Naona unatumia mitindo dhaifu ya kimantiki kuhitimisha,leta dalili usiendeshwe na nadharia.
Hizo aya zinazungumzia siku ya Kiyama,na hii ndi kauli yenye nguvu mbele ya wanazuoni wa Tafsiri akiwemo Abul Fidah.
nimeweka ile comment ili kukukumbudha kwamba sio Mimi tu ndio nasema dunia inazunguka kwa mujibu aya bali hatashekhe abdallah sheikh alfarsiy naye kaona hivyo.
lakini tukija katika ayayenyewe namna ilivyokuja naomba kuuliza.
iko wapi kauli ya Mtume juu yaufafanuzi wa aya hiyo ?
au ha ulamaa waliosema ya kuwa kutembea huko ni siku ya kiama wameegemea dalili ipi ilhali aya inataja wakati uluopo "USIIONE IMETULIA, INAKWENDA "
vipi iwe siku ya kiama wakati aya inaleta habari hizi kwa lafdhi ya sasa hivi kjuu yakitendo hicho..?
lakini pia hata hizo kauli za ulamaa wanaokataa kuzunguka dunia badi ni dhaifu kwa sababu hazina munasaba wa kueleweka wa kuonesha kwamb aya ile inazungumzia siku ya kiama.
bali zinaendana kinyume,labda waliona aya zingine zimetaja milima wakaunganiha na hii aya ndi0o ikaonekana 8nazungumzia kiama.
tena aya zenyewe zinakwenda tofauti na ile aya ya 88.Aya ya 88 inasema ya kuwa USIONE milima imetulia HIYO INAKWENDA. kwa maana ina move..
sasa aya unazozitoa zinaenda kinyume na aya hiyo ati mfano
وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ
(ATTAKWIR - 3)
Na milima ikaondolewa,
hii haizungumzii kwenda kwa milima bali inazungumzia kuondolewa kwa milima milima ikiondolewa haiwezi kutembea.hivyo haina munasaba wa wazi hata kidogo..
na pia
وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا
(ANNABAA - 20)
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
na hii pia hvyp hivyo inazungumziwa kuondolewa kwa milima haina mafungamano na ile aya kule hii ni kama hyo ya attakwiyr
sasa hapa aya inaeleza SIKU ZITAKAPO..kwa maana wakati ujao sio leo hiyo
يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا
(ATT'UR - 9)
Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso,
umeona aya inaonesha wakati unaokuja sio leo na wakati huu. ile aya ya milima kutembea inaelzea wakati huu hapa tuliopo.
ikaenda tena ikasema..
وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا
(ATT'UR - 10)
Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
hii aya inasema milima itakwenda kwa mwendo mkubwa kinyume chake milima haitokwenda kwa mwendo mdogo.
aya hii inaelezea kiama ndio maaa ikasema itakuwa inakweda KWA MWENDO mkubwaa
na aya yetu ile imesema tu kwamba milima inakwenda kwa ufundi wa mweyezi Mungu. wala aya haikusema kama inakwenda kwa mwendo mkubwa au mdogo.
sasa aya hii ya 10 nxo inaelezea kiama ya kuwa milima itakuwa inakwenda kwa mwendo mkubwa tofauti na mwendo wake wa kawaida katika aya ya 88 ya annaml.
sasa sioni mafungamao ya hizo aya na ile aya ati kuwa ina, ungumzia kiama.
kama ni hivyo ipi maana ya Allah kusema kuwa milia inakwenda kama mawingu yanavyokwenda..?
hayo mawingu yanakwenda siku ya kiama au yanakwenda hapa nyaksti hizi kabla ya kiama..?