Dunia inategemea vipi mafuta na gesi ya Urusi? Tanzania itaathirika vipi?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,318
8,231
Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa zitazuia uagizaji wa mafuta kutoka Urusi.

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Urusi kuonya kuwa inaweza kukata usambazaji wa gesi kwa nchi za Ulaya ikiwa marufuku ya mafuta itaendelea.

Je, kuna vikwazo gani kwa mafuta na gesi ya Urusi?
Marekani imetangaza kupiga kusitisha marufuku ya uagizaji mafuta, gesi na makaa ya mawe nchini Urusi, baada ya Ukraine kutaka vikwazo kuongezwa.
Uingereza itaondoa mafuta ya Urusi mwishoni mwa mwaka huu, na EU inapunguza uagizaji wake kwa mbili ya tatu.

Serikali ya Uingereza imesema hatua hii inawapa muda wa kutosha kwao kupata wasambazaji wengine.

Naibu Waziri Mkuu wa Urusi Alexander Novak amesema kukataa mafuta ya Urusi kutasababisha "matokeo mabaya kwa soko la kimataifa".

Bei ya mafuta na gesi tayari imepanda kwa kasi na inaweza kupanda zaidi ikiwa Urusi itasimamisha mauzo ya nje.

Je, Urusi inasafirisha mafuta kiasi gani?
Urusi ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa mafuta duniani, baada ya Marekani na Saudi Arabia.

Kati ya mapipa milioni tano ya mafuta ambayo husafirisha nje kila siku, zaidi ya nusu ya hayo huenda Ulaya.

Marekani haitegemei sana, na takriban 3% ya mafuta yake yaliyoagizwa kutoka nje yanatoka Urusi mnamo 2020.

Vipi kuhusu wasambazaji mbadala wa mafuta ?
Ben McWilliams anasema inapaswa kuwa rahisi kupata wasambazaji wa mafuta mbadala kuliko gesi, "kwani sio mabomba mengi. Kuna mengine yanatoka Urusi lakini pia kuna usafirishaji mwingi kutoka sehemu nyingine".

Marekani imekuwa ikiitaka Saudi Arabia kuongeza uzalishaji wake wa mafuta, lakini ilipinga maombi ya awali ya Marekani ya kuongeza pato ili kupunguza bei ya mafuta.

Saudi Arabia ndio mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta, Opec ,shirika la mafuta ambalo linachukua takriban 60% ya mafuta yasiyosafishwa yanayouzwa kimataifa. Kwa sababu hii OPEC ina jukumu muhimu katika kushawishi bei ya mafuta.

Urusi haiko katika Opec lakini imekuwa ikifanya kazi nayo tangu 2017 kuweka mipaka ya uzalishaji wa mafuta, ili kudumisha mapato kwa wazalishaji.

Marekani pia inaangalia kulegeza vikwazo vya mafuta vya Venezuela. Ilikuwa muuzaji mkuu wa mafuta wa Marekani, lakini hivi karibuni Venezuela imekuwa ikiuza mafuta yake China.

Nini kitatokea ikiwa gesi ya Urusi itaacha kwenda Ulaya Magharibi?
Bei za kupasha joto - ambazo tayari ziko juu - zitaongezeka zaidi.

Gesi ya Urusi inachukua takriban 40% ya uagizaji wa gesi asilia wa EU.
Ikiwa hii itatimia, Italia na Ujerumani itakuwa hatarini sana.

Ulaya inaweza kuwageukia wasafirishaji wa gesi waliopo kama vile Qatar - au Algeria na Nigeria, lakini kuna vikwazo vya kivitendo vya kuongeza uzalishaji kwa haraka.

Urusi hutoa takriban 5% tu za usambazaji wa gesi wa Uingereza, na Marekani haiagizi gesi yoyote ya Urusi.
Hata hivyo, bei nchini Uingereza na Marekani bado ziko juu kwa kiasi kikubwa kutokana na athari kubwa ya uhaba wa usambazaji.

Je! mbadala wa gesi ya Urusi umeweza kupatikana?
Si rahisi sana.
"Ni vigumu kuchukua mbadala wa gesi kwa sababu tuna mabomba haya makubwa ambayo yanapeleka gesi ya Urusi kwenda Ulaya," anasema Ben McWilliams, mchambuzi wa utafiti wa sera ya nishati.

Taasisi ya Think tank Bruegel inatabiri kwamba ikiwa Urusi itasimamisha usambazaji wa gesi Ulaya, basi Ulaya itaweza kuagiza gesi asilia iliyoyeyuka kutoka Marekani.

Screenshot_20220309_211050.jpg

Inaweza pia kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati, lakini kufanya hivyo si jambo la haraka au rahisi.

"Mabadiliko huchukua muda kuanzishwa kwa hivyo katika muda mfupi hili sio suluhu," anasema mchambuzi wa utafiti Simone Tagliapietra.

"Kwa majira yajayo ya baridi - kinachoweza kuleta mabadiliko ni kubadili mafuta kama vile kufungua mitambo ya nishati ya makaa ya mawe, kama vile Italia na Ujerumani zina mipango ya kufanya katika kesi ya dharura."

EU imependekeza mpango wa kuifanya Ulaya kuwa huru kutoka kwa nishati ya mafuta ya Urusi kabla ya 2030 - ikiwa ni pamoja na hatua za kubadilisha usambazaji wa gesi na kuchukua nafasi ya gesi katika joto na uzalishaji wa nishati.

Je, nini kinaweza kutokea kwa gharama za kuongeza joto na mafuta?
Wateja watakabiliwa na kupanda kwa gharama za nishati na mafuta kutokana na vita hivi.

Nchini Uingereza, gharama za nishati za kaya zimedhibitiwa na bei ya juu ya nishati.
Lakini bili zitapanda kwa £700 hadi takriban £2,000 mwezi Aprili wakati kikomo kitakapoongezwa. Wanatarajiwa kufikia takriban £3,000 wakati itaongezwa tena msimu huu wa vuli.

Bei ya petroli na dizeli nchini Uingereza pia imepanda na petroli inatarajiwa kufikia 175p kwa lita huku vita vikiendelea.

Screenshot_20220309_211159.jpg

Nchini Marekani, gharama za petroli zimefikia viwango vyake vya juu zaidi tangu 2008, huku Shirika la Magari la Marekani likisema kuwa bei ya pampu iliongezeka kwa 11% katika wiki iliyopita.

"Nadhani ikiwa tuko katika ulimwengu ambao mafuta na gesi ya Urusi kuacha kwenda Ulaya basi tutahitaji kuwa na mgao," anasema McWilliams.

"Sehemu ya mazungumzo sasa ni, je tunaweza kuwaambia kaya kupunguza vidhibiti vyao vya halijoto kwa kiwango kimoja, ambacho kinaweza kuokoa sehemu kubwa ya gesi."
 
Na ndiyo matatizo ya nchi za magharibi,hwafikirii kuhusu hasara zitakazozipata nchi masikini kwa kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa zote bali wanajifikiria wao tu(self egoism)
 
Kuibadili gesi asilia yetu kuwa mafuta ya petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta hayo kutoka mataifa ya nje
 
Kuibadili gesi asilia yetu kuwa mafuta ya petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta hayo kutoka mataifa ya nje
 
Kuibadili gesi asilia yetu kuwa mafuta ya petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta hayo kutoka mataifa ya nje
 
Back
Top Bottom