Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,360
- 11,588
Naomba niandike kwa ufupi
Kitendo cha wewe kujijua ni wewe, kulitambua jina lako, kuutambua vyema mwili wako, kipi unapenda na kipi hupendi, huyo ni nafsi wako mkuu, na huyo ndio wewe, kama utasimama kama wewe, kila jambo utakaloliamua kulitimiza, utalitimiza muda huo huo pasi na mashaka wala subira
Umewahi kutazamia kufanya jambo ambalo moyo wako kuna namna unakuzuia usilifanye? Labda kwa kudhania lingekuletea hatari mbeleni? Baadae ama siku za usoni? Labda kuna mwamba kakuudhi ie.
Katembea na mpenzi wako, unachukua silaha na kuitia kibindoni kwa lengo la kwenda kumshambulia, inatokea nafsi inakwambia achana naye, wala usisogelee malangoni pake, kwa sababu kwa kufanya hivyo, utaua na itakupelekea kwenda jela, na kama utaenda, nani atawatunza wanao?" unaghairi unaamua kumuachia Mungu. Huyo ni wewe katika nafsi ya pili
Wewe katika nafsi ya pili ndiye unaoufahamu mzunguko mzima wa maisha yako, jamii inayokuzunguka, pia sheria na taratibu zilizowekwa, huyo ndiye wasiwasi wako ndio akili, daima anajitokeza katika "kufikiri" (Reasoning)
Nina imani kila mmoja wetu hapa amewahi kuota ndoto, yule "wewe hapo" ndani ya ndoto ndiwe nafsi ya tatu
Ili kukuonesha kuwa hujui, fanya kufikiria haya:
• Hivi ukiwa unaota ndoto, unajiona ndotoni?
• Hakuna binadamu anayeota sura mpya ambazo hajawahi kuonana nazo, je hao unaowaota pasi na kuwafahamu wametoka wapi?
• Hivi umewahi kuota ndoto yenye rangi?
• Kikawaida ndoto haina maumivu ya mwili, hakuna ndoto ambayo umewahi kuota labda unaadhibiwa na ukahisi maumivu?
• Umewahi kukwama ndotoni? Unajua ni kwanini?
• Umewahi kujua kuwa hapa ninaota?
• Umewahi kuota ndoto za kujirudia rudia, labda uko shule, ama safarini. Unahisi ni kwanini?
• Kwanini ukiamka asubuhi hukumbuki ulichoota, cha ajabu mchana ama jioni ndo unakumbuka
• Na ni kwanini ukiwa mgonjwa ama mwenye maumivu ukijitibia ukiwa ndotoni unapata ahueni baada ya kuamka?
• Huenda juzi unayoifikiria haikuwepo, bali yote ilikuwa ni ndoto. Unaamini hilo?
Ndoto "wewe katika nafsi ya tatu" ipo kwa lengo la kukusumbua ili ukamilishe mipango ambayo inajua wazi ni muhimu itimie ili nafsi ya pili ibaki ikiwa imesuuzika
Tuishie hapo!