Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,375
- 14,870
Kijana Jua halizunguki hili weka akilini....jua ndilo linalozungukwa na vilivyomo kwenye mfumo wake....mfumo wa jua una sayari kadhaa ikiwemo dunia miezi kadhaa ukiwemo huu wa kwetu vimondo na takataka zingine zote zinalizunguka jua ambalo lina nguvu kubwa ya uvutano hivyo hakuna kinachotoka nje ya msari wake
Dunia hujizungusha yenyewe wakati huo huo ikilizunguka jua....mwezi nao unajizungusha wenyewe huku unaizunguka dunia hapo hapo inalizunguka jua pamoja na dunia
Ndio maana wakati fulani kunakuwa na kupatwa kwa jua ama mwezi kutokana na mizunguko yao
Jua ni nyota iliyo karibu na sisi nyota zingine zipo mbali sana nazo zina mifumo yao nayo huzungukwa vilevile ila siku zote nyota hazizunguki bali sayari na maumbo mengine
Mkuu, ninakuomba unapotaka kutoa hoja au kujibu swali mbele ya hadhara unatakiwa ufanye tafiti au uulize kwanza au ujisomee kabla ya kuwasilisha.
Nikwamba kila kitu kilichomo angani hakijatulia, yaani ama kinajizungusha, kinazunguka kitu kingine au kinaenda katika mwendo wa kawaida ( linear motion) kutoka sehemu moja kwenda nyingine, jua nalo linajizungusha hapohapo lilipo.
Na hayo ni matokeo ya "the big bang".