikaamue kuhusu obstruction.

Ukisoma Code of Federal Regulations ya mwaka 1999 na sababu za kushindwa ku-renew Ethics in Government Act ya mwaka 1977, utagundua kuwa AG amepewa mamlaka makubwa katika uteuzi na kumsimamia Special Counsel. Kwa kifupi AG ndiye Bosi wa Special Counsel.

Special Counsel aliandika ripoti akampa bosi wake, akisema amekutana na masuala magumu yanayohitaji kutatuliwa ili kutoa uamuzi fulani. AG kama Chief Prosecutor kwa kushirikiana na Deputy wake na OLC wakatatua masuala hayo na kuhitimisha kuwa ushahidi uliokusanywa hautoshelezi kumtuhumu Trump kwa obstruction.

Hana mamlaka ya kusema nani ana hatia au hana hatia; kazi yao ni kutuhumu na kuziachia mahakama kuamua kama kuna hati au vipi.
Hakuna sehemu AG Barr amesema Trump hana hatia, hiyo ni tafsiri yako kama ilivyo kwa watu wengine. Bali Barr alichosema ni kwamba ushahidi uliokusanywa kwenye uchunguzi wa Special Counsel hautoshelezi kudai kuwa Rais amefanya kosa la obstruction.

"After reviewing the Special Counsel's final report on these issues.....Deputy Attorney General Rod Rosenstein and I have concluded that the evidence developed during the Special Counsel's investigation is not sufficient to establish that the President committed an obstruction-of-justice offense."

Mueller ndiye hakuwa na mamlaka ya kusema Trump hana hatia maana hiyo sio kazi yake.

"while this report does not conclude that the president committed a crime, it also does not exonerate him.”

Prosecutor anakutuhumu tu anapodhani una hatia. Iwapo wangemwona hana hatia, wangesema kuwa hatumkuta na hatia yoyote ya kumtuhumu. Kuna lugha nyingi za kutumia, kwa mfano hakuna ushahidi wowote, au ushahdi tuliopata hautoshi kumtuhumu, kama ambavyo walivyosema kwenye volume 1. Hata hiyo conclusion ya volume 1, ilisema tu ushahidi upo wa conspiracy, lakini hautoshi kuprove beyond reasonable doubts- standard ya criminal prosecution.
Prosecutor anafanya kazi zaidi ya indictment (kutuhumu mtu kuwa ana hatia), kwa maana kwamba anamshtaki (prosecution) mtuhumiwa kwa kosa fulani ili mahakama iamue kama kuna hatia au lah!

Basis ya hoja yako na kuweka screenshot ni kwamba hukubali kwamba prosector anam-prove mtu "guilty" na sio "innocent"!

Kama unaamini kwamba kwenye mfumo wa haki tuna-assume mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo, prosecutor anawezaje kufanya kazi ya kuthibisha kuwa mtu hana hatia (kwa maana ya "exoneration")? Ina maana ali-assume ana hatia kabla?

Nafikiri hiki kipande hiki chini ndicho hukuelewa kabisa, inagwa nimeshakigusia hapo juu. Huwezi kumtuhumu mtu ambaye huwezi kumshitaki akajitetea. Mueller alifanya kazi chini ya huo msingi kuwa huwezi kumshitaki Rais; kwa hiyo asingeweza kusema kuwa kuwa ana hatia, kwa vile hakuwa na uwezo wa kumshitaki (Department policy) na kumpa nafasi ya kujitetea (principles of fairness). Kama unakumbuka mwaka 2016 kabla ya uchaguzi, Combey alilaumiwa sana kwa kumtuhumu mams Clinton halafu na kuishia kusemahakuna ushahidi wa kutosha kumshitaki. Hiyo inaitwa character assassination ambayo wanasheria hawafanyi hivyo mahakamani.
Maelezo mazuri, wala hamna aliyesema Mueller anaweza kumshtaki Rais aliye madarakani, wala aliyepinga fairness principle kwa jinsi alivyoitumia Mueller.

Sentensi hiyo ndiyo nyepesi kuliko zote. Anakuambia kuwa criminal justice system aliyokuwa akiendesha haina mamlaka ya kumtuhumu rais kwa makosa; katiba ina utaratibu mwingine wa kufanya hivyo. Maana yake nikuwa utaratibuhuo mwingine ndio utumike.
Amesema hivyo kwenye ripoti yake? Amezungumzia hilo kwenye hitimisho lake? Alishindwaje hata kuandika hilo pendekezo?

Again; bado ninaheshimu first ammendment rights zako.
Jambo la muhimu ni kwamba Mueller hajahitimisha kuhusu obatruction, sio kwa sababu ya utaratibu wa kikatiba unaohusu indictment na prosecution ya Rais aliye madarakani, hapana! Conclusion ya ripoti yake ipo wazi na inaelezea sababu wazi.

Mueller sio Special Counsel wa kwanza kumchunguza Rais aliye madarakani, Ken Starr alihitimisha uchunguzi wake kwa kupata ushahidi wa kutosha dhidi ya Bill Clinton.

Unadhani, Mueller angepata ushahidi wa kutosha (sufficient evidence) kwenye "conspiracy", conclusion yake ya Volume I angeiandikaje?

Endelea tu kuheshimu hizo 'rights' mkuu!

Tena hoja hiyo ameitumia AG Barr anaposema '' taarifa ya Mueller itakuwa ''redacted' katika makundi manne: Intelligence info , security info, grand jury materials na watu waliotajwa ambao hawakushtakiwa, Sababu ya watu hao kuwa redacted ni kwa ukweli kuwa hawakupewa nafasi ya kujitetea''
Pepripheral third parties sio watu ambao hawakupewa nafasi ya kujitetea, bali ni watu ambao hawakuwa charged na hivyo hawawezi kupata nafasi ya kujitetea.

Mkuu Nguruvi3 mbona hujaonyesha sehemu niliposema underlying evidence zimepigwa mstari?
 
El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
..anajivuna kuwa uchumi umekuwa imara chini yake huku ikiwa wazi kuwa hakubadilisha trajectory ya Obama, aaliingia kweye msafara wakati uko kwenye lango halafu anajivuna kuwa ni yeye aliyeingiza msafara ndani.
Kusema kuwa taarifa nzuri za kiuchumi ni "trajectory ya Obama" ni kupindisha ukweli. Tukiuliza Obama alifanya nini hadi mwezi June mwaka 2016, cha kusababisha uwekezaji kuongezeka US leo hii na kuongekeza kwa ajira, hamna jibu!

Hebu tuwalinganishe kidogo Obama na Trump kwenye vipengele hivi viwili : uchumi na ajira;

(Nitatumia namba za miaka miwili ya mwisho ya awamu ya pili ya Obama ili kuondoa visingizio, nikilinganisha na miaka miwili ya mwanzo ya Trump; tutatumia ulinganisho ulio fair na unao-make sense).

(i) Ukuaji wa GDP: Uchumi ulikuwa ukikua kwenye 1.5% katika kipindi cha miezi 18 ya mwisho ya Obama, wakati ulikua mara mbili hadi asilimia 3% katika miezi 18 ya mwanzo ya Trump.

(ii) Ongezeko la nafasi za ajira (job openings): Ongezeko la nafasi za ajira ilikuwa wastani wa nafasi 900 kwa mwezi - kwa miezi 21 ya mwisho ya Obama, wakati ongezeko hilo likiwa ni wastani wa nafasi 75,000 kwa mwezi - kwa miezi 21 ya mwanzo ya Trump.

(iii) Walioajiriwa: Kwa kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama, idadi ya wamarekani walioajiriwa iliongezeka kwa wastani wa watu 157,000 kwa mwezi, huku idadi hiyo ikikua kwa wastani wa watu 214,000 kwa mwezi kwa miezi 21 ya mwanzo ya Trump (ongezeko la 36%).

Ukosefu wa ajira haujawahi kuwa chini kama ulivyo sasa kwa wamarekani weusi, latino na wenye asili ya Asia. Ukosefu wa ajira kwa sasa ni 3.6% (wa chini kuliko toka mwaka 1969).

Utafiti wa Harvard na Princeton unaonesha kuwa 95% ya ajira alizotengeneza Obama kwa miaka yote minane ni kazi za muda mfupi (temporary, part time + mishahara midogo).

(iv) Ajira za viwandani (manufacturing): Katika kipindi cha miezi 21 ya mwanzo ya Trump, ajira 396,000+ za manufacuring zimeongezeka, hiyo idadi ni zaidi ya mara 10 ya idadi ya ajira hizo katika kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama. Obama alishusha ajira hizi kwa 122,000 katika miaka yake minane. Hizi ndizo ajira ambazo Obama alisema Trump anahitaji muujiza kuzirudisha maana haziwezi kurudi.

(v) Mapato ya wiki (weekly earnings): Katika kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama, WE ilipanda kwa wastani wa $1.3 kwa mwezi, huku ikipanda kwa wastani wa $2.31 (ongezeko la 76%) katika miezi 21 ya mwanzo ya Trump.

Obama huwa anadai kuhusika na taarifa nzuri za Uchumi katika kipindi cha Trump na Biden anadai hivyo pia. Kitu ambacho sio kweli kwa sababu namba hazidanganyi. FACT ni kwamba uchumi wa US upo vizuri katika kipindi cha Trump kuliko cha Obama. Dems wanaoelewa hawataki hata kuzungumzia uchumi wanaona bora wakomae na uchunguzi dhidi ya Trump.

Trump ni mfanyabiashara anayejua biashara na uwekezaji unahitaji nini. Ndio maana alivyoingia tu akashusha kodi kadhaa ikiwemo ya makampuni kutoka 35% hadi 21% kwenye tax reform yake, na kuondoa kanuni rundo zilizokwamisha uwekezaji. Matokeo yake uchumi ukapanda.

Obama kwa upande mwingine ni mwanasiasa asiye na uzoefu kwenye uwekezaji, biashara na uchumi. Hata Romney aliongelea hili kwenye Debate yake na Obama mwaka 2012.

Kwamba Obama ameacha legacy ya Uchumi bora Marekani? Labda sio kwa FACTS.

Huyu jamaa naona la,a mo takataka sana. Ana miaka sabini lakini amekuwa kila siku mlalamishi wa kutaka attention tu.
Haya mambo ya kuwa anaandika twitts kila wakati kulalamika lalamika, au kudaia kusifiwa ni dalaili ya utoto sana, na nadhani marais wengine wote wamshamjua; Rais wa China hana taimu naye tena. Trump hanywi pombee ila naona amezeeka na akili ya kitoto.
Sidhani kama kuna tatizo Trump kutumia twitter kufikisha ujumbe wake kwa wananchi, ikizingatiwa kuwa media zimekuwa too biased na mifano ni mingi mno mpaka imekuwa wazi sana.

Lakini, watu wenye chuki za wazi kama zako dhidi ya Trump ndio unakuta Mueller aliwateua kumsaidia kumchunguza Trump!
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,031
2,000
Flashback...1974

The late Lawrence J. Hogan Sr., a Maryland politician was the first Republican member of the House Judiciary Committee to call for President Nixon’s impeachment. His stand cost him support from the Republican party and his voting base, and he lost the Republican gubernatorial primary a month after Nixon resigned. “I assumed that in coming out for impeachment I would lose the nomination, which I did,” Hogan said in 1987.

Fast forward...2019

Justin Amash as the first Republican in Congress to call for the impeachment of Donald Trump is facing his own party’s wrath.
In a series of tweets on Saturday, the Michigan congressman said attempts to obstruct justice as outlined in special counsel Robert Mueller’s report on Russian interference in the 2016 election amounted to “impeachable conduct”. He also accused the attorney general, William Barr, of misleading the US public.

To be continued...
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,031
2,000
Flashback...1974

During the Watergate scandal, the majority of the American people initially opposed impeachment proceedings being launched against President Richard Nixon.

1974......................................2019
Same woman over 40 years later...!
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
8,966
2,000
Katika misingi ya haki, tunasema mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo (presumption of innocence). Katika misingi hiyo muendesha mashtaka hawezi kumtuhumu (indict) mtu hadi awe na ushahidi wa kutosha. Akiwa nayo, mashtaka (prosecution) yanafuata mahakamani, halafu hatia (conviction) au hamna hatia (innocence).

Mueller hakumu-indict Trump katika ripoti yake. Kwa maana kwamba hakuhitimisha kuwa ushahidi aliokusanya unamtosha kumtuhumu kwa kosa la "obstruction." Badala yake hakutoa hitimisho kuhusiana na kesi hiyo.

"..we did not draw ultimate conclusions about the President's conduct."

Ukisoma vizuri conclusion nzima ya Mueller, hakutoa hitimisho la kusema kosa limetendwa kutokana na masuala magumu (difficult issues) ya matendo na dhamira ya Rais aliyokutana nayo, ambayo amesema yanahitaji kuwa resolved kwanza.

"The evidence we obtained about the President's actions and intent presents difficult issues that would need to be resolved if we were making a traditional prosecutorial judgement"

Hakuwa na haja ya kusema hili kwenye hitimisho lake kama lengo lake toka mwanzo lilikuwa ni kutaka utaratibu mwingine utumike kufanya maamuzi. Conclusion ndipo mahali ujumbe husika unapopatikana. Hakuna neno lolote kwenye conclusion ya Mueller lenye muelekeo wa kuitaka Congress ikaamue kuhusu obstruction.

Ukisoma Code of Federal Regulations ya mwaka 1999 na sababu za kushindwa ku-renew Ethics in Government Act ya mwaka 1977, utagundua kuwa AG amepewa mamlaka makubwa katika uteuzi na kumsimamia Special Counsel. Kwa kifupi AG ndiye Bosi wa Special Counsel.

Special Counsel aliandika ripoti akampa bosi wake, akisema amekutana na masuala magumu yanayohitaji kutatuliwa ili kutoa uamuzi fulani. AG kama Chief Prosecutor kwa kushirikiana na Deputy wake na OLC wakatatua masuala hayo na kuhitimisha kuwa ushahidi uliokusanywa hautoshelezi kumtuhumu Trump kwa obstruction.Hakuna sehemu AG Barr amesema Trump hana hatia, hiyo ni tafsiri yako kama ilivyo kwa watu wengine. Bali Barr alichosema ni kwamba ushahidi uliokusanywa kwenye uchunguzi wa Special Counsel hautoshelezi kudai kuwa Rais amefanya kosa la obstruction.

"After reviewing the Special Counsel's final report on these issues.....Deputy Attorney General Rod Rosenstein and I have concluded that the evidence developed during the Special Counsel's investigation is not sufficient to establish that the President committed an obstruction-of-justice offense."

Mueller ndiye hakuwa na mamlaka ya kusema Trump hana hatia maana hiyo sio kazi yake.

"while this report does not conclude that the president committed a crime, it also does not exonerate him.”Prosecutor anafanya kazi zaidi ya indictment (kutuhumu mtu kuwa ana hatia), kwa maana kwamba anamshtaki (prosecution) mtuhumiwa kwa kosa fulani ili mahakama iamue kama kuna hatia au lah!

Basis ya hoja yako na kuweka screenshot ni kwamba hukubali kwamba prosector anam-prove mtu "guilty" na sio "innocent"!

Kama unaamini kwamba kwenye mfumo wa haki tuna-assume mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo, prosecutor anawezaje kufanya kazi ya kuthibisha kuwa mtu hana hatia (kwa maana ya "exoneration")? Ina maana ali-assume ana hatia kabla?

Maelezo mazuri, wala hamna aliyesema Mueller anaweza kumshtaki Rais aliye madarakani, wala aliyepinga fairness principle kwa jinsi alivyoitumia Mueller.Amesema hivyo kwenye ripoti yake? Amezungumzia hilo kwenye hitimisho lake? Alishindwaje hata kuandika hilo pendekezo?Jambo la muhimu ni kwamba Mueller hajahitimisha kuhusu obatruction, sio kwa sababu ya utaratibu wa kikatiba unaohusu indictment na prosecution ya Rais aliye madarakani, hapana! Conclusion ya ripoti yake ipo wazi na inaelezea sababu wazi.

Mueller sio Special Counsel wa kwanza kumchunguza Rais aliye madarakani, Ken Starr alihitimisha uchunguzi wake kwa kupata ushahidi wa kutosha dhidi ya Bill Clinton.

Unadhani, Mueller angepata ushahidi wa kutosha (sufficient evidence) kwenye "conspiracy", conclusion yake ya Volume I angeiandikaje?

Endelea tu kuheshimu hizo 'rights' mkuu!Pepripheral third parties sio watu ambao hawakupewa nafasi ya kujitetea, bali ni watu ambao hawakuwa charged na hivyo hawawezi kupata nafasi ya kujitetea.

Mkuu Nguruvi3 mbona hujaonyesha sehemu niliposema underlying evidence zimepigwa mstari?
Tatizo lako wewe unasoma msitali mmoja mmoja badala ya kusoma context yote. Kwa upande conspirancy, ilionekana kuwa ushahidi uliopo hautoshi; yaani kuna ushahidi lakini hautoshi kupeleka mahakamani (kwenye crimal law); hiyo siyo kusema there was NO COLLUSION. Kwanza katika sheria hakuna kitu kinaitwa Collusion, lakini AG Barr ambaye ndiye mwanasheria mkuu wa nchi aliimba mara hivyo kadhaa kabla hajatoa ripotu yenyewe.

AG kuhitimisha kuwa there was no obstruction of justice na kufunga mjadala ni kwa sababu alikuwa na hoja ya siku nyingi hata kabla hajawa AG; kwa hiyo alitoa hitimisho hilo bila hata ya kusoma ripoti yenyewe. Alikuwa akisoma kutafuta mistali inayosaidia kuhitimisha maoni yake, siyo kuelewa ripoti ina maana gani. Hiyo inaitwa confimation bias.

Kusema kuwa taarifa nzuri za kiuchumi ni "trajectory ya Obama" ni kupindisha ukweli. Tukiuliza Obama alifanya nini hadi mwezi June mwaka 2016, cha kusababisha uwekezaji kuongezeka US leo hii na kuongekeza kwa ajira, hamna jibu!

Hebu tuwalinganishe kidogo Obama na Trump kwenye vipengele hivi viwili : uchumi na ajira;

(Nitatumia namba za miaka miwili ya mwisho ya awamu ya pili ya Obama ili kuondoa visingizio, nikilinganisha na miaka miwili ya mwanzo ya Trump; tutatumia ulinganisho ulio fair na unao-make sense).

(i) Ukuaji wa GDP: Uchumi ulikuwa ukikua kwenye 1.5% katika kipindi cha miezi 18 ya mwisho ya Obama, wakati ulikua mara mbili hadi asilimia 3% katika miezi 18 ya mwanzo ya Trump.

(ii) Ongezeko la nafasi za ajira (job openings): Ongezeko la nafasi za ajira ilikuwa wastani wa nafasi 900 kwa mwezi - kwa miezi 21 ya mwisho ya Obama, wakati ongezeko hilo likiwa ni wastani wa nafasi 75,000 kwa mwezi - kwa miezi 21 ya mwanzo ya Trump.

(iii) Walioajiriwa: Kwa kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama, idadi ya wamarekani walioajiriwa iliongezeka kwa wastani wa watu 157,000 kwa mwezi, huku idadi hiyo ikikua kwa wastani wa watu 214,000 kwa mwezi kwa miezi 21 ya mwanzo ya Trump (ongezeko la 36%).

Ukosefu wa ajira haujawahi kuwa chini kama ulivyo sasa kwa wamarekani weusi, latino na wenye asili ya Asia. Ukosefu wa ajira kwa sasa ni 3.6% (wa chini kuliko toka mwaka 1969).

Utafiti wa Harvard na Princeton unaonesha kuwa 95% ya ajira alizotengeneza Obama kwa miaka yote minane ni kazi za muda mfupi (temporary, part time + mishahara midogo).

(iv) Ajira za viwandani (manufacturing): Katika kipindi cha miezi 21 ya mwanzo ya Trump, ajira 396,000+ za manufacuring zimeongezeka, hiyo idadi ni zaidi ya mara 10 ya idadi ya ajira hizo katika kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama. Obama alishusha ajira hizi kwa 122,000 katika miaka yake minane. Hizi ndizo ajira ambazo Obama alisema Trump anahitaji muujiza kuzirudisha maana haziwezi kurudi.

(v) Mapato ya wiki (weekly earnings): Katika kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama, WE ilipanda kwa wastani wa $1.3 kwa mwezi, huku ikipanda kwa wastani wa $2.31 (ongezeko la 76%) katika miezi 21 ya mwanzo ya Trump.

Obama huwa anadai kuhusika na taarifa nzuri za Uchumi katika kipindi cha Trump na Biden anadai hivyo pia. Kitu ambacho sio kweli kwa sababu namba hazidanganyi. FACT ni kwamba uchumi wa US upo vizuri katika kipindi cha Trump kuliko cha Obama. Dems wanaoelewa hawataki hata kuzungumzia uchumi wanaona bora wakomae na uchunguzi dhidi ya Trump.

Trump ni mfanyabiashara anayejua biashara na uwekezaji unahitaji nini. Ndio maana alivyoingia tu akashusha kodi kadhaa ikiwemo ya makampuni kutoka 35% hadi 21% kwenye tax reform yake, na kuondoa kanuni rundo zilizokwamisha uwekezaji. Matokeo yake uchumi ukapanda.

Obama kwa upande mwingine ni mwanasiasa asiye na uzoefu kwenye uwekezaji, biashara na uchumi. Hata Romney aliongelea hili kwenye Debate yake na Obama mwaka 2012.

Kwamba Obama ameacha legacy ya Uchumi bora Marekani? Labda sio kwa FACTS.

Sidhani kama kuna tatizo Trump kutumia twitter kufikisha ujumbe wake kwa wananchi, ikizingatiwa kuwa media zimekuwa too biased na mifano ni mingi mno mpaka imekuwa wazi sana.

Lakini, watu wenye chuki za wazi kama zako dhidi ya Trump ndio unakuta Mueller aliwateua kumsaidia kumchunguza Trump!
Angalia data hizi za unemployment rate: Kuna change gani ya trajectory? jJe kweli unaona kuwa graph imebadilika ghafla wakati wa Trump kulinganisha na wakati wa Obama?
1114805

Halafu angalia data za GDP growth rate: Je kweli unaona kuwa wakati wa Trump uchumi umekuwa kwa kasi kubwa kweli?

1114809
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,639
2,000
Naona na wewe unataka kulisha wana JF matango pori.

Kwa ambao wameweza kusoma ripoti yote na underlying evidence wameona wazi kabisa kwamba ugomvi wa Mueller na Barr ni hatua ya Barr kutoa maelezo ya uongo.

Ripoti ambayo Mueller alitaka iwasilishwe Congress kama ilivyo ilikuwa ni ripoti waliyokwishaifanyia reductions zinazotakiwa kiutaratibu.

Hii ndiyo sababu hakupendezwa kabisa na alichokuwa akifanya Barr kwani barua yake ya kwanza ilipotosha kila kitu kilichotakiwa kitolewe kwa umma.
Kiini cha mzozo wa Mueller na AG Barr ni kuhusu executive summary. Ukisoma barua ya Mueller aliyoandika, ni wazi kasema kila jambo la usalama lilizingatiwa na kuondolewa katika exec summary
Tena alisisitiza kwamba executive summary ilikuwa kwa ajili ya public

AG Barr hakutumia executive summary kwa kujua ingetoa picha kubwa zaidi na kufunika uchafu kama alivyotaka. Hadi leo hakuna anayejua exec summary ilisema nini

Katika kuonyesha amekerwa, Mueller alikataa kupitia ''summary ya AG Barr''
Alifahamu summary ya Barr ilipotosha na hakutaka kuingia katika mkenge huo wa tango pori

Leo tunajua Barr alilisha watu tango pori kwa wiki kadhaa kabla ya ripoti. Mueller kasema haku establish conspiracy, Barr anasema hakuna collusion. Conspiracy na collusion ni vitu tofauti, kimoja kikiwa katika legal term na kingine kikiwa lugha ya mtaani ya Barr na Trump

Barr anasema mamlaka kuhusu obstruction of justice aliachiwa na Mueller.
Mueller anasema hilo halikuwepo na kwamba, taarifa imeeleza kwa kina

Kuna watu wanaeneza uongo katika utaratibu wa tango pori kwakusema AG Barr ametoa kurasa 448. No! alichokifanya ni kutoa redacted version, halafu kuna redacted version ya Gang of eight. Halafu kuna taarifa kamili ambayo haijulikani kama itaona jua siku yoyote, ipo kizani

Lakini si hilo tu, kuna eneo lingine lisilowekwa hadharani '' counter intelligence''
Hili limefichwa bila kujulikana ni kwanini kiasi kwamba Gang of 8 ya congress nao hawaruhusiwi kuona. Kumbuka gang of 8 ina mamlaka ya kusoma ''top secret' za nchi
 
El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
Tatizo lako wewe unasoma msitali mmoja mmoja badala ya kusoma context yote. Kwa upande conspirancy, ilionekana kuwa ushahidi uliopo hautoshi; yaani kuna ushahidi lakini hautoshi kupeleka mahakamani (kwenye crimal law); hiyo siyo kusema there was NO COLLUSION. Kwanza katika sheria hakuna kitu kinaitwa Collusion, lakini AG Barr ambaye ndiye mwanasheria mkuu wa nchi aliimba mara hivyo kadhaa kabla hajatoa ripotu yenyewe.
Kwahiyo, hoja yako mpya kwamba Barr ametumia neno "collusion".

Neno "collusion" lilianza kutumiwa hata ya kabla Barr hajateuliwa kuwa AG. Hilo neno lilitumiwa na Dems na vyombo vya habari, na kuenea kwa umma kama crime, kabla na baada ya uteuzi wa Mueller.

Hata mawasiliano ya DOJ baina ya Deputy AG Rosenstein na Mueller (Kabla Barr hajaja DOJ) yalitumia neno "collude", pamoja na mawasiliano ya umma.

"Office recorgnized that the word "collude" was used in communications with the Acting Attorney General confirming certain aspects of the investigator's scope and the term has frequently been invoked in public reporting about the investigation"-Page 2 (Vol I, Parag.4)

Mueller anaeleza kwamba kwenye memorandum ya August 2, 2017 aliagizwa na Rosenstein kuchunguza tuhuma za maafisa wa Trump kutenda "collusion".

"..Investigate allegations that three Trump campaign officials...committed a crime or crimes by colluding with Russian government officials with respect to the Russian government's efforts to interference with the 2016 presidential election"- (Page 11, Vol I, Parag. ya mwisho)

Lakini pia ukiangalia Appointment Order No. 3915-2017 ya kumteua Mueller (Appendix A-1), hakuna alipoambiwa achunguze "conspiracy", bali "links na/au coordination"

Hata hivyo, neno "coordination" haina maana inayoeleweka kisheria.

"Like collusion, "coordination" does not have a settled definition in federal law"- Page 2 (Vol I, Parag.4)

Ndipo Mueller akaamua kuwa badala ya kuchunguza "collusion" au "coordination", achunguze "conspiracy".

"The Office's focus in analyzing questions of joint criminal liability was on conspiracy as defined in federal law"- Page 2 (Vol I, Parag.4)

What difference does it make?

AG kuhitimisha kuwa there was no obstruction of justice na kufunga mjadala ni kwa sababu alikuwa na hoja ya siku nyingi hata kabla hajawa AG; kwa hiyo alitoa hitimisho hilo bila hata ya kusoma. Alikuwa akisoma kutafuta mistali inayosaidia kuhitimisha maoni yake, siyo kuelewa ripoti ina maana gani. Hiyo inaitwa confimation bias.
Umeambatanisha memorandum ya AG Barr kwenda kwa Rosenstein yenye kuonyesha kutofautiana na theories za "obstruction"za Mueller.

Ukaambatanisha na ripoti ya Mueller (ambayo sina uhakika kama umeisoma), kwa maelezo kwamba Barr hajaisoma! Ingawa huwezi kuthibitisha hoja hii!

Lakini nadhani dhamira yako imesukumwa ni kule kudhani kuwa mimi binafsi sijaisoma!. Naomba nikuhakikishie tu kwamba ripoti ya Mueller (redacted) nishaisoma na kuielewa.

Umemzungumzia AG Barr peke yake, lakini Barr anasema yeye na Rosenstein wote wanatofautiana na Mueller kwenye theories zake. Pia uamuzi wa kutom-charge Trump na "obstruction", haukuwa wa Barr peke yake, bali ni wa Barr na Rosenstein.

"Although the Deputy Attorney General and I disagreed with some of the Special Counsel’s legal theories and felt that some of the episodes examined did not amount to obstruction as a matter of law, we did not rely solely on that in making our decision"

Kwahiyo AG Barr na Rosenstein (aliyemteua Mueller) wote waliongozwa na "confirmation bias"?

Angalia data hizi za unemployment rate: Kuna change gani ya trajectory? Je kweli unaona kuwa graph imebadilika ghafla wakati wa Trump kulinganisha na wakati wa Obama?
Hoja yako ni kwamba kwa sababu 'graph haijabadilika ghafla' maana yake Trump hajamzidi Obama kwenye kushusha tatizo la ajira!.

Kwanza, Obama kwa miaka yote rate ya chini aliyowahi kufikisha ni 4.8%. Hii rate ni ya kawaida ukiangalia hiyo "trajectory" yako (retrospectively) hadi miaka ya 1990s au nyuma zaidi, ndio maana sio habari kuifikisha. Hii ni race to the lowest rate.

Pili, ukiangalia hiyo graph kwa miezi (monthly basis) utaona hayo 'mabadiliko ya ghafla' vizuri kuliko kwa miaka.

Tatu, inabidi utafsiri hizo rate kwenda kwenye namba au idadi ya waajiriwa ili upate picha kamili kuwa uchumi umekuwa ukiongeza waajiriwa kiasi gani kwa wastani kwa mwezi, kwa miaka kadhaa. Ndicho nilichokifanya kwenye post #905.

Hii hoja kwamba 'kama wote tunaelekea juu basi wote tupo sawa,' haiwezi kufaa katika kupata ulinganisho sahihi.

Halafu angalia data za GDP growth rate: Je kweli unaona kuwa wakati wa Trump uchumi umekuwa kwa kasi kubwa kweli?
Graph uliyoweka sio sahihi maana GDP growth rate haikuwahi kuvuka 3% kwa miaka uliyoonyesha.

Ukuaji wa GDP US umekuwa chini ya 3.0% kwa mda mrefu, hadi watu wakaanza kuita hali hiyo "new normal".

Ila Trump amevunja dari hilo hadi 3.2% kwa robo ya mwaka huu, asilimia ambazo Obama hakuwahi kufikisha. Unaweza kudhani kutoka 3.0% hadi 3.2% haina maana kwenye uchumi mkubwa duniani. Lakini ina maana sana, kwa mfano ukiangalia wastani wa ongezeko la job openings kwa mwezi kwa miezi 21 ya mwisho ya Obama na ya mwanzo ya Trump utaona tofauti kubwa kama nilivyoeleza kwenye post #905.

Ukiangalia pia indicators kama stock markets indexes, business and consumer confidence, investments, exports v imports etc utaona tofauti kubwa sana kati ya hao Marais wawili.
 
(1) Ile ripoti ya Mueller haikuwa na picha.
(2) Hizo graph za uchumi zimetoka US Bureau of Economic Analysis.

Wakati wa Obama GDP ilivuka 3.0% mara nyingi sana labda kama huwezi kusoma graph, ila kwa vile alikuwa anavuta uchumi kutoka shimoni, wengine wenu hawamkuona movement hiyo kwa sababu mlitaka uchumi uwe getini siku hiyo hiyo mlipouporomosaha, kama ambavyo Trump aliukuta umeshafika. Uchumi wa Trump haujavunja record ya Obama. Kujenga ghorofa huchukua miaka mingi sana ila kulibomoa inachukua dakika cheche tu. Kama unazijua cycles za Marekani na kodi, basi subiri uone. Imebaki miezi kumi tu, Marekani irudi shimoni tena mpaka Obama mwingine atokeee.

Hizo indicators nyinge unazotumia ni BS kabisa kwani hazina uhusiano wowote na ukuaji wa uchumi. Ukitaka data kamili ziko hapa
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,031
2,000
(1) Ile ripoti ya Mueller haikuwa na picha.
(2) Hizo graph za uchumi zimetoka US Bureau of Economic Analysis.

Wakati wa Obama GDP ilivuka 3.0% mara nyingi sana labda kama huwezi kusoma graph, ila kwa vile alikuwa anavuta uchumi kutoka shimoni, wengine wenu hawamkuona movement hiyo kwa sababu mlitaka uchumi uwe getini siku hiyo hiyo mlipouporomosaha, kama ambavyo Trump aliukuta umeshafika. Uchumi wa trump haujavuta Kujenga ghorofa huchukua miaka mingi sana ila kulibomoa inachukua sdakika cheche tu. Kama unazijua cycles za Marekani na kodi, basi subiri uone. Imebaki miezi kumi tu, Marekani irudi shimoni tena.

Hizo indicators nyinge unazotumia ni BS kabisa kwani hazina uhusiano wowote na ukuaji wa uchumi. Ukitaka data kamili ziko hapa
Huyo El Jefe siku nyingi nimeachana naye, sijui Trump alimpa nini. Kuna wakati alikuwa anasifia sana stock market akisahau ni Obama aliyeitoa shimoni na Trump kaja kudakia tu na wakati anaidakia Dow Jones ilikuwa tayari inaisogelea 20,000 kutoka 5,000 alikoitoa Obama. Siku hizi haongelei tena stock market wala deni la taifa wala bei ya bidhaa chini ya Trump kwa sababu indiketa zote zinaonesha uchumi unakoelekea.
 
hao ndio voters wa Trump!
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,639
2,000
Wakuu Kichuguu na Mag3 , kama lipo jambo Trump amefanikiwa ni kuifanya Republicans isiwe ile Rep bali Republicans ya Trumpism. Amewatisha sana

Ukimsikiliza Lindsey Graham wa iliyokuwa Amigo akiwa na McCain na Liberman utashangaa
Graham amebaki kuokota mipira ya golf Marla-lago akitetea hata upuuzi

Akina Ted Cruiz na Rubio wapo kimyaa kama wamenyeshewa mvua.
Walikuwa mwiba kwa Obama wakiongozwa na McConnel aliyetak Obama awe one term pres

Hakuna anyeongelea uchumi ulikuwa wapi hadi uka qualify nchi kuwa katika recession

Hakuna anyeongelea vigezo vyote vya uchumi wakati ule na sasa. Wote wamebaki na kauli moja '' robust economy''. Katika suala la uchumi Obama ndiye aliyetengeneza akapokea Trump

Wengi hawatambui kuwa recession haikuanzia na George Bush, ilianza wakati wa Reagan
Deregulations hasa taasisi za pesa ndizo zilizopelekea anguko la uchumi baada ya muda

Kuitoa GDP katika negative na kuipeleka positive territory kwa uchumi mkubwa kama wa US si jambo la usiku mmoja. Kujenga consumer confidence baada ya hasara si jambo la usiku mmoja
Kutengeneza ajira kwa miezi 74 continuous ndicho kigezo cha recession kumalizika

Mambo aliyofanya Obama taratibu yanajidhihiri na ndiyo maana anazidi kuwa maarufu

Obamacare: Hadi leo hakuna anyetueleza sera ya Trump ni ipi na iko wapi
Wamarekani wanagundua kufuata Obamacare ilikuwa mkenge kwasababu hawaoni mbadala

Nuclear deal: Trump alidhani Iran nuclear deal ilikuwa hovyo akaifuta mara moja.
Katika miaka 2 hajawa na mbadala wa deal hiyo.
Leo akiwa Switzeland Pompeo anasema US ipo tayari kujadiliana na Iran bila condition.
Hii maana yake tayari wamekwama wanataka kurudi kwa OB

TPP: Obama alikazania sana TPP si kwasababu ya uchumi, bali kwa kuelewa usalama wa Marekani unategemea uchumi. Hivyo, US kuwa kiranja wa TPP ilikuwa mbinu ya kumdhibiti Mchina. Trump akafuta mara moja, ingawa sasa anarudi kwa mlango wa nyuma akimtumia VP

Trade War: Vita ya uchumi na China inaendelea Trump akiwaaminisha wafuasi wake kuwa zile tariff anazowekea Wachina atakayelipa ni China na si Mmarekani kama ilivyokuwa ''wall-mexico''

Hapa Trump anaumiza Wamarekani maeneo mengi, kwanza, tariff zitalipiwa na consumers US

Pili, retaliation ya tariff inaathiri Wakulima wake wanaouza Soya na bidhaa nyingine China

Tatu, makampuni kama GMC yanayojitanua kibiashara China yatafunga shughuli kwasababu ya kushindwa competition katika price

Haya yote yanatokea kukiwa na suala jingine la debt. Kwamba, lazima debt ceiling iongezwe

Katika mazingira ya kawaida na hasa waliyokuwa wanamsakama nayo Obama, ilitegemewa Republicans wawe wakali katika trade kwani wao wanaamini free trade na si protectionism.

Walitakiwa wawe wakali katika debt kwani huamini udogo na matumizi kidogo

Kwavile iliyopo ni Trumpisim na si Republicans, kila kitu kimyaaa!

Na hilo pia linaeleza ya Mueller. Ukisoma historia waliosimamia katiba wakati wa Nixon na kumuondoa walikuwa Republicans, siyo hii ya Trumpism na Barr

Tusemezane
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,031
2,000
Wakuu Kichuguu na Mag3
Obamacare: Hadi leo hakuna anyetueleza sera ya Trump ni ipi na iko wapi
Wamarekani wanagundua kufuta Obamacare ilikuwa mkenge kwa sababu hawaoni mbadala
Mkuu Nguruvi3, naomba nikukumbushe kidogo matango pori aliyotaka kutulisha El Jefe kuhusu ACA au kwa lugha ya Republicans Obama Care, nanukuu;
Halafu niseme tu kwa wale watu wanaoshikilia bango Obamacare, kuwa haitafutwa na kwamba ikifutwa itafuta wengi Congress waelewe tu kwamba wataofutwa Congress mwaka 2018 ni Democrats na sio Republicans maana ni ya kwao.
Kuna watu wengi tu walimpigia Rais Trump kura kwa ahadi ya ku-repeal na ku-replace Obamacare maana ilikuwa na bado inawaumiza. Rais Trump yupo smart sana, anawaacha wanapiga kelele, wakati hiyo Plan itakapofika Congress kabla ya Mid-term elections watakuwa na wakati mgumu either kulinda 'legacy ya Obama' au kupinga kila kitu kama wengi wao walivyoamua kufanya.
Na hiyo itaishia kuwa-cost wao zaidi kwenye Mid-term elections na Republicans wanaweza kupata Senators 60+, ukizingatia kuna Senators 10 (Democrats) wanaenda kwenye re-elections kwenye States alizoshinda Rais Trump. Kwa mtu asiyejua atasema Rais Trump hana mbadala wa ObamaCare ndio maana anasema Repeal na Replace inaweza kufanyika mwaka 2018. The good thing ni kwamba with President Trump, it will be done.
Tofauti na alivyotabiri El Jefe, Obama Care bado ipo na Trump ni kweli hakuwa na mbadala lakini Democrats kwa kutetea Obama Care waliweza kuchukua House kwa ushindi mkubwa. Huyu jamaa ni wa kuachana naye, yaonekana anawapenda sana viongozi waongo, matapeli na wenye roho kuntu.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
8,966
2,000
Mkuu Nguruvi3, naomba nikukumbushe kidogo matango pori aliyotaka kutulisha El Jefe kuhusu ACA au kwa lugha ya Republicans Obama Care, nanukuu;

Tofauti na alivyotabiri El Jefe, Obama Care bado ipo na Trump ni kweli hakuwa na mbadala lakini Democrats kwa kutetea Obama Care waliweza kuchukua House kwa ushindi mkubwa. Huyu jamaa ni wa kuachana naye, yaonekana anawapenda sana viongozi waongo, matapeli na wenye roho kuntu.
Mtu yeyote anayemani kuwa Trump ni smart lazima ana matatizo makubwa sana ya kiakili.
 
El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
(2) Hizo graph za uchumi zimetoka US Bureau of Economic Analysis.
Inaeleweka kwamba ulitaka kuonyesha kuwa taarifa zako zimetoka moja kwa moja kwenye "horse's mouth."

Hizo rates kwenye graph yako ya awali, labda ni za 'nominal' lakini sio za 'real' GDP growth, 'latter' ikizingatia mfumuko wa bei.

Kuwa halisi (real), zungumzia vitu halisi.

Wakati wa Obama GDP ilivuka 3.0% mara nyingi sana labda kama huwezi kusoma graph, ila kwa vile alikuwa anavuta uchumi kutoka shimoni, wengine wenu hawamkuona movement hiyo kwa sababu mlitaka uchumi uwe getini siku hiyo hiyo mlipouporomosaha, kama ambavyo Trump aliukuta umeshafika. Uchumi wa Trump haujavunja record ya Obama. Kujenga ghorofa huchukua miaka mingi sana ila kulibomoa inachukua dakika cheche tu.
Link ya graph uliyoweka ya BEA ina kichwa cha habari: "Real Gross Domestic Product: Percent Change From Quarter One Year Ago."

Unaelewaje maana ya "percentage change from quarter one year ago", kwa kulinganisha na hoja yako kwamba "wakati wa Obama GDP ilivuka 3.0% mara nyingi sana"?

Kama unazijua cycles za Marekani na kodi, basi subiri uone. Imebaki miezi kumi tu, Marekani irudi shimoni tena mpaka Obama mwingine atokeee.
Hapa naona unaanza kuzumgumza kama nabii.

Hizo indicators nyinge unazotumia ni BS kabisa kwani hazina uhusiano wowote na ukuaji wa uchumi.
Kwa mfano indicators zipi ni "BS kabisa na hazina uhusiano wowote na ukuaji wa uchumi"?

Ukitaka data kamili, ziko hapa
Umejuaje sina data kamili?
 
El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
Huyo El Jefe siku nyingi nimeachana naye, sijui Trump alimpa nini. Kuna wakati alikuwa anasifia sana stock market akisahau ni Obama aliyeitoa shimoni na Trump kaja kudakia tu na wakati anaidakia Dow Jones ilikuwa tayari inaisogelea 20,000 kutoka 5,000 alikoitoa Obama. Siku hizi haongelei tena stock market wala deni la taifa wala bei ya bidhaa chini ya Trump kwa sababu indiketa zote zinaonesha uchumi unakoelekea.
Mkuu Mag3 ,kumbe upo pia interested na majadiliano ya stock market, national debt na inflation??.....nilidhani upo interested na majadiliano ya "impeachment" ya Trump pekee, kutafuta unredacted report na underlying evidence kwa sababu "kuna mengi yamefichwa na Barr kwa mwamvuli wa grand jury materials" , kumshtaki Barr mwenyewe, kuhoji mashahidi waliokwishahojiwa na Mueller, kutafuta financial records na tax returns za Trump, kuchunguza upya "conspiracy", kufananisha watergate na uchunguzi wa Mueller, na kutafuta "hoja nzito" za kushawishi Republicans wamgeuke na kumuondoa Trump!!

Hii series ni zaidi ya Game of Thrones!
 
El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
Tofauti na alivyotabiri El Jefe, Obama Care bado ipo na Trump ni kweli hakuwa na mbadala lakini Democrats kwa kutetea Obama Care waliweza kuchukua House kwa ushindi mkubwa. Huyu jamaa ni wa kuachana naye, yaonekana anawapenda sana viongozi waongo, matapeli na wenye roho kuntu.
John McCain 'aliharibu sherehe' siku ile, Obamacare ingeshaondoka! Ndio maana Dems wanamsifia sana McCain.

Trump ni "tapeli, muongo na mwenye roho ngumu,"!! aisee! mnawezaje kumchukia mtu ambaye hajafanya crime kiasi hicho? Ukisoma comments za Kichuguu kwenye post #898 , za Nguruvi3 ndio kabisa yupo biased na anapanick sana! Mpo serious sana wakuu!

Obama kuna sera zake na maamuzi yake sikukubaliana nayo, lakini nimejifunza vitu vingi sana kutoka kwake, na yeye binafsi amekuwa honest kusema anadhani aliingia kwenye ile nafasi mapema sana!
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
8,966
2,000
John McCain 'aliharibu sherehe' siku ile, Obamacare ingeshaondoka! Ndio maana Dems wanamsifia sana McCain.

Trump ni "tapeli, muongo na mwenye roho ngumu,"!! aisee! mnawezaje kumchukia mtu kiasi hicho? Ukisoma comments za Kichuguu kwenye post #898 , za Nguruvi3 ndio kabisa yupo biased na anapanick sana! Mpo serious sana wakuu!

Obama kuna sera zake na maamuzi yake sikukubaliana nayo, lakini nimejifunza vitu vingi sana kutoka kwake, na yeye binafsi amekuwa honest kusema anadhani aliingia kwenye ile nafasi mapema sana!
(a) Kwa uwongo kuna ripoti kila sehemu: Pitia website ya Politifact au Washingtonpost uone.
(b) Kwa utapeli alifikia kunyimwa mikopo na subcontractors wakawa hwataki kumfanyia kazi bila malipo kwanza:: Pitia historia yake ya utapeli na bankrupticies utajua kwa nini alikuwa hakopeshwi tena na mabeki yote ya Marekani isipokuwa Deutsche Bank tu?
(c) Kwa roho mbaya hilo liko wazi kabisa: Ukiacha hiyo ya birther na ya McCain kutokumshukuru kwa mazishi ya kitaifa, angalau nadhani unalijua hili
 
Top Bottom