Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
(a) Kwa uwongo kuna ripoti kila sehemu: Pitia website ya Politifact au Washingtonpost uone.
Nimeangalia baadhi ya hizo unazoita 'uongo' kwenye hizo links mbili, na nimegundua kuna maneno mengi tu ambayo yametafsiriwa kimakosa kama uongo. Inawezekana sio kimakosa bali ni kwa makusudi kabisa ili kutimiza ajenda fulani.

Kama mtu anaorodhesha na kuweka kumbukumbu ya maneno ya uongo ya mtu mwingine, halafu katika mchakato huo na yeye anasema uongo, nadhani mtu huyo anakuwa sio wa kutegemewa kama chanzo cha taarifa.
(b) Kwa utapeli alifikia kunyimwa mikopo na subcontractors wakawa hwataki kumfanyia kazi bila malipo kwanza:: Pitia historia yake ya utapeli na bankrupticies utajua kwa nini alikuwa hakopeshwi tena na mabeki yote ya Marekani isipokuwa Deutsche Bank tu?
Huo unaouita "utapeli" (fraud) ulithibitishwa mahakamani? Maana kama mtu ametapeliwa ana-file 'civil lawsuit'.

Bankruptcy ni mchakato wa kawaida kwa biashara, mtu au taasisi zinazopitia hali ngumu kifedha!

Kampuni zinapo-file bankruptcy mahakamani (chapter 11 protection) ina maana haziwezi kulipa madeni yake kwahiyo zinauza assets ili kulipa madeni na kuanza upya au kusuka upya deal la kulipa madeni (restructuring debt) na sheria inayalinda makampuni hayo.

Madhara ya zoezi hili pamoja na mambo mengine ni kuongeza 'credit risk' kwa aliye-file, na kusababisha ugumu kupata mikopo mipya na kupata huduma au bidhaa kwa mkopo!

Kwahiyo ku-file bankruptcy kama Trump alivyofanya, ni mkakati mzuri tu na wa kawaida wa kulipa madeni katika 'corporate America'.
(c) Kwa roho mbaya hilo liko wazi kabisa: Ukiacha hiyo ya birther na ya McCain kutokumshukuru kwa mazishi ya kitaifa, angalau nadhani unalijua hili
Mazingira (circumstances) yanayozunguka hali fulani yanaweza kuhalalisha matumizi ya maneno makali.

Kwa mfano, hiyo link inazungumzia Trump kutumia maneno makali dhidi ya watu waliotuhumiwa kwa ubakaji. Trump aliguswa na kitendo cha kikatili cha kubakwa kwa mwanadada Trisha na hivyo kupelekea kusema anahitaji kurudishwa kwa hukumu ya kunyongwa hadi kufa (death penalty) New York dhidi ya waliohusika.

Jimbo la New York halina hukumu ya kunyongwa hadi kufa. Kama kuhitaji hukumu hiyo katika hali hiyo maana yake ni roho mbaya, basi watu wengi wana roho mbaya.

Kuna States 30 Marekani bado zinaruhusu hukumu ya kunyongwa hadi kufa. Tanzania bado kuna hukumu ya kunyongwa hadi kufa.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,101
2,000
Nimeangalia baadhi ya hizo unazoita 'uongo' kwenye hizo links mbili, na nimegundua kuna maneno mengi tu ambayo yametafsiriwa kimakosa kama uongo. Inawezekana sio kimakosa bali ni kwa makusudi kabisa ili kutimiza ajenda fulani.

Kama mtu anaorodhesha na kuweka kumbukumbu ya maneno ya uongo ya mtu mwingine, halafu katika mchakato huo na yeye anasema uongo, nadhani mtu huyo anakuwa sio wa kutegemewa kama chanzo cha taarifa.

Huo unaiota "utapeli" (fraud) ulithibitishwa mahakamani? Maana kama mtu ametapeliwa ana-file 'civil lawsuit'.

Bankruptcy ni mchakato wa kawaida kwa biashara, mtu au taasisi zinazopitia hali ngumu kifedha!

Kampuni zinapo-file bankruptcy mahakamani (Chapter 11 protection) ina maana haziwezi kulipa madeni yake kwahiyo zinauza assets ili kulipa madeni na kuanza upya au kusuka upya deal la kulipa madeni (restructuring debt) na sheria inayalinda makampuni hayo.

Madhara ya zoezi hili pamoja na mambo mengine ni kuongeza 'credit risk' kwa aliye-file, na kusababisha ugumu kupata mikopo mipya na kupata huduma au bidhaa kwa mkopo!

Kwahiyo ku-file bankruptcy kama Trump alivyofanya, ni mkakati mzuri tu na wa kawaida wa kulipa madeni katika 'corporate America'.

Mazingira (circumstances) yanayozunguka hali fulani yanaweza kuhalalisha matumizi ya maneno makali.

Kwa mfano, hiyo link inazungumzia Trump kutumia maneno makali dhidi ya watu waliotuhumiwa kwa ubakaji. Trump aliguswa na kitendo cha kikatili cha kubakwa kwa mwanadada Trisha na hivyo kupelekea kusema anahitaji kurudishwa kwa hukumu ya kunyongwa hadi kufa (death penalty) New York dhidi ya waliohusika.

Jimbo la New York hamna hukumu ya kunyongwa hadi kufa. Kama kuhitaji hukumu hiyo katika hali hiyo maana yake ni roho mbaya, basi watu wengi wana roho mbaya.

Kuna States 30 Marekani bado zinaruhusu hukumu ya kunyongwa hadi kufa. Tanzania bado kuna hukumu ya kunyongwa hadi kufa.
Hawa nao ni waongo
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,763
2,000
Mtu yeyote anayemani kuwa Trump ni smart lazima ana matatizo makubwa sana ya kiakili.
Huyo mtu hata akili ya kusoma sidhani kama alikuwa anayo na IQ yake sidhani kama inaitafuta hata 90, halafu eti kila siku kuwashambulia wasomi wanaomzidi akili kama Obama. Kama si pesa za babake zilizokuwa zikimkwamua kila alipobugi step na kuzama kwenye lindi la madeni katika maisha yake angebakia kuwa mhuni tu.
John McCain 'aliharibu sherehe' siku ile, Obamacare ingeshaondoka! Ndio maana Dems wanamsifia sana McCain.
Ukisoma comments za Kichuguu kwenye post #898 , za Nguruvi3 ndio kabisa yupo biased na anapanick sana! Mpo serious sana wakuu!
El Jefe, ushauri tu mdogo...ukivuliwa nguo unachutama. Trump alikuwa na House na Senate na kwa nini umemkazania tu marehemu John McCain na huwataji Republicans wengine waliokataa? Unawataja Democrats kuwa ndio wanamsifia John McCain, je Republicans wangapi wanamuunga mkono Trump katika kumponda John McCain...unaweza kuwataja?
 

El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
El Jefe, ushauri tu mdogo...ukivuliwa nguo unachutama. Trump alikuwa na House na Senate na kwa nini umemkazania tu marehemu John McCain na huwataji Republicans wengine waliokataa? Unawataja Democrats kuwa ndio wanamsifia John McCain, je Republicans wangapi wanamuunga mkono Trump katika kumponda John McCain...unaweza kuwataja?

Mag3 Namkazania McCain kwa sababu yeye alikuwa against Obamacare kwa mda mrefu, halafu siku ya kura akageuka! Hao akina Susan Collins na Murkowski sijawataja kwa sababu wao walitegemewa kupinga maana wanajulikana ni moderates.

Sijasema Republicans wanamuunga mkono Trump kumponda McCain, ila ni wazi hizi sifa anazopewa McCain na Dems ni kwa sababu ya ile kura yake. McCain na Trump walikuwa na 'issues' zao kwa mda mrefu.
 

El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
Hawa nao ni waongo
Wanavyozungumza ni kama tangazo fulani lililolipiwa kwa ajili ya maslahi fulani. Hata hivyo, kuna videos nyingi za watu binafsi wakitoa maoni yao.

Mkuu Kichuguu , Mueller ameshatoa hitimisho lake, kila mwananchi anaweza kuwa na maoni yake.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Yawezekana mnatetea upuuzi wa Trump ku'justify' ujinga unaoendelea kutendekea hapa nchini kwetu. I find it so hard to argue with some of you people; it is like you have eyes but can't see and you have ears but can't hear or listen.

Kuitawala Marekani si rahisi kama mnavyodhani...eti mtu, hata akiwa Rais, anaweza kuamka tu na kuanza kutoa kauli za ajabu ajabu na watu wakamnyamazia. The honeymoon will soon be over and somebody is in for a very rude awakening...

Marekani mambo hayaendi hivyo kama anavyofikiria
Nilikuwa napitia mabandiko ya nyuma nikaliona hili. JF inakumbukumbu kweli!
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Mkuu Nguruvi3, naomba nikukumbushe kidogo matango pori aliyotaka kutulisha kuhusu ACA au kwa lugha ya Republicans Obama Care, nanukuu;
Tofauti na alivyotabiri El Jefe, Obama Care bado ipo na Trump ni kweli hakuwa na mbadala lakini Democrats kwa kutetea Obama Care waliweza kuchukua House kwa ushindi mkubwa. Huyu jamaa ni wa kuachana naye, yaonekana anawapenda sana viongozi waongo, matapeli na wenye roho kuntu.
Mkuu , kuna tango pori la Trumpacare! kwik kwik kwik! tukaambiwa linafanyiwa reconciliation na lile la House, mbavu zangu jamani
Mi nilishaachana naye kitambo, nashkuru ana ni follow. Nikiandika anajibu!

Trumpcare oh my God. Rudi mabandiko kati ya 20 na 37 utakutana na kituko hicho! kwi kwi

Watu wakalishwa tango pori eti Obamacare itafutwa '' kwa single stroke'' ya Trump

Leo GOP hawataki kusikia kabisa mtu anagusa ObamaCare! Barr amejaribu kupeleka mahakamani, Republicans katika House wamemuonya

Trump mwenyewe anaogopa hasa katika pre existing condition ambayo ndiyo sehemu kubwa ya Obamacare. Wameihujumu sana lakini wameshindwa kwasababu ile ''pillar'' ya pre existing condition haiwezi kufumuliwa. Obamacare leo ni popular sana kuliko miaka 5 nyuma

Trump aliwalisha matango na wakafakamia kwa kuwaambia siku ya kwanza anafuta Obamacare. Hakujua imetengenezwa kwa utaratibu gani na inahitaji kura za namna gani

Ndivyo Trump anavyoamini kuwa impeachment ikitokea atakwenda SCOTUS! Can you believe that! kwamba, Rais wa Marekani anaamini impeachment inafutwa na SCOTUS

Trump akatupa tango jingine nalo ni la porini, kwamba anafuta nuclear deal ya Iran
Huwezi kuamini US ndiyo wanawaomba Iran warudi mezani!

Pompeo na Trump wanasema milango ipo wazi Iran warudi mezani. Rouhani anasema watarudi ikiwa nuclear deal ipo mezani

''Siasa za viunga vya DC hazitazamwi kwa jicho la Tanzania''
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,543
2,000
Obama alishawaambia wakitaka waibadilishe jina wafute kutoka neno Obamacare waipe jina lingine wakitaka.

Republicans walilishwa matango pori na Trump wakajaribu kuivuruga bila kuwa na mpango wowote mbadala mwisho wa sikuu wakakumbana na hasira za wananchi ambao ndio wanufaika wa Obamacare.
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,419
2,000
Trump ni aina ya viongozi ambao wametokea kwa wave ya populism inayoendelea duniani.

Ni viongozi wasio na 'clue' nini wanafanya ila wanaenda tu.

Kazi yao ni kuharibu kila wanachoshika.

Kuna kila dalili ya recesion inaikumba marekani.

Trade war na China ambayo haina faida itakuwa chanzo kimoja wapo.
Wakuu Kichuguu na Mag3 , kama lipo jambo Trump amefanikiwa ni kuifanya Republicans isiwe ile Rep bali Republicans ya Trumpism. Amewatisha sana

Ukimsikiliza Lindsey Graham wa iliyokuwa Amigo akiwa na McCain na Liberman utashangaa
Graham amebaki kuokota mipira ya golf Marla-lago akitetea hata upuuzi

Akina Ted Cruiz na Rubio wapo kimyaa kama wamenyeshewa mvua.
Walikuwa mwiba kwa Obama wakiongozwa na McConnel aliyetak Obama awe one term pres

Hakuna anyeongelea uchumi ulikuwa wapi hadi uka qualify nchi kuwa katika recession

Hakuna anyeongelea vigezo vyote vya uchumi wakati ule na sasa. Wote wamebaki na kauli moja '' robust economy''. Katika suala la uchumi Obama ndiye aliyetengeneza akapokea Trump

Wengi hawatambui kuwa recession haikuanzia na George Bush, ilianza wakati wa Reagan
Deregulations hasa taasisi za pesa ndizo zilizopelekea anguko la uchumi baada ya muda

Kuitoa GDP katika negative na kuipeleka positive territory kwa uchumi mkubwa kama wa US si jambo la usiku mmoja. Kujenga consumer confidence baada ya hasara si jambo la usiku mmoja
Kutengeneza ajira kwa miezi 74 continuous ndicho kigezo cha recession kumalizika

Mambo aliyofanya Obama taratibu yanajidhihiri na ndiyo maana anazidi kuwa maarufu

Obamacare: Hadi leo hakuna anyetueleza sera ya Trump ni ipi na iko wapi
Wamarekani wanagundua kufuata Obamacare ilikuwa mkenge kwasababu hawaoni mbadala

Nuclear deal: Trump alidhani Iran nuclear deal ilikuwa hovyo akaifuta mara moja.
Katika miaka 2 hajawa na mbadala wa deal hiyo.
Leo akiwa Switzeland Pompeo anasema US ipo tayari kujadiliana na Iran bila condition.
Hii maana yake tayari wamekwama wanataka kurudi kwa OB

TPP: Obama alikazania sana TPP si kwasababu ya uchumi, bali kwa kuelewa usalama wa Marekani unategemea uchumi. Hivyo, US kuwa kiranja wa TPP ilikuwa mbinu ya kumdhibiti Mchina. Trump akafuta mara moja, ingawa sasa anarudi kwa mlango wa nyuma akimtumia VP

Trade War: Vita ya uchumi na China inaendelea Trump akiwaaminisha wafuasi wake kuwa zile tariff anazowekea Wachina atakayelipa ni China na si Mmarekani kama ilivyokuwa ''wall-mexico''

Hapa Trump anaumiza Wamarekani maeneo mengi, kwanza, tariff zitalipiwa na consumers US

Pili, retaliation ya tariff inaathiri Wakulima wake wanaouza Soya na bidhaa nyingine China

Tatu, makampuni kama GMC yanayojitanua kibiashara China yatafunga shughuli kwasababu ya kushindwa competition katika price

Haya yote yanatokea kukiwa na suala jingine la debt. Kwamba, lazima debt ceiling iongezwe

Katika mazingira ya kawaida na hasa waliyokuwa wanamsakama nayo Obama, ilitegemewa Republicans wawe wakali katika trade kwani wao wanaamini free trade na si protectionism.

Walitakiwa wawe wakali katika debt kwani huamini udogo na matumizi kidogo

Kwavile iliyopo ni Trumpisim na si Republicans, kila kitu kimyaaa!

Na hilo pia linaeleza ya Mueller. Ukisoma historia waliosimamia katiba wakati wa Nixon na kumuondoa walikuwa Republicans, siyo hii ya Trumpism na Barr

Tusemezane
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,763
2,000
John McCain 'aliharibu sherehe' siku ile, Obamacare ingeshaondoka! Ndio maana Dems wanamsifia sana McCain.
Kwa hiyo John McCain ndiye aliyesababisha Democrats kutwaa Congress? Are you insinuating that the control of Congress depended solely on how John McCain voted! This is really very disingenuous of you El Jefe...shame on you! Remember before the 2018 elections the House had 247 Republicans and only 188 Democrats. After the elections it is the reverse; 241 - 194 all because of McCain!
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Kwa hiyo John McCain ndiye aliyesababisha Democrats kutwaa Congress? Are you insinuating that the control of Congress depended solely on how John McCain voted! This is really very disingenuous of you El Jefe...shame on you!
Remember before the 2018 elections the House had 247 Republicans and only 188 Democrats. After the elections it is the reverse; 241 - 194 all because of McCain!
Kilichotokea siku ile ni mambo mawili. Kwanza, McCain aliuliza uko wapi mbdala wa Obamacare kabla ya kutupa watu nje ya Obamacare? Pili, concern yake ni kuwa wakati wa kupitisha Obamacare Republicans mmoja au wawili waliunga mkono. McCain akasema hiyo si njia nzuri ya kuitisha mswada mkubwa unaochukua 6% ya Bajeti ya US. Ni lazima kuwe na at least concensus

Consensus alyotaka siyo ya Dems 100% au 25% ni kupata japo wachache ili mswada uwe bipartisan. Hilo lingesaidia kujenga hoja kuwa mswada ni Bipartisan mbele ya umma

Republicans wengi walimwelewa McCain lakini walikuwa na hofu na popularity ya Trump hasa katika Republicans. Walihofia akina Banon na jinsi walivyowaendea kombo GOP wote waliokataa kumuunga mkono Trump. Walijua nguvu ya Trump na kumpa benefit of doubt

Kwanini Republicans na Trump wanamlaumu McCain ili kuficha ukweli kuwa hawana mbdala wa Obamacare. Hakuna , narudia tena hakuna mtu aliyewahi kuona ''Trump care'' wakati wa kampeni, uchaguzi na hata Urais hadi leo hii

Hili ni kosa la Wamarekani kwa sehemu fulani na hasa media. Wagombea wote wa Urais , 15 Republicans na 2 Dems katika uchaguzi wa 2016 walikuwa na Healthcare platform isipokuwa Donald Trump peke yake. Trump aliachiwa kwasababu ya controversies zake na watu kuendekeza vitu vilivyowashtua kuliko platform. Hii ndiyo ilikuwa trick ya distractions

Kwasasa media na Wamarekani wanauliza, ikiwa Obamacare ni mbaya uko wapi mbdala wake? Nini sera za Trump katika medicare, pre existing conditions, insurance n.k.?

Trump anajua Healthcare ni mwiba, hivyo anawaaminisha watu ataacha pre existing condition
Kufanya hivyo ni kusema ataacha Obamacare kwani pre existing condition ndiyo nguzo ya Obamacare. Hivyo sasa anatumia DOJ kubomoa Obamacare

Jaribio hilo linakutana na upinzani mkali wa seneti na House. Kilichosababisha dhahma ya midterm election 2018 ni Obamacare.

Watu walichagua Dems ili kuhakikisha wanailinda Obama care.

Tayari maseneta na House wamemuonya Barr kuacha suala hilo kwani ni balaa mbele ya safari

Trump kwa kujua ugumu anasukuma mzigo kwa DOJ akisema hakubaliani na kuondoa pre existing condition. Yaani aidhinishe hoja ya DOJ halafu awakane !
Katika kupoteza hoja lazima amtubukize McCain ili mjadala uwe juu ya yeye kumsema marehemu. Hicho kinaitwa distractions, lakini sasa anagota! Watu wanahoji upo wapi mbdala?
 

El Jefe

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
293
500
Kwa hiyo John McCain ndiye aliyesababisha Democrats kutwaa Congress? Are you insinuating that the control of Congress depended solely on how John McCain voted! This is really very disingenuous of you El Jefe...shame on you! Remember before the 2018 elections the House had 247 Republicans and only 188 Democrats. After the elections it is the reverse; 241 - 194 all because of McCain!

First of all, Democrats didn't take control of Congress instead they took over the majority in the House of Representatives (The House).

Congress is bicameral comprising of the House and the Senate.

Secondly, are you insinuating that Republicans lost control of the House solely because of 'obamacare'?
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
MUELLER APEW A WITO WA BUNGE

Suala la Mueller na Russia bado linafukuta na kumpa wazimu Rais Trump kila uchao
Wikii hii kamati za sheria na usalama zimemwita kisheria mchunguzi Mueller kwenda ku testify

Wito huo ni walazima (subpoena) ukiwa ni mbele ya kamera kinyume na kujifungia vyumbani

Hilo ndilo kamati ilitaka litokee ingawa Mueller mwenyewe hakupenda kuepuka siasa

Rais Trump na WH hawana jinsi ya kumzuia kama walivyofanya kwa watu wengine akiwemo Mcgahn na Hope Hicks aliyekwenda na kukataa kujibu baadhi ya maswali

Mueller ni Raia huru na immunity yoyote haimhusu

Wapo wanaojiuliza kuna kitu gani kipya zaidi watarajie kutoka kwa Mueller?

Uwepo wake utafikisha ujumbe kuhusu taarifa yake na kujibu maswali yanayojitokeza

Baadhi ya hayo ni upotoshaji AG Barr aliamua kuyageuza kwa tafsiri yake.
Mathalan suala la ''collusion'' dhidi ya criminal conspiracy
Kwanini kama hawakuweza kumsafisha Rais pia hawakuweza kumshtaki

Majibu yake yatatatua utata na kitendawili ndani ya taarifa

Rais Trump kama kawaida kaanza kwa kumshambulia.
Hii si mara ya kwanza, Trump amemshambulia Mueller bila ushahidi wa aina yoyote

Wakati huo huo anatumia taarifa hiyo kudai imemsafisha

Wachunguzi wa mambo wanamuona Trump kama anachezea ndevu za Simba.

Ikiwa Mueller atabadilika na kujibu mapigo kinyume na taaluma, huo ndio utakuwa mwisho wa Urais wa Trump. Mueller anaweza kusema maneno matatu tu historia ikajirudia kwa Nixon

Hata hivyo frustration za Trump zina maana kubwa. Kwanza, jitihada zake za kuwazuia watu wasitoe ushahidi zinazidi kukwama mahakamani, na hajaweza kumuzia mtu kama Mueller

Tarehe 17 inaweza kuwa na matokeo mawili, kwanza, kumsafisha Trump once and for all
Pili, kumtia katika matatizo makubwa sana ya impeachment.

Haya ya Mueller si habari njema hata kidogo, ni upanga wenye ncha mbili

Tusemezane
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,101
2,000
===
Na huyu jaji yupo upande wa Trump!? Na kweli hoja zake hazina mashiko !?
Kwani umesoma hiyo ruling ya Judge kweli au umesoma maoni ya mwandishi huyo wa Russian Times. Ruling yenyewe ni hii hapa; je kweli ukiiisoma utahitimisha kuwa "Federal judge destroys key Mueller report claim'?

Kama huwezi kusoma ruling yote, summary yake unaweza kuipata hapa
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
VIUNGANI DC
MUELLER KWENDA KAMATI ZA BUNGENI
TRUMP NA CONGRESSWOMEN, NJIA YA KUBADILI MAWAZO YA UMMA

Mueller anatarajiwa kurudi katika kamati mbili za Bunge kutetea taarifa yake
Mueller ameitwa kwa wito ''subpoena' na akiwa afisa mwandamizi wa idara ya FBI ametii wito

Kwa tabia na hulka, Mueller hapendi kuwa katikati ya timbwili linaloendelea akisema taarifa yake inajieleza na wala hataki iwe suala la siasa.
Ni ngumu sana kufahamu ikiwa Mueller ataeleza chochote cha ziada atakapohojiwa

DOJ imetoa taarifa ikimtaka abaki ndani ya taarifa yake ikichelea kuwa Mueller akienda ''kombo' hilo linaweza kubadili mwelekeo wa maongezi katika viunga vya DC na upepo mbaya kuvuma

Kurejea kwa Mueller kunaonekana kumsumbua Rais Trump ambaye licha ya kumshambulia kwa hoja za uongo, maelezo ya Trump yana upotoshaji wa makusudi

Trump anadai Mueller alimuomba kazi ya FBI na kumkatalia siku moja kabla ya kuteuliwa kuwa mchunguzi. Ukweli ni kuwa aliyemwalika Mueller WH ni Trump na wala si kwa kazi ya FBI
Swali hilo likizuka, linaweza kuwa na majibu yatakayofedhehesha

Yapo mengi katika taarifa kama obstruction of justice, na kwamba hakukuwepo na ushahidi wa kutosha kuhusu collusion. Haya nayo yakitolewa majibu yanaweza kubadilisha uelekeo hasa yakipata ufafanunuzi.

Katika hali ya taharuki, Rais Trump ameshambuliwa Wabunge 4 wa rangi wanaojiita ''squad''
Hawa squad wamekuwa mwiba hata kwa Democrat na ilikuwa suala la muda tu wangeleta tatizo

Majuzi walimshambulia Spika Pelosi, wengine wakitoa kauli zenye utata kuhusu Israeli
Hali hiyo imempa Trump silaha ya kuwashambulia ingawa lengo ni kuondoa watu kutoka Mueller

Kama Wabunge hao ''wanaichukia Marekani' asemavyo Trump, basi yeye aliichukia kabla yao
Kwa kufuatilia kauli zilizotolewa, Wabunge walikosoa sera jambo na si kuitukana Marekani

Huyu ni mtu aliyeitukana sana Marekani, serikali ya Obama na Obama mwenyewe
Leo amekuwa mtu mzuri sana wa kuitetea Marekani

Kitendo cha kuwataka ''warudi makwao'' kimezua hoja nzito katika mijadala
Inaweza kuwa ni kikundi cha watu wake kinachoona sahihi lakini Republicans wana wakati mgumu wa kutetea ubaguzi. Hofu kubwa ni kutorudisha House mikononi mwao

Karata za Trump ni kucheza na base yake ambayo kwa sehemu kubwa ni ya kibaguzi'' racist'
Lakini hilo lina faida na hasara zake. Kuwagawa watu kwa rangi kuna faida kwavile watu weupe ni wengi. Hata hivyo, kwa hesabu kunapunguza wale ''moderate'' waliompa ushindi 2016

Kwahivyo karata anayocheza ina sehemu mbili, ya muda mfupi na mrefu.
Mwakani atalazimika sana kutafuta moderate hasa sehemu kama Michigan, Wisconsin n.k.

Kwa hali yoyote, mahojiano ya Mueller yanaweza kurudisha mjadala wa Russia kuwa mbichi

Tusemezane
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,040
2,000
Nadhani utafutaji " mchawi" umekwisha...hasa ule ulionzishwa na Demo baada ya kipigo cha HRC.
===

A federal judge in frank terms Tuesday dismissed a lawsuit by the Democratic National Committee (DNC) against key members of the Trump campaign and WikiLeaks over hacked DNC documents, saying they "did not participate in any wrongdoing in obtaining the materials in the first place" and therefore bore no legal liability for disseminating the information.
The ruling came as Democrats increasingly have sought to tie the Trump team to illegal activity in Russia, in spite of former Special Counsel Robert Mueller's findings that the campaign in fact refused multiple offers by Russians to involve them in hacking and disinformation efforts.
President Trump, in a tweet late Tuesday, noted that the judge in the case, John Koeltl, was appointed by Bill Clinton. The president called Koeltl's decision "really big 'stuff'" and "yet another total & complete vindication and exoneration."
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,763
2,000
Nadhani utafutaji " mchawi" umekwisha...hasa ule ulionzishwa na Demo baada ya kipigo cha HRC.
===
Ha ha haa TUJITEGEMEE, utaokotezaokoteza hizi spin za RT News hadi lini? Je, did not participate in any wrongdoing in obtaining the materials in the first place, unaelewa maana yake? Kwa ufahamisho ni kweli kabisa kwamba hao watajwa hawakuhusika katika ku-obtain the materials in the first place kwani wahusika hasa wa hilo walikuwa ni Warusi, over?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom