Mfamaji
JF-Expert Member
- Nov 6, 2007
- 6,629
- 1,951
haya maswali yote yanatokana na kwamba bibadamu tumeshindwa kuukubali ukweli mchungu kuhusu kifo, ndio maana tunatengeneza nadharia kibao za kufikirika ili kujifariji kuwa kuna cha zaidi baada ya kifo.
lakini ukweli unabaki palepale, binadamu ni myama kama wanyama wengine, kabla ya kuzaliwa haukuwepo kabisa, kuwa conscious kuwa wewe ni wewe haipo kwa binadamu pekee hata sokwe na tembo wanahuo uwezo. baada ya kifo it's over!
N.B ushauri wangu,
usivumilie upuuzi na dhiki duniani kwa kujipa moyo kuwa utaenda "kula bata" baada ya kifo, haya ndio maisha yako pekee hivyo basi jaribu kuhakikisha you get the best out of it. Nchi nyingi masikini zinaendelea kuoza kwenye umasikini na siasa za hovyo kwakuwa watu wake hawaoni umuhimu wa kupambana kubali hali kwani wanaamini wataenda "kupumzika" paradiso/peponi. Haya ni mawazo ya kikoloni yaliyoletwa na wanyonyaji wetu ili wao wafaidi maisha wakati sisi tunangojea kufaidi baada ya kifo.
Wewe ni mmoja wa wale wenye karma ya kijinga ya kuamini amini tu. Kuamini kuwa wewe ni kama sokwe na ukifa its over na kuamini kuwa Mungu ndiye aliyekuumba tumboni mwa mama yako, hatuwezi kukubadili maana ni karma yako, tena ni laana.
Kwa hiyo hata tukienda hatua nyingine tukakuambia kuwa Mungu unayemfahamu wewe haumbi tena kama alivyofanya kwa Adam ha Hawa si utashaangaa kufa na kusema tunamkufuru Mungu?
Au ukiambiwa unalowaza, tayari kuna milions of people wanawaza kitu hicho hicho si utabisha tu kama jiwe? Sasa hii inaitwa TOTAL MIND, au universal mind kwamba sisi wote tuko connected kwa sababu ni roho moja yenye vipande vingi vikakaa kwa kila mmoja wetu utakubali vipi wakati ndio wale wa kusema tu ndioooooo......soma kitu kinaitwa omnipotent, omniscient and onmipresent.
Hebu kubali tu kwamba reicarnation sio myth, bali ni uhalisia. Sio kama tukifa tuaenda kula bata hapana. Tutakuwa kwenye bliss ..yaani raha ya milele au tutakuwa kwenye mateso milele. Maana yake ni kuwa kwa mfano kama una jambo linokusumbua , kinachosusumbuka ni conciuous mind yako ambayo itaiaminisha unconscious mind yako ambayo huwezi itenganisha na roho yako. Roho italibeba lilivyo na ukifa kabla ya kusolve huo usumbufu ukizaliwa tena utaendelea kusumbuka kwa jambo hilo hilo hadi utatue.
Hebu waza ni kwa nini kuna watu wanapenda kuwa wanamuziki wakati wengine hawataki hata kusikia, na hao wanaopenda wanaamini tu kuwa ukiwa mwanamuziki utakuwa tajiri. Kiuhalisia sio kweli, lakini atafanya tu kwa sababu maisha ya mwanzo alikuwa akihangaikia hilo na hakupata, sasa anaendelea kusaka hadi kieleweke. Hii ndio karma. Kuna mifano mingi tu tuayoshuhudia hata kwa familia zetu, na kwa taarifa ni kwamba ukifa sio lazima ukazaliwe tena ulaya , au jirani, unawewa kuzaliwa kwenye ukoo au familia hiyo hiyo na hii haitokei kwa muda mfupi. Yaweza kuchukua hata miaka 20-50. Ila kwa sababu ya ubishi utasema ni genetic. Ukiwa na nafasi nitakueleza tofauti ya genetic na Karma bure kama shule za magufuli