Dunia ni gereza la roho za wafu

Dunia ni gereza la roho za wafu

haya maswali yote yanatokana na kwamba bibadamu tumeshindwa kuukubali ukweli mchungu kuhusu kifo, ndio maana tunatengeneza nadharia kibao za kufikirika ili kujifariji kuwa kuna cha zaidi baada ya kifo.
lakini ukweli unabaki palepale, binadamu ni myama kama wanyama wengine, kabla ya kuzaliwa haukuwepo kabisa, kuwa conscious kuwa wewe ni wewe haipo kwa binadamu pekee hata sokwe na tembo wanahuo uwezo. baada ya kifo it's over!

N.B ushauri wangu,
usivumilie upuuzi na dhiki duniani kwa kujipa moyo kuwa utaenda "kula bata" baada ya kifo, haya ndio maisha yako pekee hivyo basi jaribu kuhakikisha you get the best out of it. Nchi nyingi masikini zinaendelea kuoza kwenye umasikini na siasa za hovyo kwakuwa watu wake hawaoni umuhimu wa kupambana kubali hali kwani wanaamini wataenda "kupumzika" paradiso/peponi. Haya ni mawazo ya kikoloni yaliyoletwa na wanyonyaji wetu ili wao wafaidi maisha wakati sisi tunangojea kufaidi baada ya kifo.
Mkuu unaweza ukaniambia ulikuwa wapi kabla ya kuzaliwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binadamu huzaliwa, hukua, na hufa. Lakini binadamu huyu huzaliwa pasipo ufahamu wa chanzo chake na kuvaa umbo la mwili lililotengenezwa kwa yai la mama na mbegu ya baba.

Kabla hatujaendelea na uchambuzi wa mada, unaweza kujiuliza maswali yafuatayo ;

Je, kabla ya kuzaliwa ulikuwa wapi?

Je, ni kitu gani kinakufanya ujisikia kuwa wewe ni wewe?

Je, kwanini hauhisi kwamba wewe sio yule mwingine, lakini wewe ni wewe?

Kitu gani kinakufanya kuwa wewe?

Je, wewe ni nani? Wewe ni mwili? wewe ni hisia ya kujisikia kuwa wewe ni wewe?

Je, ukifa, wewe unakwenda wapi?

Je, maiti yako ni wewe?

Baada ya maswali machache ya falsafa juu ya chanzo cha binadamu, tunabaini kuwa, binadamu ni viumbe wanaozaliwa na kufa, na huzaliwa tena na tena katika namna tofauti, miili tofauti, na maeneo tofauti katika mchakato uitwao incarnation.

Mwili wa binadamu unapokufa, nguvu au nafsi hai inatoka ndani ya mwili na kupitia mchakato mpya wa kutafuta makazi ndani ya mwili mwingine.

Nafsi zetu zimefungwa na adhabu endelevu ya karma ambayo inatufanya tuyalipe matendo yetu katika miili mipya baada ya kufa na kuzaliwa upya.

Baada ya kufa, nafsi yako itachagua maisha ambayo yatakulipa kisasi ama yatakurudishia wema kwa kadiri ya maisha yako kabla ya kifo. Kama ulikuwa muuaji katika maisha ya mwanzo, basi baada ya kuzaliwa upya nafsi yako itachagua maisha ya mtu mpya mwenye hali ya unyonge ili kusudi uadhibiwe kwa kisasi kile kile cha mauaji.

Vivyo hivyo, maisha ya sasa ya mtu mnyonge yatalipwa kwa wema na furaha katika maisha yajayo ndani ya mwili mpya.

Hii ndio dhana ya karma, ambayo huenda ina uhusiano wa moja kwa moja na mafundisho ya mbingu na jehanamu. Ama msemo wa wahenga usemao " malipo ni hapa hapa duniani" . Kimsingi, nafsi zetu zinachukua miili mipya kulipa karma kwa kadiri ya matendo yetu.

Incarnation inapotokea, nafsi yako inakuwa imeshafahamu maisha yako yote yajayo katika mwili mpya, na hivyo kukufanya upitie hatua zote za hatma yako. (destination).

Mchakato huu, unahusiana moja kwa moja na kitu kinachoitwa DEJAVU, yaani kumbukizi zinazompata mtu ghafla na kutambua kuwa anafanya mambo ambayo alishakwisha kuyafanya.

Kumbukumbu hizi za DEJAVU zinatupa taarifa kuwa maisha yetu yalishachorwa na nafsi zetu kabla hatujaja duniani. Huu ni ufunuzi wa kiroho unaotukumbusha kuwa tunapitia mambo ambayo yalishakwisha kuonwa na kupangiliwa.

Binadamu ni roho zilizotekwa ndani ya gereza la dunia, na ni roho ambazo zitaendelea kuja tena na tena katika miili tofauti ili kulipa KARMA na ku-experience maisha mapya tofauti na yale kabla ya kifo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna ukweli hapo,
hakuna mahusiano Kati ya waliopo hai na waliokufa , hizo ni porojo kama zingine hakuna cha dajavu wala reicnation

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waafrika hatuko tayari kujifunza vitu vipya na ndio maana hadi leo tumebaki nyuma sana! Hili jambo hata wapigania haki za mtu mweusi kule Ughaibuni linawakatisha sana tamaa. Mimi hiki naona kama ni Kilema na Laana!
Na hiki ni kilema kikubwa Mungu aliumba viumbe vingi, Vinavyoonekena na Visivyoonekana na akampa mamlaka Binadamu avitawale.........Lakini wapiiiiii....Bhana ukimuuliza mwanadamu unatawala kiumbe gani kisichoonekana.....???? hana la kusema.....Bure kabisaaaaa.....!!!!
 
inawezekana kabisa ni karma na inawezekana pia kabla ya kifo chako uliishi maisha ya kifahari dunia nyingine au bara lingine, na kwamba nafsi yako ilinuia ku-experience maisha ya ufukara katika mwili mpya.

Hauwezi kufahamu kuwa uliishi maana memory yako inafutwa kabisa kukuwezesha kuishi maisha mapya bila marue rue ya kale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua ili mtu aweze kuthibisha au kuamini kile unachokisema au unachokiandika lazima uwe na chanzo. Je ni mwazo yako binafsi au umejifunza sehemu na kama umejifunza naomba kujua vyanzo vya elimu hii?

Hii ni elimu inayotokana na tafakari ya kina ya mtu binafsi (self reflection) pamoja na kutizama mambo katika ulimwengu wa kufikirika. Lakini ni kweli, ni elimu inayopatikana vitabuni pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haya maswali yote yanatokana na kwamba bibadamu tumeshindwa kuukubali ukweli mchungu kuhusu kifo, ndio maana tunatengeneza nadharia kibao za kufikirika ili kujifariji kuwa kuna cha zaidi baada ya kifo.
lakini ukweli unabaki palepale, binadamu ni myama kama wanyama wengine, kabla ya kuzaliwa haukuwepo kabisa, kuwa conscious kuwa wewe ni wewe haipo kwa binadamu pekee hata sokwe na tembo wanahuo uwezo. baada ya kifo it's over!

N.B ushauri wangu,
usivumilie upuuzi na dhiki duniani kwa kujipa moyo kuwa utaenda "kula bata" baada ya kifo, haya ndio maisha yako pekee hivyo basi jaribu kuhakikisha you get the best out of it. Nchi nyingi masikini zinaendelea kuoza kwenye umasikini na siasa za hovyo kwakuwa watu wake hawaoni umuhimu wa kupambana kubali hali kwani wanaamini wataenda "kupumzika" paradiso/peponi. Haya ni mawazo ya kikoloni yaliyoletwa na wanyonyaji wetu ili wao wafaidi maisha wakati sisi tunangojea kufaidi baada ya kifo.

Hujui uwazalo katika ulimwengu wa Roho hakuna hilo

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna siku nilikua katika mji Fulani sio tz sasa nilikua na shida fulani ya kunua bidhaa..basi ilinijia wazo linasema pita pale utakuta upande wapili na kweli nikafanya hivyo upande wa pili nikaikuta direct hio shop na mim nilikua mgeni kabisa ndio Mara yangu ya kwanza katika huo mji...nilishangaa sana hadi Leo sielewi
 
Huo ni ufunuo wa Deja'Vu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii inaitwa Deja'Vu. Unafanya jambo ambalo unahisi kabisa ulishawahi kuliona unalifanya katika namna ile ile.

Hapo nafsi yako inakufunulia kuwa, maisha yako yalishachorwa na kupangiliwa kabla haujazaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Niko safarini sasa juzi nilifika mahali nikawa natafuta sehemu ya kulala nikakosa.. Nikampigia rafiki yangu akanielekeza mahali pengine
Hapo mahali sijawahi kufika, lakini nilipofika nikakumbuka nilishawahi kufika but kwa njia ya ndoto.. Very vivid memory... Ndoto yote ilikuja kama vile ndio siku hiyo

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom