Ambokile Amanzi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 961
- 1,333
Binadamu huzaliwa, hukua, na hufa. Lakini binadamu huyu huzaliwa pasipo ufahamu wa chanzo chake na kuvaa umbo la mwili lililotengenezwa kwa yai la mama na mbegu ya baba.
Kabla hatujaendelea na uchambuzi wa mada, unaweza kujiuliza maswali yafuatayo ;
Je, kabla ya kuzaliwa ulikuwa wapi?
Je, ni kitu gani kinakufanya uhisi kuwa wewe ni wewe?
Je, kwanini hauhisi kwamba wewe sio yule mwingine, lakini wewe ni wewe?
Kitu gani kinakufanya kuwa wewe?
Je, wewe ni nani? Wewe ni mwili? wewe ni hisia ya kujisikia kuwa wewe ni wewe?
Je, ukifa, wewe unakwenda wapi?
Je, maiti yako ni wewe?
Baada ya maswali machache ya falsafa juu ya chanzo cha binadamu, tunabaini kuwa, binadamu ni viumbe wanaozaliwa na kufa, na huzaliwa tena na tena katika namna tofauti, miili tofauti, na maeneo tofauti katika mchakato uitwao incarnation.
Mwili wa binadamu unapokufa, nguvu au nafsi hai inatoka ndani ya mwili na kupitia mchakato mpya wa kutafuta makazi ndani ya mwili mwingine.
Nafsi zetu zimefungwa na adhabu endelevu ya karma ambayo inatufanya tuyalipe matendo yetu katika miili mipya baada ya kufa na kuzaliwa upya.
Baada ya kufa, nafsi yako itachagua maisha ambayo yatakulipa kisasi ama yatakurudishia wema kwa kadiri ya maisha yako kabla ya kifo. Kama ulikuwa muuaji katika maisha ya mwanzo, basi baada ya kuzaliwa upya nafsi yako itachagua maisha ya mtu mpya mwenye hali ya unyonge ili kusudi uadhibiwe kwa kisasi kile kile cha mauaji.
Vivyo hivyo, maisha ya sasa ya mtu mnyonge yatalipwa kwa wema na furaha katika maisha yajayo ndani ya mwili mpya.
Hii ndio dhana ya karma, ambayo huenda ina uhusiano wa moja kwa moja na mafundisho ya mbingu na jehanamu. Ama msemo wa wahenga usemao " malipo ni hapa hapa duniani" . Kimsingi, nafsi zetu zinachukua miili mipya kulipa karma kwa kadiri ya matendo yetu.
Incarnation inapotokea, nafsi yako inakuwa imeshafahamu maisha yako yote yajayo katika mwili mpya, na hivyo kukufanya upitie hatua zote za hatma yako. (destination).
Mchakato huu, unahusiana moja kwa moja na kitu kinachoitwa DEJA'VU, yaani kumbukizi zinazompata mtu ghafla na kutambua kuwa anafanya mambo ambayo alishakwisha kuyafanya.
Kumbukumbu hizi za DEJA'VU zinatupa taarifa kuwa maisha yetu yalishachorwa na nafsi zetu kabla hatujaja duniani. Huu ni ufunuzi wa kiroho unaotukumbusha kuwa tunapitia mambo ambayo yalishakwisha kuonwa na kupangiliwa.
Binadamu ni roho zilizotekwa ndani ya gereza la dunia, na ni roho ambazo zitaendelea kuja tena na tena katika miili tofauti ili kulipa KARMA na ku-experience maisha mapya tofauti na yale kabla ya kifo.
Sent using Jamii Forums mobile app