Dunia ni gereza la roho za wafu

Dunia ni gereza la roho za wafu

Kun
Binadamu huzaliwa, hukua, na hufa. Lakini binadamu huyu huzaliwa pasipo ufahamu wa chanzo chake na kuvaa umbo la mwili lililotengenezwa kwa yai la mama na mbegu ya baba.

Kabla hatujaendelea na uchambuzi wa mada, unaweza kujiuliza maswali yafuatayo ;

Je, kabla ya kuzaliwa ulikuwa wapi?

Je, ni kitu gani kinakufanya uhisi kuwa wewe ni wewe?

Je, kwanini hauhisi kwamba wewe sio yule mwingine, lakini wewe ni wewe?

Kitu gani kinakufanya kuwa wewe?

Je, wewe ni nani? Wewe ni mwili? wewe ni hisia ya kujisikia kuwa wewe ni wewe?

Je, ukifa, wewe unakwenda wapi?

Je, maiti yako ni wewe?

Baada ya maswali machache ya falsafa juu ya chanzo cha binadamu, tunabaini kuwa, binadamu ni viumbe wanaozaliwa na kufa, na huzaliwa tena na tena katika namna tofauti, miili tofauti, na maeneo tofauti katika mchakato uitwao incarnation.

Mwili wa binadamu unapokufa, nguvu au nafsi hai inatoka ndani ya mwili na kupitia mchakato mpya wa kutafuta makazi ndani ya mwili mwingine.

Nafsi zetu zimefungwa na adhabu endelevu ya karma ambayo inatufanya tuyalipe matendo yetu katika miili mipya baada ya kufa na kuzaliwa upya.

Baada ya kufa, nafsi yako itachagua maisha ambayo yatakulipa kisasi ama yatakurudishia wema kwa kadiri ya maisha yako kabla ya kifo. Kama ulikuwa muuaji katika maisha ya mwanzo, basi baada ya kuzaliwa upya nafsi yako itachagua maisha ya mtu mpya mwenye hali ya unyonge ili kusudi uadhibiwe kwa kisasi kile kile cha mauaji.

Vivyo hivyo, maisha ya sasa ya mtu mnyonge yatalipwa kwa wema na furaha katika maisha yajayo ndani ya mwili mpya.

Hii ndio dhana ya karma, ambayo huenda ina uhusiano wa moja kwa moja na mafundisho ya mbingu na jehanamu. Ama msemo wa wahenga usemao " malipo ni hapa hapa duniani" . Kimsingi, nafsi zetu zinachukua miili mipya kulipa karma kwa kadiri ya matendo yetu.

Incarnation inapotokea, nafsi yako inakuwa imeshafahamu maisha yako yote yajayo katika mwili mpya, na hivyo kukufanya upitie hatua zote za hatma yako. (destination).

Mchakato huu, unahusiana moja kwa moja na kitu kinachoitwa DEJA'VU, yaani kumbukizi zinazompata mtu ghafla na kutambua kuwa anafanya mambo ambayo alishakwisha kuyafanya.

Kumbukumbu hizi za DEJA'VU zinatupa taarifa kuwa maisha yetu yalishachorwa na nafsi zetu kabla hatujaja duniani. Huu ni ufunuzi wa kiroho unaotukumbusha kuwa tunapitia mambo ambayo yalishakwisha kuonwa na kupangiliwa.

Binadamu ni roho zilizotekwa ndani ya gereza la dunia, na ni roho ambazo zitaendelea kuja tena na tena katika miili tofauti ili kulipa KARMA na ku-experience maisha mapya tofauti na yale kabla ya kifo.

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna kasoro nyingi ktk hii falsafa.Swali , hiyo kalma ilianza lini na itaisha lini.hizo nafsi ziliumbwa na nani? Hizo nafsi zinauhusiano na kabila rangi nk.İli nafsi zijifunze kutokana na makosa kwa nini zisiwe na kumbukumbu ya maisha ya nyuma, Hizo dhambi(ubaya) ni zipi? Maana dhambi sehemu moja inaweza isiwe dhambi sehemu nyingine Maswali ni mengi bora niishie hapa.
 
Kumbukumbu halisi za kabla ya kifo chako zinafutika kabisa na huwezi kujua lolote.

Lakini kuna namna ya kubaini mambo uliyokuwa unafanya kabla ya kifo. Tafakari ni mambo gani unapenda sana kufanya sasa hivi, au tafakari ni vitu gani unavifanya kwa uwezo mkubwa kuliko kawaida.

Huenda ndio mambo uliyokuwa unayafanya katika maisha yako kabla ya kifo, na kwamba nafsi yako inakufunulia na kukuvuta nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
"Huenda ndio mambo ".............
Hiyo sentensi wewe mwenyewe una walakini,means huna uhakika,sasa hapa sioni uhalisia wa hiyo "incarnation" maana ingekuwa na faida kama tungeweza kuwa na kumbukumbu ya matukio hayo na ujue unawajibika na iyo "karma" baada ya kifo chako cha awali....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Huenda ndio mambo ".............
Hiyo sentensi wewe mwenyewe una walakini,means huna uhakika,sasa hapa sioni uhalisia wa hiyo "incarnation" maana ingekuwa na faida kama tungeweza kuwa na kumbukumbu ya matukio hayo na ujue unawajibika na iyo "karma" baada ya kifo chako cha awali....

Sent using Jamii Forums mobile app
Fuatilia post za juu hapo nimeeeleza ni kwa namna gani mtu anaweza kukumbuka maisha yake ya nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kun

kuna kasoro nyingi ktk hii falsafa.Swali , hiyo kalma ilianza lini na itaisha lini.hizo nafsi ziliumbwa na nani? Hizo nafsi zinauhusiano na kabila rangi nk.İli nafsi zijifunze kutokana na makosa kwa nini zisiwe na kumbukumbu ya maisha ya nyuma, Hizo dhambi(ubaya) ni zipi? Maana dhambi sehemu moja inaweza isiwe dhambi sehemu nyingine Maswali ni mengi bora niishie hapa.
Sifahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda kuna nafsi mpya katika miili mipya. Lakini nafsi za kale hazifi na zitaendelea kurudi na kurudi katika miili mipya!
si kweli, kila kiumbe huja duniani kikiwa timilifu kwa maana mwili roho na nafsi vipya. kwa nini nasema hivi?

jiulize miaka 50 nyuma popolution ya watu duniani ilikuwa ni chini ya nusu ya ilivyo sasa. Sasa kwa hii idadi iliyoongezeka je nafsi ama roho zao zimetoka wapi??

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachofikiri ni kuwa huenda kuna nafsi mpya katika miili mipya. Lakini nafsi za kale hazifi.
Natanguliza shukuruni kwa wana JF,
Huu mtazamo wa MR/MRS Ambokile Amanzi siku moja mwaka 2018 niliupata kuuona katika sizoni moja hivi jina limenitoka kidogo ila nakumbuka mwishoni wanamalizia na WHITE SNAKE,
kulikuwa na wahusika wawili ambao walikuwa wapenzi huko nyuma na baadae wakazaliwa upya na wakatupwa mabara tofauti ila mwishowe walikuwa katika mahusiano tena ya kimapenzi ndipo kila ambacho walikuwa wanakifanya wakahisi kama walishawahi kufanya huko nyuma labda ndiko amepata elimu hii aloiweka mezani,

Mtazamo wangu, mimi hainiingii akilini hata kidogo kutokana na mfululizo wa maswali ambayo yanakimbiana na Dhana au Wazo la mtoa mada,

1, je binadam wa kwanza alipewa roho ya nani? Ikiwa yeye ni first of the all.

2, Incase of Population dhana au wazo hili linakosa mashiko kwa kuwa idadi ya watu sasa hivi ni kubwa tofauti na huko nyuma, jee unataka kuniambia roho moja inapandikizwa kwa mtu zaidi ya mmoja?
nawapongeza wale walochangia kuhusu idadi ya watu kama hoja yao...

3, suala la umri, ni wazi kuwa zamani watu walikuwa na uwezo wa kuishi hadi miaka 300 nk tofauti na zama za sasa, jee unawezaje kuishi kwa kipindi kifupi cha miaka 40 na ukayafanya yale ya nyuma yaani kinyume chake mfano; mwizi kuwa Mwema?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom