Kaka hivi hizi kauli unaziegemeza kwa nani ? Maana naona kama unampangia Allah cha kufanya.
Unaweza kuniambia ni mwanachuoni gani aliyekitangulia katika kauli hizi,ili nimsome yeye maana naona unazidi kukosea na kukaa mbali na ukweki.
Naomba unitajie jina la mwanachuoni aliye kitangulia katika hizi kauli zako.
ni ayagani Allah kajisifia ufundi wa kuumba alafu iwe hilo tukio la kujisifia kwake linagusia siku ya kiama...?
kama ipo nipe hapa.
Allah akijisifia ufundi wake wa kuumba basi jua hilo linafidisha kabla ya kiama katika maisha ya kila siku.
kuhusu aya ulizotoa nimekujibu kweye ile comment kule juu niliedit.
aya nimezisoma nazijua hazina mafungamano yoyote ya ile aya.
aya hizo kweli zinaongelea kiyama ila hazina mafungamano na aya ya 88 hata kidogo.
aya zenyewe zinakwenda tofauti na ile aya ya 88.Aya ya 88 inasema ya kuwa USIONE milima imetulia HIYO INAKWENDA. kwa maana ina move..
sasa aya unazozitoa zinaenda kinyume na aya hiyo ati mfano
وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ
(ATTAKWIR - 3)
Na milima ikaondolewa,
hii haizungumzii kwenda kwa milima bali inazungumzia kuondolewa kwa milima milima ikiondolewa haiwezi kutembea.hivyo haina munasaba wa wazi hata kidogo..
na pia
وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا
(ANNABAA - 20)
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
na hii pia hvyp hivyo inazungumziwa kuondolewa kwa milima haina mafungamano na ile aya kule hii ni kama hyo ya attakwiyr
sasa hapa aya inaeleza SIKU ZITAKAPO..kwa maana wakati ujao sio leo hiyo
يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا
(ATT'UR - 9)
Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso,
umeona aya inaonesha wakati unaokuja sio leo na wakati huu. ile aya ya milima kutembea inaelzea wakati huu hapa tuliopo.
ikaenda tena ikasema..
وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا
(ATT'UR - 10)
Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
hii aya inasema milima itakwenda kwa mwendo mkubwa kinyume chake milima haitokwenda kwa mwendo mdogo.
aya hii inaelezea kiama ndio maaa ikasema itakuwa inakweda KWA MWENDO mkubwaa
na aya yetu ile imesema tu kwamba milima inakwenda kwa ufundi wa mweyezi Mungu. wala aya haikusema kama inakwenda kwa mwendo mkubwa au mdogo.
sasa aya hii ya 10 nxo inaelezea kiama ya kuwa milima itakuwa inakwenda kwa mwendo mkubwa tofauti na mwendo wake wa kawaida katika aya ya 88 ya annaml.
sasa sioni mafungamao ya hizo aya na ile aya ati kuwa ina, ungumzia kiama.
kama ni hivyo ipi maana ya Allah kusema kuwa milia inakwenda kama mawingu yanavyokwenda..?
hayo mawingu yanakwenda siku ya kiama au yanakwenda hapa nyaksti hizi kabla ya kiama..?