Duh... Netanyahu kayakanyaga aisee!

Duh... Netanyahu kayakanyaga aisee!

Alichokutana nacho hatathubutu tena kunyanyua mdomo kwa Iran hata kama USA kamuahidi kumlinda, Israel imevunjwa vunjwa siyo mchezo na wao wameshindwa kwenda kuharibu Uranium ya Iran japo ndo ilikua lengo ila wamefeli wameishia kupiga mahandaki matupu, Iran wanaenda kumiliki Nuclear ndani ya muda mfupi kwanzia sasa
Huu ndio.ukweli
 
Hawa wanaosherekea Sasa hivi ndio walikuwa wanapangwa wa wapindue nchi na netanyau kichaa
******
 

Attachments

  • IMG_20250624_161633_740.jpg
    IMG_20250624_161633_740.jpg
    179.8 KB · Views: 7
Muirani ndio anataka muende miaka 3 on battle tuone matokeo huwezi kusinamisha vita mapema hivi daaah
Kama Iran anataka vita ya miaka mitatu si aanzishe upya?

Israel ilitaka kulipua vinu vya nyuklia na imemaliza kazi. Ni kazi ya Iran sasa kuifuta Israel.
Ngonjera nyingi ila vitendo zero.
 
Kama Iran anataka vita ya miaka mitatu si aanzishe upya?

Israel ilitaka kulipua vinu vya nyuklia na imemaliza kazi. Ni kazi ya Iran sasa kuifuta Israel.
Ngonjera nyingi ila vitendo zero.
Kwahio kuanzia Leo tusijekusikia Iran ana nyuklia Tena kwakua kazi mumeimaliza sawa,? Tukisikia mna anzisha maneno maneno maana yake mnatafuta kingine Iran hana nyuklia na program imefungwa rasmi.
 
Sawa, mleta mada hebu niambie Israel ameshaharibu sehemu zote alioona zilikuwa zikichangia kwa asilimia nyingi kumsaidia iran kukamilisha mpango wake wa Nuclear, na watu muhimu kawaondoa.

Sasa nakuuliza ulitaka apige makazi ya watu maana hicho ndicho kilichobakia! Mimi sioni kingine...

Na Labda hapa ungesema wameshindwa kumuondoa Ayatollah.

Na labda pia waIran hawakuwa na utayari kufanya mapinduzi.

Hayo mawili nafkiri yangeeleweka zaidi, yani Israel kucheza kwenye Anga la Irani akipiga kila anachotaka, na sijaskia kuna ndege ya Israel imedondoshwa, na huku Iran akimpiga Israel na kupiga anachopata nafasi ya kupiga, na unasema Iran mshindi?

Unafikiri Israel ingeenda kwa mfumo wa kubutua chochote anachokutana nacho huko Iran pangebaki salama?
Iran kashinda vita , Israel na USA wameomba amani baada ya kuona mziki wa Iran ni mzito kuliko walivyotegemea, ingekua Israel kashinda hii vita angeendelea kuishambulia Iran kama anavyofanya Gaza hadi leo bado anaua watoto, ila huo ujinga umemtokea puani.

Kuhusiana na kwenda kuharibu mpango wa Nuclear wamefeli vilevile wamepiga vinu lakini hamna mafanikio yoyote hamna leakage yoyote ya Uranium wala mionzi yoyote iliyovuja, ingekua kweli wamefanikiwa kuharibu leo hii ungeshasikia watu wamekufa huko Iran kutokana ma athari ya Nuclear iliyoshambuliwa, ila hali ni shwari wananchi wa Qom wanaoishi karibu na Fordow wako salama wanaendelea na mishe zao na wako karibu na kinu cha Nuclear kilichopigwa, maana yake shambulio limefeli
 
Sasa unajua lengo la Israel lifetime?
Yes tunajua lengo la Israel lilikuwa kuichapa Iran. Lakini cha kushangaza Israel ndo ilianza kuchapwa mpaka Marekani akaja kusaidia ili kuiepusha na kipigo.
 
Iran sio Palestina tuliwaambia nyie hamkusikia, Kilichompata Netanyau anajutia ujinga wake, hana hata lengo moja alilofanikisha, Ila Iran amekamilisha malengo yote, ndio maana Trump anataka hii vita isimame maana Israeli inaenda kuangamizwa na Iran.
💯
 
Niaje waungwana

Nafikiri mashambulizi ya mwaka jana kati ya Iran na Israel, yalimpofusha sana Netanyahu kwa kuamini kwamba Iran ilikuwa na silaha chache, na dhaifu kwa kuweza kufanya maangamizi katika ardhi ya Israel.

Ikumbukwe kwamba katika mashambulizi yale Iran alitumia makombora ya kawaida na ya masafa mafupi, hivyo hata madhara na uharibifu wake huko Israel haukuwa mkubwa kivile, hali iliyomfanya Netanyahu aamini kwamba Iran haina silaha za maana za kupambana nae, lakini pia aliamini kwamba Iron dome na Thaad zikiongezwa na kurekebishwa vizuri, basi muajemi atachapika vizuri bila kurusha au kuingiza chochote katika ardhi ya Israel.

Masikini, jamaa hakujua kwamba Ayatollah alikuwa anampimia upeo wake wa akili ulipoishia. Akaenda Marekani kuonana na Trump kisha wakapanga namna watakavyoivamia Iran, kutawala anga, na kuzuia kombora kurushwa nchini kwao Israel.

Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Neta akaanza uvamizi kwa mashambulizi ya kushtukiza huku wakiwa wameshajipanga na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na washirika wengine kuzuia mashambulizi ya Iran kwenda Israel. Mpaka hapo walikuwa wanajua Iran haina silaha au makombora ya maana ya kupenya ulinzi wao. Kwa bahati mbaya hali ikawa tofauti na walivyotarajia.

Vinu vikaanza kutumwa Israel katika speed na nguvu ya ajabu kiasi ya kwamba Iro dome na Thaad zao zikabaki kama maonesho tu au mavyuma ya kukamatia kumbi kumbi. Iron dome balada ya kuzuia kombora, inazuia nzi na upepo.

Netanyahu akaona maji yamezidi unga, kinachozuiwa hakionekani, akamwambia baba yake Trump aingilie kati. Baba na yeye kuingilia kati kaishia kupiga hewa, huku mzigo ukiwa umeshahamishwa zamani. Baada ya hapo wakafikiri hilo tukio linamfanya muajemi aogope au kusalimu amri, badala yake ikawa kama vile wamempeleka mzaramo mkoleni. Yani ndo amezidisha mashambulizi na kuigeza Tel Aviv kama Mogadishu.

Baada ya plan kushindwa eti wameamua kuomba poo kwa kutaka vita isimame. Muajemi hataki kusikia hilo, bado anaendeleza kipondo tu huko Israel. Japo wao ni mabingwa wa kuficha taarifa, lakini ukiona Trump anakimbilia kutaka mapigano yasitishwe au vita iishe basi ujue ameona madhara makubwa mno yaliofanywa na Iran huko Israel. Maana ni yeye ndio alikuwa anasema eti waachwe waendelee kuchapana. Sasa imekuaje tena kutaka vita isimame. Za kuambiwa changanya na zako.

Vita sio poa. Nina imani Netanyahu anajuta kuanzisha huu mzozo na vita ikisimama naamini hatokuja tena kuigusa Iran kindezi ndezi vile.

Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo. Fikiria leo hii Trump anapambana ili vita iishe. Ujue kuna jambo kubwa limetokea huko Israel halitakiwi kusemwa 🤣🤣🤣
Afu kuna kenge wanasema Iran ndio kaomba vita kusimama hahaha mimi na uhakika Iran angetaka yeye kusimamisha vita US na Israel wangekataa kabisa mpaa wabadilishe regime kama wanavyo dai 🤣
 
Ushahidi uliotolewa na shirika la nguzu za atomic mitambo ya Iran ya nyuklia ipo sama, hakuna dalili yoyote kua mitambo hiyo imeathirika, America mwenyewe ameshindwa kuleta madhara yoyote katika shambuluo lake, achana na huyo Israeli uwezo wake kwa Iran umedhihirika ni mdogo sana, hata Iran mwenyewe haihofii tena Israeli na ndio sababu Trump anataka hii vita isimame, maana Israeli hana uwezo tena wa kabiliana na Iran kwa hali yoyote. Msilolijua Iran hii vita amejiandaa nayo kwa muda mrefu, kitu ambacho Israeli hawezi kwenda nayo hata mwezi mmoja atakua amesha tepepeta vibaya sana
Perfect.. umeandika point tupu mkuu 👍
 
Unaongea kitu gani hapa?
Umeelewa post yangu nilokujibu?

Nimekuambia vile Israel ilikuwa inalenga, sasa Yeye anaona amekamilisha, wewe unasema vita ya mwezi, kwani alikuambia anataka kupigana au anataka kukomesha mambo ya Nuclear?

Elewa tofauti hapo...!!!
Unaweza kulenga kitu lakini ukakosa shabaha ya kufikia malengo, mwisho wa siku ukaamua kuachana na mission yako ambayo unaona umeshindwa kuendelea nayo kutokana na cost fulani.

Hivyo hivyo kwa Israel ilitaka kuharibu, lakini Iran walilifahamu hilo mapema kabla ya shambulizi na kuamua kuhamisha kila kitu. Kumbuka kabla ya shambulizi Israel ilikuwa imesha ahidi mapema kuwa utashambulia mifumo ya nyuklia ya Iran. Hivyo Iran sio wapumbavu wa kusubiri waje washambuliwe vinu vyao walivyovitengeneza muda mrefu na kwa gharama kubwa. Hivi mtu akikwambia kwamba mimi napanga kuja kuiba tv yako nyumbani kwako, wewe utakosa njia ya kuepusha mapema wizi huo kwa kutafuta sehemu salama ambayo mwizi akifika hawezi kuiona?

Una uhakika gani kama kweli walifanikiwa kushambuliwa na wakati wataalam wanaoshughulika na mambo ya nyuklia wameona hakuna madhara yoyote yaliofanyika katika maeneo yalioshambuliwa hivyo hakuna hatari yoyote inayoweza kusababishwa na shambulizi lile. Kumbuka sehemu yenye mionzi ya nyuklia ikishambuliwa lazima athari kubwa itokee kutokana na sumu itayosambaa kwa upepo. Ila kwa Iran hakuna madhara yoyote kwa watu wanaozunguka eneo la Nyuklia, hii inamaanisha kuwa wakati wa shambulizi hakuna kitu kilichokuwa ndani ya kiwanda cha nyuklia.

Sema Israel iliona kile ilicholenga kimeshindikana na kwa upande mungine yeye ndo anaechezea kichapo zaidi ya kile wanachopata Iran.
 
Yes tunajua lengo la Israel lilikuwa kuichapa Iran. Lakini cha kushangaza Israel ndo ilianza kuchapwa mpaka Marekani akaja kusaidia ili kuiepusha na kipigo.
Kwahiyo vinu vya nyuklia bado vipo
 
Afu kuna kenge wanasema Iran ndio kaomba vita kusimama hahaha mimi na uhakika Iran angetaka yeye kusimamisha vita US na Israel wangekataa kabisa mpaa wabadilishe regime kama wanavyo dai 🤣
Wanajifariji tu mkuu, lakini mioyoni wanakiri kuwa waligaragazwa vibaya sana na Iran. Hii vita imempa heshima na ushindi mkubwa Iran kiasi ya kwamba hata alipozichapa kambi za Marekani huko kwa waarab wote walikaa kimya, maana waliogopa kufungua mdomo wangebondwa wao, Israel pamoja na Mmarekani wao.
 
🌟❗️Israeli security expert Yossi Melman:

▪️An Iranian missile destroyed 7 buildings in one location

▪️Iranian missiles have the ability to destroy underground concrete structures

▪️i24 News Network: Israeli Home Front Command research has shown that Iranian missiles are also capable of targeting underground concrete rooms and buildings
 
Netanyahu kweli amshukuru Trump kamukoa na Trump alitumia akili kuto kujibu kipigo cha Iran.

Mtu mwenye akili atajiuliza kwanini USA aliwaondoa askari zake kama si kumuogopa Iran. Mtu mwenye akili pia atasema Iran kapiga base na alijua haina askari ni sababu ya kumdhalalisha USA, Iran imetoa message sisi tumepiga base yenu hio iwe na askari au hakuna ni kama wamepiga ndani ya USA. Watu lazima wafahamu base ya Al Ouded ni katika base kubwa ya USA iliopo nje ya USA.

Kuhusu Israel katoka kapa hata CNN wanasema Nuclear facilities za Iran zote hazikudhurika sana na hasa ile Fowdar kwa hio Israel hakugain sana kabahatika kuwauwa viongozi wa kijeshi kwa sababu miaka 20 alijiandaa kuipiga Iran kwa kuingiza drones na maboom Iran kwa kutumia nchi za Europe na Wairan wenye asili ya kiyahudi na wapinzani lakini katoka kapa. Hakuweza pindua, hakuweza kuzidestroyed Missiles za Iran. THAAD, IRON DOME, HEGS defense system zote zimefailed.

Missiles za Iran zime proved ni one of the best Missiles 👌
 
Kama Iran anataka vita ya miaka mitatu si aanzishe upya?

Israel ilitaka kulipua vinu vya nyuklia na imemaliza kazi. Ni kazi ya Iran sasa kuifuta Israel.
Ngonjera nyingi ila vitendo zero.
Hivyo Iran hana Nuclear tenaaa????
 
Alichokutana nacho hatathubutu tena kunyanyua mdomo kwa Iran hata kama USA kamuahidi kumlinda, Israel imevunjwa vunjwa siyo mchezo na wao wameshindwa kwenda kuharibu Uranium ya Iran japo ndo ilikua lengo ila wamefeli wameishia kupiga mahandaki matupu, Iran wanaenda kumiliki Nuclear ndani ya muda mfupi kwanzia sasa
Nakubaliana na wewe kwa 100% mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom