safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,169
- 15,851
- Thread starter
- #201
hiyo solar minimum ni sehemu au ni hali ambayo inapatwa na juaa tu hapo ilipo..?Ndiyo mkuu, nimeisoma hiyo ibara, licha ya mapungufu machache ya lugha iliyotumika lakini nimeielewa.
Tafsiri yake:-
Katika tahadhari ya kutisha, NASA inatabiri kwamba jua litafikia kile kiitwacho "Solar minimum" mwishoni mwa 2019 au 2020, na pindi hali hiyo itakapotokea, jua litatoa joto dogo sana kuliko kawaida, maana yake ni kwamba zebaki katika kipima joto (hapa duniani) itashuka na kupelekea kutokea kwa kipindi kirefu cha baridi (au vipindi vifupi vifupi vya baridi kwa muda mrefu katika uso wa dunia) jambo ambalo litaathiri hali ya hewa juu ya uso wa sayari (dunia):
Maoni yangu (maoni ya mleta ibara):-
Kama ni kweli (basi) tutakumbwa na masuala mazito juu ya sayari hii na maisha yatakuwa hovyo. (Mwisho wa tafsiri.)
Maneno yaliyomo kwenye mabano ni maneno yangu binafsi ili tafsiri inyooke.
Kesho na mimi nitatoa maoni yangu kuhusu hii kadhia.
Inshallah.
kwa sababu kama ikiwa ni sehemu maana yke wanakubali kwamba jua linakwenda lina move.
kwa sababu jua kitu hakiwezi kufikia kitu kingine mpaka kimoja wapo kiwe kina move.
sasa kusema kwamba sun will reach " linareach vipi na limekaa hapo hapo
na kama ni hali tu kama ilivyo ugonjwa kwa binadamu basi ntasitisha swali langu hapo juu