Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,446
- 7,821
Nigeria ni nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani nyuma ya Angola, ilianza rasmi uchimbaji mafuta na kuyauza nje kibiashara mwaka 1956, kufikia mwaka 2000 mapato ya mafuta ghafi yalikuwa 98% ya mapato yote Nigeria iliyopata kwa kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi.
Pamoja na mafuta ghafi kuwa chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni Nigeria bado iliingia gharama kubwa kuagiza mafuta yaliyosafishwa kwa miaka yote.
Kiwanda cha Dangote kimeanza rasmi uzalishaji lakini bado kina safari kuelekea kuzalisha kwenye uwezo wake unaotarajiwa ili kutosheleza mahitaji ya ndani.
Ni safari ya zaidi ya miaka 68 kwa nchi hii iliyo magharibi mwa Afrika, tutegemee safari hii kwa gesi yetu kuweza kuifanya kimiminika(LPG) ili iweze kutumiwa kwa matumizi mbalimbali? Tanzania tunanunua gesi ya kupikia inayojazwa kwenye mitungi kwasababu tumeshindwa kuweka mitambo ya kuifanya LPG huku yetu tukiiuza nje!
Nchi za kiarabu ziliwezaje kutumia mafuta yake mapema na kuwatoa kwenye lindi la umasikini kufikia utajiri wa kiwango cha juu!